Friday, 27 October 2017

Simba kutua Dar kwa ndege za kukodi

Simba kutua Dar kwa ndege za kukodi

Kikosi cha Simba kinatarajia kurejea jijini Dar es Salaam leo kwa maandalizi ya mwisho ya mechi yao ya kesho dhidi ya Yanga.

Simba walikuwa kambini mjini Zanzibar kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Taarifa zinaeleza, Simba watawasili kwa kutumia ndege za kukodi tayari kwa ajili ya mechi hiyo.

Kikosi hicho kitaingia kambini jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.


Hata hivyo, Simba wamekuwa wakifanya uficho kuhusiana na sehemu watakayokaa jijini Dar es Salaam wakimalizia maandalizi yao hayo ya mwisho kabla ya kesho.

Maneno ya Christina Shusho kwa viongozi Tanzania

Maneno ya Christina Shusho kwa viongozi Tanzania

Msanii wa muziki wa Injili Tanzania Christina Shusho, amewataka watanzania kuwaombea viongozi wetu wa kitaifa, kwani tuna kila sababu ya kujivunia watu hao kutokana na uongozi wao uliotukuka.

Christina Shusho ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio, na kusema kwamba Tanzania tuna bahati kupa viongozi wenye hekima ambao wanaliongpoza taifa kwa amani, tofauti na nchi zingine za jirani kwa Afrika Mashariki.

"Najivunia sana viongozi wetu, tena niwaambie tu watanzania tuwaombee sana, tuna bahati ya kupata viongozi wenye upendo, na pia tudumishe upendo wetu tuwe na subira kwenye mambo yetu tudumishe hii amani, Mungu ametupendelea sana nchi za wenzetu wanalia na amani yao", amesema Christina Shusho.

Kauli hiyo ya Shusho imefuatia baada ya kuporomoshewa matusi na wakenya, kutokana na mihemko waliyonayo kipindi hiki cha uchaguzi, na kusema kwamba Wakenya wanahitaji  maombi pia kwani wanapitia kipindi kigumu.

Wauawa kwa Mapanga Usiku

Wauawa kwa Mapanga Usiku

Mume na mke wameuawa kwa kukatwa mapanga wakiwa wamelala nyumbani kwao.

Wanandoa hao walikuwa na kesi mbili za kugombea ardhi katika baraza la aridhi la Kata ya Hunyari, Tarafa ya Chamriho wilayani Bunda.

Ofisa Tarafa ya Chamriho Boniphace Maiga, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 22, mwaka huu.

Aliwataja waliouawa  kuwa ni Magina   Masengwa (61) na mke wake, Sumaye Sebojimu (58) ambao wote ni wakazi wa kitongoji cha Kiborogota Kijiji cha Mariwanda wilayani Bunda.

Maiga alisema   wanafamilia hao walivamiwa usiku na watu wasiojulikana na wakiwa wamelala na kukatwa mapanga kabla ya wavamizi hao  kutoweka na kuacha maiti za watu hao ndani ya nyumba hiyo.

Maiti hao waligundulika kesho yake asubuhi na mjukuu wao aliyekuwa anakwenda shambani.

“Ofisi yangu ilipokea taarifa ya mauwaji hayo kwamba watu wawili mume na mke wameuawa kwa kukatwa mapanga.

“Kwa hiyo chanzo cha mauaji hayo inasadikika huenda kinatokana na mgogoro wa shamba kwa sababu  walikuwa na kesi mbili katika baraza la ardhi la Kata ya Hunyari,” alisema Maiga.

Alisema   polisi walimkamata   Nyangi Nyabirumo, mkazi wa kijiji hicho kwa mahojiano na anaendelea kushikiliwa Kituo cha Polisi Wilaya ya Bunda.

Maiga alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.

Alisema  hali hiyo inaweza kusababisha upande wa pili nao kukasirika na kulipiza kisasi jambo ambalo  ni kinyume cha sheria.

Burundi yajiondoa rasmi katika mahakama ya ICC

Burundi yajiondoa rasmi katika mahakama ya ICC

Rais Nkurunziza alichukua madaraka kwa awamu ya tatu, licha ya kuwepo kwa kipindi cha mihula miwili katika katiba ya taifa hilo.

Burundi limekuwa taifa la kwanza mwanachama wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa jinai kujiondoa katika mahakama hiyo.

Serikali ya taifa hilo la Afrika ya kati liliuarifu Umoja wa Mataifa UN kuhusu hatua hiyo mwaka mmmoja uliopita , na hii leo kujitoa kwao kunaanza kuidhinishwa rasmi.

Inaonekana kama kipimo cha jamii ya kimataifa kuhusu haki.

Ni hatua sio ya kawaida.

Je kutakuwa na athari zake na ni kwa nini ni muhimu?.

Kulingana na mwandishi wa BBC Anna Holligan kujiondoa kwa Burundi ni majuto makubwa.

Mahakama ya ICC imeanza kutathmini iwapo inaweza kuchunguza ghasia za kisiasa zilizoibuka baada ya rais Nkurunziza kuchukuwa madaraka kwa awamu ya tatu, licha ya kuwepo kwa kipindi cha mihula miwili katika katiba ya taifa hilo.

ICC bado ina uwezo kuchunguza uhalifu uliotekelezwa wakati Burundi ilipokuwa mwanachama wa mahakama hiyo.

Lakini haiwezi kuchunguza uhalifu wowote wa siku zijazo.

Hatua hiyo inaweza kuwa mfano na kuonyesha viongozi wengine kwamba kujiondoa katika mahakama hiyo ni njia mojawapo ya kuepuka jicho la kimataifa hadi pale Jamii ya kimataifa itakapochukua hatua na taasisi kama vile Umoja wa Afrika ama baraza la usalama la umoja wa mataifa litakapowafuatilia washukiwa na kuyakumbusha mataifa kwamba kujiondoa katika ICC hakumaanishi moja kwa moja kwamba waathiriwa hawatopata haki.

Simba vs Yanga kufa na kupona kesho

Simba vs Yanga kufa na kupona kesho

MECHI za Ligi Kuu Bara z i n a t a r a j i a kuendelea wikiendi hii kwa mzunguko wa nane kuchezwa, huku miamba miwili ya soka Tanzania, Simba na Yan­ga ikitarajia kukutana kwenye Uwanja wa Uhu­ru jijini Dar es Salaam, kesho Jumamosi.

Mchezo huu unatara­jiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na timu hizo kuwa katika nafasi sawa ya msimamo wa ligi licha ya Simba kuongoza kwa idadi ya mabao ya kufunga, huku kila moja ikihitaji kukaa kileleni.

Mechi hii inatarajiwa kuwa ni ya vita na kisasi kutokana na hali jinsi ilivyo katika mechi husika ambapo kila upande utahitaji ku­fanya vyema.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yanatarajiwa kuifanya mechi hiyo kuwa ni ya vita na kisasi.

MAKOCHA KUTETEA VIBARUA VYAO
Imekaa vibaya kwa upande wa makocha wa timu zote mbili, kutokana na historia za timu hizo ambapo mara nyingi makocha wamekuwa wakifungashiwa vi­rago vyao pale wanapofungwa na wapinzani wao.

Hivi karibuni kulizuka uzushi juu ya Yanga kutaka kumuondoa ko­cha wake, George Lwandamina kutokana na matokeo mabaya katika mechi za awali jambo am­balo uongozi wa klabu hiyo ulika­nusha, lakini waswahili husema lisemwalo lipo, hivyo mechi hiyo inaweza kuwa katika wakati mgu­mu kwa upande wake.

Vilevile kwa upande wa Simba, Kocha Joseph Omog amekalia kuti kavu kwa muda mrefu kuto­kana na uongozi wa klabu hiyo kutaka kumuondoa kutokana na madai ya kutokifundisha vyema kikosi hicho kwa kuona kuwa kimemzidi uwezo, lakini mkataba aliosaini umeonekana kumbeba kutokana na baadhi ya vipengele kuwabana waajili wake.

Hivyo basi, mechi hii ndiyo itakayotoa maamuzi juu ya kuen­delea kuwepo katika kikosi hicho kwa kuwa inadaiwa kuna kipenge­le alichosaini kinaeleza kuwa iwapo t i m u haitaongoza msimamo wa ligi, itawapa nguvu viongozi kuweza kuvunja kandar­asi hiyo.

Mshambuliaji wa Simba, Haruna Niyonzima akiopambana na wachezaji wa Simba.
Hivyo, atakuwa na kibarua kigumu kuhakikisha anafanikiwa kushinda mchezo huo ambao utakuwa na upinzani mkubwa.

KILA TIMU ITAHITAJI KUKAA KILELENI
Simba na Yanga zimefungana katika msimamo wa ligi kuto­kana na zote kuwa na pointi 15, huku Simba ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga. Simba ina mabao 19 na Yanga ina mabao 10.

Hivyo, kutokana na jinsi msi­mamo ulivyo, timu ambayo itashinda katika mchezo huo ndiyo itakayopata nafasi ya kuongoza msimamo wa ligi na iwapo itatokea wakatoa sare na Mtibwa Sugar yenye pointi 15 ikishinda mechi yao ya Ju­mapili dhidi ya Singida United basi itakaa kileleni.

KUONYESHANA UBORA WA VIKOSI
Kila timu inajinadi kuwa na kikosi bora ambacho imekisa­jili msimu huu, hivyo mashabiki wanasubiri kwa hamu kubwa kuona timu gani itaonyesha ufundi zaidi katika mchezo huo.

AJIBU, NIYONZIMA & OKWI VIVUTIO
Kwa sasa habari ya mjini ka­tika timu hizo ni kuhusiana na viwango vya wachezaji Ibrahim Ajibu wa Yanga na Haruna Niy­onzima na Emmanuel Okwi wa Simba, hivyo kila mmoja atahi­taji kuona wanafanya nini ka­tika mechi hiyo ya kesho.

Kwa upande wa Okwi, ndiye mchezaji kinara wa mabao kwenye ligi akiwa na mabao nane ambayo yameifanya kiko­si hicho kukaa kileleni kwa to­fauti ya mabao.

Aidha, wachezaji Ajibu na Niyonzima, kwa sasa ni gumzo kutokana na viwango wana­vyoonyesha. Mashabiki wa timu hizo wamekuwa waki­rushiana maneno huku wale wa Yanga wakidai Simba wamepoteza mchezaji (Ajibu) kwani amekuwa muhimu Jang­wani na Niyonzima akipondwa kwa kuonyesha uwezo wa ka­waida tofauti na ule aliokuwa akionyesha Yanga.

HOFU YA MASHABIKI
Hofu kubwa ya mashabiki kuelekea mchezo huo, itakuwa namna ya kuingia uwanjani kwani kwa muonekano wa haraka Uwanja wa Uhuru jinsi ulivyo hauwezi kukidhi mahitaji ya mashabiki kutokana na udo­go wa uwanja huo tofauti na ule wa Taifa ambao ni mkubwa.

Kuna uwezekano mkubwa kwa mashabiki wengi kuanga­lia mpira huo kupitia runinga kutokana na kushindwa ku­ingia uwanjani licha ya kuhitaji kuwaona wachezaji ‘live’ uwan­jani.

Dongo la Haji Manara

Dongo la Haji Manara

TIMU ya Simba leo imetua kwa ndege jijini  Dar wakitokea Unguja walipokuwa wameweka kambi ya wiki moja kabla ya mchezo wa kesho na watani wao wa jadi, Yanga SC.

Timu hiyo imepokelewa na viongozi mbalimbali wa Simba wakiongozwa na msemaji wa timu hiyo, Haji Manara, huku akirusha kijembe kwenda kwa watani hao  kupitia akaunti yake ya Instagram akisema: Mara paap,,tumetua dar,,,,okey mnaweza kupitia njia ya kilwa,,au ya kisarawe,,au daraja la kiluvya lishajengwa??Swaumu oyeeeee😊😊

Diamond Azua Gumzo Mitandaoni Baada Ya Kuonekana Akimpiga Kiss Mtoto Wake Wakike,,,,


MAGAZETI YA LEO 27 OCTOBER








Audio | Qboy Msafi Ft Mr Blue _ Kamoyo | Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/285110/by/g0k
8FWrgxq

Audio | Bracket Ft Korede bello _ Just Like That | Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/285158/by/OkoOtyDjTu

Audio | Coyo _ Tulipotoka | Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/285103/by/_zrbwPKpuO