Thursday, 8 February 2018

Diamond, Mobeto wamaliza fofauti zoa

Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond amesema mazungumzo katika kesi yake Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto kati yake na mwanamitindo Hamisa Mobeto,  imekwenda vizuri.

“Niseme tu mambo yameenda vizuri na kama mnavyojua mambo ya mahakamani ikitokea ninahitajika nitakuja,” amesema.

Diamond alifika mahakamani hapo leo Februari 8, 2018  kusikiliza kesi inayomkabili ya matunzo ya mtoto Prince Abdul iliyofunguliwa na Mobeto.

Amesema yeye na Mobeto hawana shida yoyote, ila kuna watu waliokuwa wakizungumza maneno na kumchochea Mobeto.

"Tunahitaji kuweka mambo sawa. Tunahitaji kuwa katika mstari kwa sababu vitu vidogo vinaharibu upande wa mama na upande wa baba kwa hiyo tulikuwa tunaweka mambo sawa ili kesho na keshokutwa yasilete sintofahamu baina yetu,” amesema na Diamonda na kuongeza:

“Ikitokea kuna mtafaruku baina ya mtoto, kila mtu anakuwa na mawazo yake, kwa hiyo ni lazima kumjenga mtoto na kuhakikisha kuwa mtoto anajengwa na kulelewa  katika malezi bora.”

Alipoulizwa ni kiasi gani cha fedha anachoweza kumudu kutoa kwa ajili ya matunzo ya mtoto huyo, amesema kiasi cha fedha kinazungumzwa zaidi lakini mtoto anahitaji matunzo mengi.

"Kiasi cha pesa tunachoandika sehemu kama hizi tunazungumza tu. Mtoto ana mahitaji mengi wakati mwingine mtoto wako unaweza kumpa hata Sh100 milioni. Huwezi kusema siwezi kumpa kwa sababu niliandikisha nitampa Sh100,000. Tumeweka mazingira mazuri ya kiasi kitakachomfanya akue katika malezi bora,” amesema.

Msanii huyo amesema kupitia kesi hiyo amejifunza vitu vingi na kwamba,  mazungumzo yao ndani ya mahakama hiyo ni siri yao: “mambo yamekwisha.”

Amesema atahakikisha mtoto huyo anakuwa katika mazingira mazuri, kumsomesha kadri ya uwezo wake utakavyoruhusu kwa maelezo kuwa maisha ni kupanda na kushuka.

“Kuna wakati unakuwa hauna unasema leo mie sina basi mambo yanakuwa Bundasiliga leo mnakula mihogo maisha ndivyo yalivyo,” amesema.

Wabunge ANC wakutana kumjadili Zuma

Afrika Kusini.  Kamati ya Bunge ya Chama cha ANC (caucus) inakutana mchana huu katika kikao cha siri ambacho hata hivyo ajenda zake hazikuwekwa wazi kwa waandishi wa habari.

Kamati hiyo inakutana huku kukiwa na shinikizo linalomtaka Rais Jacob Zuma kuachia madaraka.

Duru za habari zinasema kiongozi mkuu wa ANC, Cyril Ramaphosa ndiye atayehutubia kikao cha kamati hiyo inayokutana mjini Cape Town.

Maofisa wa chama hicho hawakuwa tayari kueleza ajenda muhimu za mkutano huo wa dharura mbali ya kusisitiza kuwa ni mkutano wa ndani.

Hata hivyo, taarifa zinasema wabunge hao huenda wakajadili suala la kuondoka madarakani kwa Rais Zuma na kipindi cha mpito kuelekea katika uchaguzi mkuu mwakani.

Awali, Ramaphosa amesema amekuwa akifanya  mazungumzo ya moja kwa moja na Rais Zuma kuhusiana na kipindi cha mabadiliko na masuala yanayohusu wadhifa wa rais wa nchi hiyo.

Zuma ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009 na ambaye anakabiliwa na madai ya ufisadi amekuwa na nafasi finyu ya ushawishi tangu Ramaphosa arithi nafasi ya kiongozi mkuu wa ANC.

Katika taarifa, Ramaphosa amesema yeye na Zuma wanatarajia kukamilisha mazungumzo na waifahamishe nchi kuhusiana na mazungumzo katika siku zijazo.

 Amesema mazungumzo hayo ni nafasi ya kutafuta suluhisho bila kuleta mgawanyiko nchini humo.

Wabunge ANC wakutana kumjadili Zuma

Afrika Kusini.  Kamati ya Bunge ya Chama cha ANC (caucus) inakutana mchana huu katika kikao cha siri ambacho hata hivyo ajenda zake hazikuwekwa wazi kwa waandishi wa habari.

Kamati hiyo inakutana huku kukiwa na shinikizo linalomtaka Rais Jacob Zuma kuachia madaraka.

Duru za habari zinasema kiongozi mkuu wa ANC, Cyril Ramaphosa ndiye atayehutubia kikao cha kamati hiyo inayokutana mjini Cape Town.

Maofisa wa chama hicho hawakuwa tayari kueleza ajenda muhimu za mkutano huo wa dharura mbali ya kusisitiza kuwa ni mkutano wa ndani.

Hata hivyo, taarifa zinasema wabunge hao huenda wakajadili suala la kuondoka madarakani kwa Rais Zuma na kipindi cha mpito kuelekea katika uchaguzi mkuu mwakani.

Awali, Ramaphosa amesema amekuwa akifanya  mazungumzo ya moja kwa moja na Rais Zuma kuhusiana na kipindi cha mabadiliko na masuala yanayohusu wadhifa wa rais wa nchi hiyo.

Zuma ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009 na ambaye anakabiliwa na madai ya ufisadi amekuwa na nafasi finyu ya ushawishi tangu Ramaphosa arithi nafasi ya kiongozi mkuu wa ANC.

Katika taarifa, Ramaphosa amesema yeye na Zuma wanatarajia kukamilisha mazungumzo na waifahamishe nchi kuhusiana na mazungumzo katika siku zijazo.

 Amesema mazungumzo hayo ni nafasi ya kutafuta suluhisho bila kuleta mgawanyiko nchini humo.

Tigo wapunguza gharama

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo imepunguza gharama za kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kitaifa na kimataifa kwa asilimia 27.5.

Takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kuwapo kwa punguzo hilo katika robo ya nne ya mwaka iliyoishia Desemba 2017 ikilinganishwa na robo ya tatu ya mwaka ulioishia Septemba.

Ripoti ya robo ya tatu ilionyesha kuwa Tigo ndiyo mtandao wenye gharama kubwa Tanzania katika kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi kitaifa na kimataifa jambo ambalo limekuwa tofauti na robo ya nne ya mwaka.

Katika robo ya tatu ya mwaka wateja wa Tigo walikuwa wakilipia Sh360 kwa dakika (kabla ya VAT) katika kupiga simu ndani ya mtandao ambayo imeshuka hadi kufikia Sh261 katika robo ya nne ya mwaka, ikiwa ni pungufu ya Sh99 sawa na asilimia 27.5.

Hata hivyo, kushuka kwa gharama za kupiga simu ndani ya mtandao katika robo ya nne, takwimu zinaonyesha kuwa  tozo za Tigo bado zipo juu ya wastani wa gharama za kupiga simu ambazo ni Sh249 kwa dakika.

Katika kupiga simu nje ya mtandao wateja wa Tigo walikuwa wakilipia Sh480 kwa dakika katika robo ya tatu ya mwaka ambayo imeshuka hadi kufikia Sh348 ambayo ni sawa na pungufu ya asilimia 27.5.

Licha ya kuwapo kwa punguzo hilo, tozo hiyo bado ipo juu ya wastani wa gharama za kupiga simu nje ya mtandao ambazo ni Sh329 kwa dakika.

Katika kupiga simu Afrika  mashariki wateja wa Tigo walikuwa wakilipia Sh1,022 kwa dakika katika robo ya tatu ya mwaka ambayo imepungua hadi kufikia Sh739 katika robo ya nne ya mwaka ikiwa ni pungufu ya Sh283 sawa na asilimia 27.7.

"Kupungua kwa gharama hizo kumeifanya Kampuni ya Tigo kuwa miongoni mwa kampuni zinazotoza tozo iliyo chini ya kiwango cha wastani ya kupiga simu Afrika ya Mashariki ambayo ni Sh745 kwa dakika,"amesema.

Katika kupiga simu kimataifa, Tigo ilikuwa ikitoza Sh1,737 katika kupiga simu kwa dakika katika robo ya tatu ya mwaka ambayo imepungua hadi kufikia Sh1,258, ikiwa ni pungufu ya Sh479 sawa na asilimia 27.6.

Kupungua kwa gharama hizo kunaifanya Tigo kuwa chini ya wastani wa tozo za kupiga simu kimataifa ambayo ni Sh1,273.

Kutuma ujumbe mfupi
Katika kutuma ujumbe ndani ya mtandao, Kampuni ya Tigo imepunguza gharama hadi kufikia Sh51 katika robo ya nne ya mwaka kutoka Sh70 iliyokuwapo katika robo ya tatu ya mwaka, hiyo ni sawa na pungufu ya Sh19 sawa na asilimia 27.14.

Tozo hizo za kutuma ujumbe mfupi ziko sawa na wastani uliowekwa  wa Sh51 kwa kila ujumbe.

Katika kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kimataifa gharama imepungua hadi kufikia Sh156 katika robo ya nne ya mwaka kutoka Sh 215 ya robo ya tatu ya mwaka ikiwa ni pungufu ya Sh59 sawa na asilimia 27.4.

Gharama hizo ziko juu ya wastani wa tozo za kutuma ujumbe nje ya nchi ambayo ni Sh95.

Serikali yakiri uwepo wa mgogoro kati ya wananchi na JWTZ

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi amekiri kuwepo kwa mgogoro wa wananchi na Jeshi la Kujenga Taifa (JWTZ) eneo la Kisakasaka.

Akizungumza leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Jimbo la Dimani Juma Ally Juma aliehoji Kuna mgogoro wa  kati ya Jeshi la polisi na wananchi wa Kisakasaka hali iliyoleta  wasiwasi kwa wananchi,  Je? ni lini serikali itapatia ufumbuzi wa mgogoro huo?

“Ni kweli kwamba mgogoro huu ni wa muda mrefu nataka nimfahamishe Mh. Juma kwamba mimi binafsi nimefika eneo hilo nilifanya mazungumzo na uongozi wa kikosi pamoja na uongozi wa eneo pamoja na wananchi wa pale kulizungumza na kama nilivyosema kwenye swali langu la msingi inachokwamisha kutatua sasa hivi ni suala la fedha za kupima kwasababu jeshi lilisharidhia kufanya mabadiliko ya mipaka yake ili wananchi wanaoonekana ndani ya kambi waweze kutolewa lakini   .Hata hivyo nitazungumza na Mh. Mbunge ili kumueleza zaidi ni hatua gani zinazostahili kuchukuliwa kwa mujibu wa ziara niliyoifanya pale na fedha zikipatikana,” amesema Waziri Mwinyi.

New AUDIO: Orezi ft. Tekno – Whine For Daddy

New AUDIO: Orezi ft. Tekno – Whine For Daddy

New AUDIO: Orezi ft. Tekno – Whine For Daddy

Orezi collaborates with Tekno on his first single of 2018 titled ‘Whine for Daddy.’ The song comes after his 2017 hit songs, ‘Hallelujah’ and ‘Cooking Pot’.

Orezi describes ‘Whine for Daddy’ as a “Sugar Daddy jam” aimed at making people dance. According to him, “I was just trying to make a record that people can dance to, just whine and Daddy will take care of you.”




Audio | Saida Karoli & Hanson Baliruno – Akatambala | Mp3 Download

Audio | Saida Karoli & Hanson Baliruno – Akatambala | Mp3 Download




Audio | Saida Karoli & Hanson Baliruno – Akatambala | Mp3 Download




Audio | Charly na Nina – Try me | Mp3 Download

Audio | Charly na Nina – Try me | Mp3 Download

Audio | Charly na Nina – Try me | Mp3 Download

Audio | Mr Kesho – Nitakupa Love | Mp3 Download

Audio | Mr Kesho – Nitakupa Love | Mp3 Download

Audio | Mr Kesho – Nitakupa Love | Mp3 Download

New VIDEO: Chindo Man ft Rayvanny – Mama Lao

New VIDEO: Chindo Man ft Rayvanny – Mama Lao

New VIDEO: Chindo Man ft Rayvanny – Mama Lao


DOWNLOAD VIDEO

Wednesday, 7 February 2018

Hizi ndizo Njia tatu za kupunguza foleni Dar

Wakati Serikali ikiendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali kukabiliana na changamoto ya foleni jijini Dar es Salaam, Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (Jica) limekuja na mwarobaini wa tatizo hilo.

Timu ya wataalamu wa shirika hilo imefanya utafiti ulioonyesha njia mbalimbali zinazoweza kutumiwa kukabiliana na foleni kubwa, ikiwamo ujenzi wa reli.

Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa mpangilio wa sekta ya usafirishaji katika Jiji la Dar es Salaam kwa mwaka 2018 hadi 2040, mwakilishi wa Jica nchini, Toshio Nagasa alisema kufikia mwaka 2040 wakazi wa jiji hilo watakuwa wameongezeka kutoka milioni sita hadi 12. Kutokana na ongezeko hilo Nagasa alisema ni muhimu kwa Serikali kuweka mazingira wezeshi ya usafiri ili kuwezesha sehemu zote za jiji kufikika kwa urahisi huku shughuli za uchumi zikiendelea.

“Kukabiliana na msongamano utakaojitokeza katika kipindi hicho ni muhimu Serikali ikafikiria kujenga miradi ya reli, ambayo inaweza kusafirisha watu wengi kwa pamoja, hii itasaidia kupunguza magari binafsi kuingia barabarani,” alisema.

Licha ya reli, mpango huo umeshauri kuwapo kwa barabara za juu katika makutano ya Morocco, Chang’ombe na Mwenge.

Kingine kilichoelekezwa katika mpango huo, ni uwapo wa miji midogo maeneo ya pembezoni ili kupunguza msongamano katikati ya jiji.

Kauli ya Serikali

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana alisema wataalamu hao wameshauri miji hiyo midogo iwekewe huduma zote za msingi ili watu wengi wasiende mjini. Alisema utekelezaji wa mradi huo utagharimu Sh19.1 bilioni ukihusisha ujenzi wa miundombinu.

Wakati huohuo, mkurugenzi wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam mhandisi Patrick Mfugale alimweleza waziri wa Ujenzi na Usafirishaji wa Lesotho, Lehlohonolo Moramotse, kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere (Tazara) wenye thamani ya Sh95 bilioni, unatarajia kukamilika Mei na kutumika rasmi mwishoni mwa Oktoba. Waziri huyo yupo nchini na wataalamu wa wizara yake kujifunza namna ambavyo wenzao wanasimamia ujenzi, ukarabati na utunzaji wa barabara.

Serikali yaahidi kuboresha mishahara

Serikali ya Tanzania imeahidi kuanza kuboresha maslahi ya watumishi ya walimu ikiwemo mishahara yao kipindi hiki kutokana na kumaliza zoezi la muda mfupi la uhakiki wa wafanyakazi hewa katika sehemu mbalimbali za ajira.

Hayo yamewekwa wazi na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI George Joseph kakunda leo (Jumatano) katika mkutano wa 10 kikao cha saba cha Bunge kinachoendelea mjini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Karagwe Innocent Bashungwa alipotaka kujua ni lini serikali itawapandishia mishahara walimu.

"Utaratibu huu ambao ulikuwa umesimama kwa kipindi kifupi cha miaka kama miwili hivi kupisha uhakiki wa watumishi ambapo ni zoezi lililofanywa kwa umahiri na ueledi mkubwa, baada ya kuwa tumelikamilisha sasa tutaingia kwenye awamu ambayo ni ya kuboresha maslahi ya watumishi ikiwemo mishahara yao", amesema Kakunda.

Kwa upande mwingine, Mhe. kakunda amewatoa hofu walimu wote ambao hawakupandishwa madaraja yao kutokea mwaka 2016 hadi 2017 na kudai katika mwaka huu wa fedha wameshafanya matayarisho wa kupandisha madaraja hayo.

Askari Magereza 11 wasimamishwa

Jeshi la Magereza Tanzania limewasimamisha kazi askari wake kumi na moja waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya mwanakijiji, Aloyce Makalla (41) wiki iliyopita.

Taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo zinasema askari hao walisimamishwa kazi na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dk Juma Malewa juzi.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, John Masunga alithibitisha kusimamishwa kwa askari hao lakini hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani zaidi akisisitiza kuwa msemaji wa jeshi hilo ni Kamishna Jenerali pekee.

Askari waliosimamishwa ambao walishafikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Korogwe mwishoni mwa wiki mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kassim Mkwawa ni Jonas Makere, Shadrack Lugendo, Lazaro Stephen, Mussa Zuberi, Ramadhan Yusuf, Robert Alfred, Fhidirish Osmas, Alfonce Revocatus, Mbesha Naftari, Hamis Msola na Michael Elias.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa hatua ya kuwasimamisha kazi askari hao imechukuliwa ikiwa ni kupisha vyombo vya sheria kufanya kazi yake kwa uhuru zaidi na kwamba hatima yao itategemea uamuzi wa mahakama hiyo.

Askari hao wa Wilaya ya Korogwe walifikishwa katika mahakama hiyo wakikabiliwa na shtaka la kumuua, Makalla, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kerenge wilayani humo.

Ilidaiwa mahakamani hapo na mwanasheria mwandamizi wa Serikali, Saraji Iboru kuwa Januari 22 saa 9.30 katika kitongoji cha Mapangoni Kijiji cha Kerenge, washtakiwa hao kwa pamoja walimuua mwanakijiji huyo.

Iboru ambaye alikuwa akisaidiana na mwendesha mashtaka kiongozi, Shosa Naiman alidai kwamba siku ya tukio, washtakiwa hao walikwenda nyumbani kwa Makalla wakimtuhumu kwamba Januari 15 alimjeruhi askari mwenzao aitwaye Sajenti Stephen.

Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji. Hakimu Mkwawa aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 15 itakapotajwa tena.