Sunday, 4 February 2018

Mtemela: baadhi ya Viongozi wa Kanisa wanaweza kuwa chanzo cha migogoro

Askofu mstaafu wa Kanisa Anglikana, Donald Mtetemela amesema baadhi ya viongozi wa kanisa wanaweza kuwa chanzo cha migogoro kutokana na tamaa ya mali na madaraka.

Askofu Mtetemela amesema hayo leo Jumapili Februari 4,2018 wakati ya misa ya kuwekwa wakfu na kusimikwa Askofu mteule Jackson Sosthnes wa kanisa hilo Dayosisi ya Dar es Salaam.

Amesema migogoro makanisa ni kazi ya shetani anayevuruga huduma ya Mungu ili isifanikiwe, hivyo kuwa katika hali ya hatari muda wote.

Askofu Mtetemela amesema migogoro haiwahusu waumini wa kanisa hilo pekee bali makanisa yote.

“Migogoro ni njia ya shetani ili kudhoofisha huduma ya kanisa, kazi yake ni kuingiza watu wasiofaa ili waweze kuwa viongozi. Utakuta mtu amevaa ngozi ya kondoo kumbe mbwa mwitu na wengine wanaingiza maandiko ambayo si maneno yaliyoandikwa kwenye vitabu vya dini,” amesema.

Amesema migogoro huleta chuki na roho ya kulipiza kisasi.

Amemweleza Askofu Jackson kuwa kazi yake si nyepesi, hivyo anatakiwa awe imara.

Askofu Jackson anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Valentino Mokiwa aliyeondolewa madarakani na uongozi wa juu wa kanisa hilo takriban mwaka mmoja uliopita.

Hospitali ya Aga Khan yaandaa Kampeni kuhamasisha Wananchi kupima saratani ya Utumbo



Hospitali ya Aga Khan kwa kushirikia na Mpango wa Taifa wa Damu Salama imeandaa kampeni kuhamasisha wananchi kupima saratani ya utumbo ili kujihami na ugonjwa huo.

Upimaji wa saratani ya utumbo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya saratani duniani ambayo huadhimishwa kila Februari 4.

Akizungumza leo Jumapili Februari 4,2018 daktari bingwa wa magonjwa ya saratani wa Hospitali ya Aga Khan, Dk Harrison Chuwa amesema hospitali hiyo imeamua kuhamasisha upimaji wa ugonjwa huo baada ya kuona kuna ongezeko la wagonjwa.

Amesema ili kujua kama una ugonjwa huo, kuna kipimo ambacho kinauzwa kwenye maduka ya dawa.

"Kipimo hiki unaweza kujipima mwenyewe ukiwa nyumbani, ukibainika kuwa na saratani ya utumbo ndipo unaweza kuwaona madaktari kwa uchunguzi zaidi," amesema.

Daktari bingwa wa magonjwa ya saratani wa hospitali hiyo, Dk Aleesha Adatia amesema ugonjwa huo unatibika iwapo mgonjwa atawahi kutibiwa.

"Wagonjwa wengi huwa wanafika hospitali wakiwa wamechelewa, tunashauri watu kujipima kwa kutumia kipimo hicho angalau mara moja kila mwaka," amesema.

Kuhusu dalili, Dk Adatia amesema ni kutoka damu wakati wa kujisaidia haja kubwa, kuchoka na kupungua uzito.

Ofisa kutoka Mpango wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, Fatma Mjungu amesema wanashirikiana na hospitali hiyo kwa kuwa kuna mahitaji makubwa ya damu kwa wagonjwa wa saratani.

"Ndiyo maana tupo hapa wakati wenzetu wanahamasisha upimaji wa saratani ya tumbo sisi tunahamasisha watu wajitolee kuchangia damu," amesema.

Amesema asilimia 25 ya damu inayokusanywa na mpango huo inatumiwa na wagonjwa wa saratani.

Amesema asilimia 42 ya damu inayokusanywa na mpango huo inatumiwa na watoto, huku asilimia 21 ikitumiwa na akina mama.

"Hivyo, ongezeko la saratani ya utumbo inasababisha matumizi makubwa ya damu, tunaomba jamii ichangie damu," amesema.

Sugu atembelewa na Wabunge wa Chadema, CUF Mahabusu



Wabunge wamefika Gereza Kuu la Ruanda jijini Mbeya kumjulia hali mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu'.

Waliomtembelea Sugu ni mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema na wa Tandahimba (CUF), Katani Katani.

Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wapo mahabusu wakikabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Lema na Katani wakiongozwa na mwenyeji wao Mbunge wa  Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda pia wamefika nyumbani kwa Desderia Mbilinyi, mama mzazi wa Sugu eneo la Sae jijini Mbeya kwa ajili ya kumfariji na kumtia moyo kutokana na misukosuko anayopitia mtoto wake.

Wakizungumza na familia ya Sugu, wabunge hao wamesema yupo gerezani kwa kuwa anapigania haki za wananchi.

Lema amemtaka mama huyo kuwa na moyo wa uvumilivu.

Shamsa Ford afunguka kuhusu ndoa yake



MSANII mwenye uwezo mkubwa anapokuwa mbele ya kamera Shamsa Ford, amefunguka kuwa kama angeamua kufuata mambo ya mjini na kujivika ustaa mwingi kama wafanyavyo wengine ingewezekana mpaka leo hii ndoa yake isingekuwepo kabisa.

Akizungumza na gazeti hili Shamsa, alisema kuwa ameamua kujishusha kabisa kwasababu anaamini kwenye ndoa hakuna ufundi wala ustaa wowote zaidi ya kujiheshimu na kutambua kuwa unapopewa heshima ya kuwa mke na wewe lazima uibebe ipasavyo.

“Siwezi kufanya ujinga wa kuichezea ndoa yangu kabisa kwani ndoa ni kitu adimu mno hivyo unapoipata lazima uilinde na kama ustaa uuache mlangoni unapoingia nyumbani la sivyo itakuwa ni shida na ndoa haiwezi kudumu,” alisema Shamsa.

Rais Magufuli asema anaposikia matatizo yametokea huwa anajiuliza akimbilie wapi

Rais Dkt. John Magufuli amesema mara zote anaposikia matatizo yametokea eneo fulani fulani huwa anajiuliza akimbilie wapi ili aweze kupata msaada wa utatuzi wa jambo hilo bila ya kuleta athari yeyote katika taifa.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo (Jumapili Februari 04, 2018) wakati alipohudhuria hafla ya kumweka wakfu na kumsimika Mchungaji Jackson Sosthenes kuwa Askofu wa tano wa Kanisa la Anglikana Dayosis ya Dar es Salaam.

"Sisi viongozi wa serikali mara nyingi huwa tunawategemea viongozi wa makanisa na misikiti katika kutuongoza, nafahamu serikali haina dini lakini naheshimu sana dini na kuthamini mawaidha pamoja na mafundisho yanatolewa na viongozi wa dini wawe waislamu, wakristo hata wahindu tunayaheshimu sana", alisema Rais Magufuli.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli aliendelea kwa kusema "siku zote sisi viongozi ndani ya serikali huwa tunafurahi sana kuona makanisa na misikiti ikiwa imetulia, unaposikia mahali fulani fulani kuna migogoro sisi viongozi na hasa mimi huwa najiuliza ninapopata matatizo ntakimbilia wapi. Kwa sababu makanisa na misikiti ni sehemu ya uponyaji wa roho zetu. Uponyaji wa roho ni mahali ambako kuna manufaa zaidi kuliko kwenye uponyaji wa mwili".

Kwa upande mwingine, Dkt. Magufuli amedai endapo mahali kwenye uponyaji wa mwili ukisikia kumeanza matatizo basi unapaswa kutazambua jinsi taifa unaloliongoza roho zake zitakavyopotea.

TUNDA: SIWEZI KUMUHESHIMU ANTI N’GO

Tunda Sebastian ‘Tunda’.
MUUZA nyago maarufu Bongo na mwenye visa kila kukicha Tunda Sebastian ‘Tunda’ amefunguka kuwa kamwe hawezi kuirudisha heshima yake aliyokuwa akiitoa kwa staa maarufu wa filamu Aunt Ezekiel, kama ilivyokuwa huko nyuma.
Staa maarufu wa filamu Aunt Ezekiel akiwa na mpenzi wake Moze Iyobo.
“ Mimi nilikuwa najua ni mwenye busara lakini hakuna kitu hivyo siwezi kumuheshimu tena hata kidogo maana zamani nilikuwa namchukulia kama dada lakini nimemvua cheo hicho kabisa kwangu hakipo,” alisema
Tunda.


DODOMA TENA! KAIBUKA NABII MWINGINE MPYA KAMJIBU NABII TITO! (VIDEO)


SHAMSA FORD: NINGEKUWA MZEMBE NINGESHAHARIBU

Shamsa Ford
MSANII mwenye uwezo mkubwa anapokuwa mbele ya kamera Shamsa Ford, amefunguka kuwa kama angeamua kufuata mambo ya mjini na kujivika ustaa mwingi kama wafanyavyo wengine ingewezekana mpaka leo hii ndoa yake isingekuwepo kabisa.
 
Akizungumza na gazeti hili Shamsa, alisema kuwa ameamua kujishusha kabisa kwasababu anaamini kwenye ndoa hakuna ufundi wala ustaa wowote zaidi ya kujiheshimu na kutambua kuwa unapopewa heshima ya kuwa mke na wewe lazima uibebe ipasavyo.
 
“Siwezi kufanya ujinga wa kuichezea ndoa yangu kabisa kwani ndoa ni kitu adimu mno hivyo unapoipata lazima uilinde na kama ustaa uuache mlangoni unapoingia nyumbani la sivyo itakuwa ni shida na ndoa haiwezi kudumu,” alisema Shamsa.

DIAMOND: WEMA, MOBETO NA TUNDA NI FAMILIA YANGU

Wema Sepetu.
MKURUGENZI wa lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Diamond, amefungukia ishu yake na mastaa watatu, Wema Sepetu, Hamisa Mobeto na Tunda Sabasita.
 
Amesisitiza kuwa urafiki wao umepitiliza kiasi cha kuwa sehemu ya familia yake. Akizungumza na Spoti Xtra, Diamond alisema kwamba wasanii hao hayuko nao kimapenzi tena.

Mkurugenzi wa lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Diamond.
“Kikubwa watu wanatakiwa watambue kwamba Wema alikuwa mpenzi wangu enzi hizo lakini kwa sasa hatuna mapenzi zaidi ya kuwa marafiki waliyopitiliza, kwani tuko kama ndugu

           Hamisa Mobeto.
“Kwa maana hiyo utagundua wazi kuwa hata huko nyuma tulikuwa tukigombanishwa zaidi na mashabiki zetu jambo ambalo sasa haliwezi kujirudia kwa sababu tumeshakua watu wazima.




Tunda Sabasita
“Suala la Tunda linasemwa sana ila ukweli ni kwamba hata yeye ni rafiki yangu mkubwa na ndiyo maana anaonekana sana katika familia yangu, suala la Mobeto lipo wazi kabisa kuwa ni mzazi mwenzangu hivyo naye atabaki kama rafiki wa karibu tu kwa kila jambo letu linapotokea.

“Pamoja na kwamba juzi hakutokea katika utambulisho wa Maromboso kwani kadi ya mwaliko tulimpa sema hakuja kutokana na kupata dharura,” alisema Diam-ond.

WASTARA AMWAGA MACHOZI AIRPOT, AKIONDOKA INDIA KUTIBIWA (VIDEO)

Msanii wa filamu za Kibongo, baada ya kuchangiwa fedha kwa ajili ya kwenda kutibiwa mguu nchini India, hatimaye leo ameondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea nje ya nchi kwa matibabu.

MZEE KINGUNGE NGOMBALE-MWIRU KUZIKWA KESHO …RATIBA IPO HAPA

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru enzi za uhai wake.
RATIBA  ya mazishi ya aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru, iliyotolewa na familia yake  leo inaonyesha atazikwa kesho Jumatatu katika shughuli itakayoanza saa 9:30 hadi 11:30 katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo iliyotolewa na mwenyekiti wa kamati maalum ya shughuli hiyo, Omary Kimbau, inaonyesha kwamba mwili wa marehemu utatolewa leo saa 10 jioni Hospitali ya Muhimbili na kupelekwa nyumbani kwake Victoria/Makumbusho ambako ibada na mila zitafanywa usiku mzima.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shughuli zitakazofanywa kesho ni kama ifuatavyo:
 
Jumatatu tarehe 5/2/2018
– Saa 1:00 asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
– Saa 2:00 asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi kupata kifungua kinywa
– Saa 4:00 asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani kwa marehemu
– Saa 6:00 mwili kuwasili Karimjee Hall  kuagwa
– Saa 6:00 mchana 9;00 kuaga mwili wa marehemu
– Saa 9:00 alasiri mpaka 9:30 kuelekea makaburini Kinondoni
– Saa 9:30 mpaka 11:30 maziko
– Saa 11:30 jioni 12:30 kuelekea nyumbani kwa chakula cha jioni
1:30 usiku mpaka. 2:45 chakula cha usiku waombolezaji wote
3:00 usiku- waombolezaji wote hitimisho la shughuli nzima
Kingunge Ngombale-Mwiru alifariki Ijumaa wiki hii katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akitibiwa majeraha baada ya kuumwa na mbwa wake.

Tunda "Diamond nipo nae karibu, nionane na Zari niongee naye nini?

Tunda "Diamond nipo nae karibu, nionane na Zari niongee naye nini?

Video Vixen maarufu Bongo Tunda ambaye amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na Star Diamond Platnumz, amezungumza kwenye Exclusive Interview ambapo ameongelea ishu ya yeye kudaiwa kutoka kimapenzi na Diamond huku akielezea kama Zari the Boss Lady alishawahi kumtafuta kuhusu ishu hiyo..
SHOW MORE



Wabunge wamtaka Waziri Mpango kubadili sera za Taifa



picha ya mtandao

Hali ya uchumi nchini imewaibua wabunge wakitaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kubadili sera za Taifa ili kuchochea ukuaji wake.

Wakichangia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Bunge za Bajeti; Uwekezaji na Mitaji na ile ya Viwanda, Biashara na Mazingira kwa mwaka 2017 juzi, wabunge hao walisema hali hiyo inajidhihirisha kutokana na takwimu zilizotolewa na taasisi kadhaa ikiwamo Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alisema umefika wakati kwa Wizara ya Fedha na Mipango kukubali kubadili sera za kibajeti.

Alinukuu takwimu za BoT za mwaka 2011 hadi Desemba 2017 kuwa Pato la Taifa kwa mwaka 2011 lilikua kwa asilimia 7.8 lakini sasa inakisia litakua kwa asilimia 6.8.

Mbunge huyo alisema pia mzunguko wa fedha umeshuka kutoka asilimia 22 kwa mwaka 2011 hadi asilimia 1.8 mwaka huu na ukuaji wa usafirishaji nje wa mazao hasa ya kilimo kilichoajiri watu wengi, pia umeshuka.

Bashe alisema ongezeko la idadi ya watu ni asilimia zaidi ya mbili lakini ukuaji wa kilimo ni asilimia 0.04 , hivyo hakuna muunganiko.

Alisema takwimu hizo zinatoa jibu kuwa sera za Taifa hazitoi kichocheo cha ukuaji wa biashara na uchumi katika nchi.

“Hili jambo tunaweza kusema humu ndani ya Bunge lisiufurahishe upande wa Serikali lakini tuna jukumu la kuwaambia ukweli na ni muhimu Wizara ya Fedha na Mipango ikakubali kwamba sera za Wizara ya Fedha si rafiki katika kuchochea uchumi wetu kukua,” alisema Bashe na kuongeza kuwa taarifa iliyopelekwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Msajili wa Hazina inaonyesha mapato ya BoT yanayotokana na biashara yameshuka kwa asilimia 63.

Alimshauri Waziri wa Fedha atakapowasilisha bungeni mpango wake wa maendeleo kwa mwaka wa fedha 2018/19 awasilishe na muundo wa namna gani Tanzania inawekeza katika uzalishaji.

Akijibu suala hilo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema baadhi ya hatua chache zinazochukuliwa kukuza uchumi ndizo zenye matukio ya moja kwa moja lakini nyingi zinachukua muda kuona matokeo.

Alisema Serikali inachofanya sasa ni kutumia fedha nyingi za bajeti kuongeza au kuchachua miundombinu na kulipa madai ambayo yamehakikiwa.

Alisema hatua nyingine wanazochukua ni kushusha kodi katika maeneo ambayo wanahamasisha kama Taifa.

Mbunge wa Momba (Chadema), David Silinde alisema katika taarifa ya wepesi wa kufanya biashara kwa viashiria vya nchi kumi na moja ambavyo vimetolewa, Tanzania imeporomoka kwa viashiria saba.

Alichambua kipengele cha upitishaji wa shehena bandarini akisema takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya 180 kati ya 190 ingawa bandari ndiyo mahali pekee kunakoiingizia nchi fedha nyingi.

Alisema hali ni mbaya na katika Bandari ya Dar es Salaam kwani kuna mlundikano wa makontena ambayo yamezuiwa kwa sababu ya mgongano.

“Watu wa TBS (Shirika la Viwango) wanasema hawawezi kuruhusu makontena yatoke mpaka wapate certification kutoka TRA (Mamlaka ya Mapato). TRA wanasema hawawezi kutoa mizigo hadi wapate certification kutoka TBS unaweza kuona contradiction (mgongano) ya watu wanaofanya kazi katika Serikali moja, wanavyoshindwa kufanya kazi kwa pamoja,” alisema.

Alisema kwa kuonyesha kuwa uchumi umeendelea kuyumba, Serikali imefunga baadhi ya benki kwa utetezi kuwa wigo wake ni mdogo.

“Ukiangalia zile benki 12, benki nane zinatakiwa kufungwa kwa sababu zina - run (zinajiendesha) chini ya faida. Nilipenda Serikali iangalie hili,” alisema.

Alisema mzunguko wa fedha umepungua kwa asilimia 45 na watu hawawezi kuagiza vitu lakini bado Serikali imekuwa ikisema kuwa fedha zipo.

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alisema katika bajeti zilizopita, kambi ya upinzani ilisema kitendo cha kuondoa kodi ya majengo kwenye halmashauri kwenda TRA ni kuzifanya zisiendelee.

Alisema Waziri wa Fedha na Mipango anavunja sheria kwa makusudi katika suala la kodi ya majengo kwa sababu Serikali imeshindwa kukusanya kodi na kuirejesha katika halmashauri kama sheria inavyomtaka.

“Mnatudanganya kuwa mmefanikiwa nitakupa mfano mmoja wa halmashauri yetu (Kinondoni) 2016/17 walikusanya Sh10 bilioni wakiwa na Halmashauri ya Ubungo tukawa tunapanga kuongeza mkapata tamaa mkachukua… Sasa hivi miezi sita imepita hamjaleta hata senti tano,” alisema.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema wanarejesha fedha walizozikusanya kutoka na kodi ya majengo kama sheria inavyotaka.

“Tukisema kule Geita wakusanye kodi ibaki kulekule na kule Mererani wakusanye inayotokana na Tanzanite ibaki kulekule hatutakuwa na Taifa.”

Alisema bajeti ya maendeleo ya Mkoa wa Dar es Salaam ilikuwa ni Sh14.2 bilioni na wamepeleka Sh11 bilioni ambayo ni asilimia 70 kwa miezi sita lakini kodi waliyokusanya ya majengo ni Sh10 bilioni.

“Nimuulize Kinondoni walikusanya Sh10 bilioni lakini ni mradi gani wamefanya kwa kodi ya majengo? Tusilidanganye Taifa hili na tukalikatakata, ”alisema.

Alisema Mdee analidanganya Bunge na kwamba mwaka 2014/15 Kinondoni ilikusanya Sh5 bilioni lakini Serikali ilipeleka zaidi ya Sh9 bilioni kwa ajili ya maendeleo.

Ufisadi katika vitambulisho

Katika mchango mwingine, Silinde alisema mradi wa hati za kusafiria umekuwa ukitekelezwa kwa gharama za dola 40 milioni za Marekani.

“Kuna taarifa nimezipata kuwa mradi huo ulikuwa na thamani ya dola 16 milioni sawa na pauni 11 milioni. Kuna taarifa kuna kampuni ambayo ilishapewa memorandum of understanding (makubaliano ya awali) ambayo haikusainiwa hadi dakika ya mwisho lakini mwisho wa siku ilipewa kampuni ya HID,” alisema.

Alisema kampuni HID ambayo imepewa kazi hiyo wakati haijawahi kufanya kazi ya mradi wa hati za kusafiria mahali popote na imekuwa ikitengeneza kadi za ku-swap.

Silinde alisema kampuni hiyo imeingia ubia na watu ambao walikuwa Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa) wakati uliopita.

“Kwa hiyo mwenyekiti ufisadi bado upo na uchumi umeendelea kuyumba lakini watu wameendelea kufichaficha tu kwa namna fulani, kama tunapinga ufisadi lazima hatua ichukuliwe,” alisema.

Alisema taarifa walizonazo za ndani katika mradi wa hati za kusafiria, kuna ufisadi wa kutisha katika jambo hilo.

Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba alisema ufisadi hauna nafasi kwa Serikali ya Awamu ya Tano ambayo alisema iko macho.

“Taarifa alizosema si hizo, mwanzoni wakati hatua zilipokuwa zikichukuliwa kabla ya Serikali kuingilia kati ukubwa wa mradi ule na dola zilizokuwa zikihitajika kutumika ni 192 milioni,” alisema.

Alisema sehemu za mradi zilikuwa nne na gharama za dola 57.8 milioni za Marekani zitatumika kukamilisha mradi huo wa hati za kusafiria za kielektroniki.