Sunday, 4 February 2018

TUNDA: SIWEZI KUMUHESHIMU ANTI N’GO

Tunda Sebastian ‘Tunda’.
MUUZA nyago maarufu Bongo na mwenye visa kila kukicha Tunda Sebastian ‘Tunda’ amefunguka kuwa kamwe hawezi kuirudisha heshima yake aliyokuwa akiitoa kwa staa maarufu wa filamu Aunt Ezekiel, kama ilivyokuwa huko nyuma.
Staa maarufu wa filamu Aunt Ezekiel akiwa na mpenzi wake Moze Iyobo.
“ Mimi nilikuwa najua ni mwenye busara lakini hakuna kitu hivyo siwezi kumuheshimu tena hata kidogo maana zamani nilikuwa namchukulia kama dada lakini nimemvua cheo hicho kabisa kwangu hakipo,” alisema
Tunda.


DODOMA TENA! KAIBUKA NABII MWINGINE MPYA KAMJIBU NABII TITO! (VIDEO)


SHAMSA FORD: NINGEKUWA MZEMBE NINGESHAHARIBU

Shamsa Ford
MSANII mwenye uwezo mkubwa anapokuwa mbele ya kamera Shamsa Ford, amefunguka kuwa kama angeamua kufuata mambo ya mjini na kujivika ustaa mwingi kama wafanyavyo wengine ingewezekana mpaka leo hii ndoa yake isingekuwepo kabisa.
 
Akizungumza na gazeti hili Shamsa, alisema kuwa ameamua kujishusha kabisa kwasababu anaamini kwenye ndoa hakuna ufundi wala ustaa wowote zaidi ya kujiheshimu na kutambua kuwa unapopewa heshima ya kuwa mke na wewe lazima uibebe ipasavyo.
 
“Siwezi kufanya ujinga wa kuichezea ndoa yangu kabisa kwani ndoa ni kitu adimu mno hivyo unapoipata lazima uilinde na kama ustaa uuache mlangoni unapoingia nyumbani la sivyo itakuwa ni shida na ndoa haiwezi kudumu,” alisema Shamsa.

DIAMOND: WEMA, MOBETO NA TUNDA NI FAMILIA YANGU

Wema Sepetu.
MKURUGENZI wa lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Diamond, amefungukia ishu yake na mastaa watatu, Wema Sepetu, Hamisa Mobeto na Tunda Sabasita.
 
Amesisitiza kuwa urafiki wao umepitiliza kiasi cha kuwa sehemu ya familia yake. Akizungumza na Spoti Xtra, Diamond alisema kwamba wasanii hao hayuko nao kimapenzi tena.

Mkurugenzi wa lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Diamond.
“Kikubwa watu wanatakiwa watambue kwamba Wema alikuwa mpenzi wangu enzi hizo lakini kwa sasa hatuna mapenzi zaidi ya kuwa marafiki waliyopitiliza, kwani tuko kama ndugu

           Hamisa Mobeto.
“Kwa maana hiyo utagundua wazi kuwa hata huko nyuma tulikuwa tukigombanishwa zaidi na mashabiki zetu jambo ambalo sasa haliwezi kujirudia kwa sababu tumeshakua watu wazima.




Tunda Sabasita
“Suala la Tunda linasemwa sana ila ukweli ni kwamba hata yeye ni rafiki yangu mkubwa na ndiyo maana anaonekana sana katika familia yangu, suala la Mobeto lipo wazi kabisa kuwa ni mzazi mwenzangu hivyo naye atabaki kama rafiki wa karibu tu kwa kila jambo letu linapotokea.

“Pamoja na kwamba juzi hakutokea katika utambulisho wa Maromboso kwani kadi ya mwaliko tulimpa sema hakuja kutokana na kupata dharura,” alisema Diam-ond.

WASTARA AMWAGA MACHOZI AIRPOT, AKIONDOKA INDIA KUTIBIWA (VIDEO)

Msanii wa filamu za Kibongo, baada ya kuchangiwa fedha kwa ajili ya kwenda kutibiwa mguu nchini India, hatimaye leo ameondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea nje ya nchi kwa matibabu.

MZEE KINGUNGE NGOMBALE-MWIRU KUZIKWA KESHO …RATIBA IPO HAPA

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru enzi za uhai wake.
RATIBA  ya mazishi ya aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru, iliyotolewa na familia yake  leo inaonyesha atazikwa kesho Jumatatu katika shughuli itakayoanza saa 9:30 hadi 11:30 katika makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo iliyotolewa na mwenyekiti wa kamati maalum ya shughuli hiyo, Omary Kimbau, inaonyesha kwamba mwili wa marehemu utatolewa leo saa 10 jioni Hospitali ya Muhimbili na kupelekwa nyumbani kwake Victoria/Makumbusho ambako ibada na mila zitafanywa usiku mzima.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shughuli zitakazofanywa kesho ni kama ifuatavyo:
 
Jumatatu tarehe 5/2/2018
– Saa 1:00 asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
– Saa 2:00 asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi kupata kifungua kinywa
– Saa 4:00 asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani kwa marehemu
– Saa 6:00 mwili kuwasili Karimjee Hall  kuagwa
– Saa 6:00 mchana 9;00 kuaga mwili wa marehemu
– Saa 9:00 alasiri mpaka 9:30 kuelekea makaburini Kinondoni
– Saa 9:30 mpaka 11:30 maziko
– Saa 11:30 jioni 12:30 kuelekea nyumbani kwa chakula cha jioni
1:30 usiku mpaka. 2:45 chakula cha usiku waombolezaji wote
3:00 usiku- waombolezaji wote hitimisho la shughuli nzima
Kingunge Ngombale-Mwiru alifariki Ijumaa wiki hii katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa akitibiwa majeraha baada ya kuumwa na mbwa wake.

Tunda "Diamond nipo nae karibu, nionane na Zari niongee naye nini?

Tunda "Diamond nipo nae karibu, nionane na Zari niongee naye nini?

Video Vixen maarufu Bongo Tunda ambaye amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na Star Diamond Platnumz, amezungumza kwenye Exclusive Interview ambapo ameongelea ishu ya yeye kudaiwa kutoka kimapenzi na Diamond huku akielezea kama Zari the Boss Lady alishawahi kumtafuta kuhusu ishu hiyo..
SHOW MORE



Wabunge wamtaka Waziri Mpango kubadili sera za Taifa



picha ya mtandao

Hali ya uchumi nchini imewaibua wabunge wakitaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kubadili sera za Taifa ili kuchochea ukuaji wake.

Wakichangia taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Bunge za Bajeti; Uwekezaji na Mitaji na ile ya Viwanda, Biashara na Mazingira kwa mwaka 2017 juzi, wabunge hao walisema hali hiyo inajidhihirisha kutokana na takwimu zilizotolewa na taasisi kadhaa ikiwamo Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alisema umefika wakati kwa Wizara ya Fedha na Mipango kukubali kubadili sera za kibajeti.

Alinukuu takwimu za BoT za mwaka 2011 hadi Desemba 2017 kuwa Pato la Taifa kwa mwaka 2011 lilikua kwa asilimia 7.8 lakini sasa inakisia litakua kwa asilimia 6.8.

Mbunge huyo alisema pia mzunguko wa fedha umeshuka kutoka asilimia 22 kwa mwaka 2011 hadi asilimia 1.8 mwaka huu na ukuaji wa usafirishaji nje wa mazao hasa ya kilimo kilichoajiri watu wengi, pia umeshuka.

Bashe alisema ongezeko la idadi ya watu ni asilimia zaidi ya mbili lakini ukuaji wa kilimo ni asilimia 0.04 , hivyo hakuna muunganiko.

Alisema takwimu hizo zinatoa jibu kuwa sera za Taifa hazitoi kichocheo cha ukuaji wa biashara na uchumi katika nchi.

“Hili jambo tunaweza kusema humu ndani ya Bunge lisiufurahishe upande wa Serikali lakini tuna jukumu la kuwaambia ukweli na ni muhimu Wizara ya Fedha na Mipango ikakubali kwamba sera za Wizara ya Fedha si rafiki katika kuchochea uchumi wetu kukua,” alisema Bashe na kuongeza kuwa taarifa iliyopelekwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Msajili wa Hazina inaonyesha mapato ya BoT yanayotokana na biashara yameshuka kwa asilimia 63.

Alimshauri Waziri wa Fedha atakapowasilisha bungeni mpango wake wa maendeleo kwa mwaka wa fedha 2018/19 awasilishe na muundo wa namna gani Tanzania inawekeza katika uzalishaji.

Akijibu suala hilo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema baadhi ya hatua chache zinazochukuliwa kukuza uchumi ndizo zenye matukio ya moja kwa moja lakini nyingi zinachukua muda kuona matokeo.

Alisema Serikali inachofanya sasa ni kutumia fedha nyingi za bajeti kuongeza au kuchachua miundombinu na kulipa madai ambayo yamehakikiwa.

Alisema hatua nyingine wanazochukua ni kushusha kodi katika maeneo ambayo wanahamasisha kama Taifa.

Mbunge wa Momba (Chadema), David Silinde alisema katika taarifa ya wepesi wa kufanya biashara kwa viashiria vya nchi kumi na moja ambavyo vimetolewa, Tanzania imeporomoka kwa viashiria saba.

Alichambua kipengele cha upitishaji wa shehena bandarini akisema takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya 180 kati ya 190 ingawa bandari ndiyo mahali pekee kunakoiingizia nchi fedha nyingi.

Alisema hali ni mbaya na katika Bandari ya Dar es Salaam kwani kuna mlundikano wa makontena ambayo yamezuiwa kwa sababu ya mgongano.

“Watu wa TBS (Shirika la Viwango) wanasema hawawezi kuruhusu makontena yatoke mpaka wapate certification kutoka TRA (Mamlaka ya Mapato). TRA wanasema hawawezi kutoa mizigo hadi wapate certification kutoka TBS unaweza kuona contradiction (mgongano) ya watu wanaofanya kazi katika Serikali moja, wanavyoshindwa kufanya kazi kwa pamoja,” alisema.

Alisema kwa kuonyesha kuwa uchumi umeendelea kuyumba, Serikali imefunga baadhi ya benki kwa utetezi kuwa wigo wake ni mdogo.

“Ukiangalia zile benki 12, benki nane zinatakiwa kufungwa kwa sababu zina - run (zinajiendesha) chini ya faida. Nilipenda Serikali iangalie hili,” alisema.

Alisema mzunguko wa fedha umepungua kwa asilimia 45 na watu hawawezi kuagiza vitu lakini bado Serikali imekuwa ikisema kuwa fedha zipo.

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alisema katika bajeti zilizopita, kambi ya upinzani ilisema kitendo cha kuondoa kodi ya majengo kwenye halmashauri kwenda TRA ni kuzifanya zisiendelee.

Alisema Waziri wa Fedha na Mipango anavunja sheria kwa makusudi katika suala la kodi ya majengo kwa sababu Serikali imeshindwa kukusanya kodi na kuirejesha katika halmashauri kama sheria inavyomtaka.

“Mnatudanganya kuwa mmefanikiwa nitakupa mfano mmoja wa halmashauri yetu (Kinondoni) 2016/17 walikusanya Sh10 bilioni wakiwa na Halmashauri ya Ubungo tukawa tunapanga kuongeza mkapata tamaa mkachukua… Sasa hivi miezi sita imepita hamjaleta hata senti tano,” alisema.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema wanarejesha fedha walizozikusanya kutoka na kodi ya majengo kama sheria inavyotaka.

“Tukisema kule Geita wakusanye kodi ibaki kulekule na kule Mererani wakusanye inayotokana na Tanzanite ibaki kulekule hatutakuwa na Taifa.”

Alisema bajeti ya maendeleo ya Mkoa wa Dar es Salaam ilikuwa ni Sh14.2 bilioni na wamepeleka Sh11 bilioni ambayo ni asilimia 70 kwa miezi sita lakini kodi waliyokusanya ya majengo ni Sh10 bilioni.

“Nimuulize Kinondoni walikusanya Sh10 bilioni lakini ni mradi gani wamefanya kwa kodi ya majengo? Tusilidanganye Taifa hili na tukalikatakata, ”alisema.

Alisema Mdee analidanganya Bunge na kwamba mwaka 2014/15 Kinondoni ilikusanya Sh5 bilioni lakini Serikali ilipeleka zaidi ya Sh9 bilioni kwa ajili ya maendeleo.

Ufisadi katika vitambulisho

Katika mchango mwingine, Silinde alisema mradi wa hati za kusafiria umekuwa ukitekelezwa kwa gharama za dola 40 milioni za Marekani.

“Kuna taarifa nimezipata kuwa mradi huo ulikuwa na thamani ya dola 16 milioni sawa na pauni 11 milioni. Kuna taarifa kuna kampuni ambayo ilishapewa memorandum of understanding (makubaliano ya awali) ambayo haikusainiwa hadi dakika ya mwisho lakini mwisho wa siku ilipewa kampuni ya HID,” alisema.

Alisema kampuni HID ambayo imepewa kazi hiyo wakati haijawahi kufanya kazi ya mradi wa hati za kusafiria mahali popote na imekuwa ikitengeneza kadi za ku-swap.

Silinde alisema kampuni hiyo imeingia ubia na watu ambao walikuwa Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa) wakati uliopita.

“Kwa hiyo mwenyekiti ufisadi bado upo na uchumi umeendelea kuyumba lakini watu wameendelea kufichaficha tu kwa namna fulani, kama tunapinga ufisadi lazima hatua ichukuliwe,” alisema.

Alisema taarifa walizonazo za ndani katika mradi wa hati za kusafiria, kuna ufisadi wa kutisha katika jambo hilo.

Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Mwigulu Nchemba alisema ufisadi hauna nafasi kwa Serikali ya Awamu ya Tano ambayo alisema iko macho.

“Taarifa alizosema si hizo, mwanzoni wakati hatua zilipokuwa zikichukuliwa kabla ya Serikali kuingilia kati ukubwa wa mradi ule na dola zilizokuwa zikihitajika kutumika ni 192 milioni,” alisema.

Alisema sehemu za mradi zilikuwa nne na gharama za dola 57.8 milioni za Marekani zitatumika kukamilisha mradi huo wa hati za kusafiria za kielektroniki.

Mimi Mars afunguka sifa za mwanaume kuwa nae

Msanii ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya 'Sitamani' chini ya Mdee Music, Mimi Mars amefunguka na kudai endapo atahitaji kuingia katika mahusiano kwa mara nyingine tena basi anataka kuwa na mwanaume mwenye kujielewa na kujitambua.

Mimi amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza katika 'Backstage' ya Bongo flava Top 20 kutoka East Afrika Radio baada ya kuulizwa ni kigezo gani huwa anaangalia pindi anapotaka kuwa na mwanaume katika mahusiano yake.

"Awe mtu anajielewa na kujitambua, awe na pesa lakini sio lazima kwa sana maana mimi mwenyewe sasa hivi nimeanza kupata 'mkwanja' kwa hiyo namshukuru Mwenyezi Mungu,' You know its good' vitu viwili vitatu naweza kujifanyia mwenyewe", alisema Mimi Mars.

Pamoja na hayo, Mimi Mars aliendelea kwa kusisitizia baadhi ya mambo kwamba "sana sana awe mtu anajielewa na kuweza kunisaidia hata mimi kunipa changamko katika akili yangu. Ila sitaki mtu ambae yupo katika sekta ambayo mimi nipo ili tuwe na kitu tofauti cha kuongelea"

Kwa upande mwingine, Mimi Mars amesema anatamani siku moja naye aje kuolewa ili aweze kuwa na familia yake pamoja na watoto.

Mbunge wa Chadema atishiwa maisha



Mbunge wa  (CHADEMA) Tarime Vijijini, John Heche amefunguka na kusema ameanza kupata vitisho mbalimbali kutoka kwa watu wasiojulikana wakimtishia maisha yake baada ya kusema ukweli kuhusu kupanda kwa gharama za vitambulisho vya Taifa.

Akiongea na www.eatv.tv Heche amedai kuwa ameanza kupata vitisho hivyo na kudai kuwa haviwezi kumrudisha nyuma katika kuisimamia Serikali na kuibana Serikali na kusema hawezi kubadili msimamo wake hata siku moja.

"Mtakumbuka kuwa majuzi jioni nilizungumza bungeni kuhusu kudanganywa umma juu ya mradi wa e-passports na kupanda kwa gharama za vitambulisho vya Taifa. Maelezo yangu bungeni yalitokana na Taarifa kutoka Kamati ya PAC na yalijibiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi. Sasa ndugu zangu nimeanza kupata vitisho dhidi ya ‘credibility’ yangu na maisha yangu. Ndugu zangu Taifa letu linapitia wakati ngumu Sana" alisema Heche

Heche aliendelea kusema kuwa

"Genge la wahalifu wa ki Uchumi na kisiasa kamwe lisitarajie nitatishika ama kubadili msimamo. Vitisho vilivyoanza dhidi yangu baada ya kuibua Ufisadi Katika Vitambulisho vya Taifa na E -Pasport havitaniogopesha kamwe. Njia zao ovu ama kunitisha ama kutaka kuchafua heshima yangu ama kunitengenezea kesi ama kuninifanyia alichofanyiwa Mhe. Tundu Lisu hazitanirudisha nyuma" alisisitiza Heche

Mbali na hilo Heche ameweka wazi kuwa kwa sasa anaandaa nyaraka muhimu ili azipeleke Bungeni kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza ubadhirifu uliofanyika katika Vitambulisho vya Taifa pamoja na E- Passports.

Source:eatv

Samatta arejea kwenye ubora wake



Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Ally Samatta amerejea kwenye ubora wake baada ya jana kucheza kwa dakika 68 na kuisaidia timu yake ya KRC Genk kuibuka na ushindi wa 1-0 ugenini.

Samatta ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitatu jana amecheza mchezo wake wa tatu tangu apone majeraha ya mishipa ya paja ambayo aliyapata Novemba 4 mwaka jana.

Genk jana imeshinda mchezo wake wa Ligi kuu nchini Ubelgiji dhidi ya wenyeji Royal Excel Mouscron kwenye uwanja Le Canonnier mjini Mouscron, Ubelgiji.

Baada ya Samatta kutoka nafasi yake ilichukuliwa na mshambuliaji kutoka DR Congo, Dieumerci N'Dongala ambaye alifunga bao pekee la ushindi katika mchezo huo dakika ya 83.

Jumanne wiki hii Samatta aliichezea Genk na kutoa pasi ya bao la kwanza la timu yake lakini bao hilo halikusaidia timu hiyo kushinda kwani ilifungwa 3-2 ugenini dhidi ya Kortrijk katika mechi ya Kombe la Ubelgiji.

Hii ndio Ratiba ya Mazishi ya Mzee Kingunge kesho

Mzee Kingunge Ngombale Mwiru enzi za uhai wake.

Ratiba ya mazishi ya Baba yetu mpendwa Mzee Kingunge Ngombale Mwiru(Baba Kinje)
Jumapili tarehe 4/2/2018
– Saa 10:00 jioni mwili kutoka Hospitali kuelekea nyumbani Victoria/Makumbusho Kingunge street.
-Saa 11:00 jioni mwili kuwasili nyumbani na taratibu za ibada mila na desturi kuendelea usiku mzima(mkesha)

Jumatatu tarehe 5/2/2018
– Saa 1:00 asubuhi mpaka saa 2:00 asubuhi waombolezaji kuwasili nyumbani Kwa ajili ya kuanza taratibu za mazishi.
– Saa 2:00 asubuhi mpaka saa 3:30 asubuhi Kupata kifungua kinywa/Chai Kwa waombolezaji wote
– Saa 4:00 asubuhi mpaka saa 5:00 misa nyumbani Kwa marehemu
– Saa 6:00 mwili kuwasili karemjee halll Kwa kuagwa
– Saa 6:00 mchana 9;00 kuaga mwili wa marehemu
– Saa 9:00 aalasiri mpaka 9:30 kuelekea makaburini kinondoni
– Saa 9:30 mpaka 11:30 maziko
– Saa 11:30 jioni 12:30 kuelekea nyumbani Kwa chakula cha jioni.
waombolezaji wote
1:30 usiku mpaka. 2:45 chakula cha usiku waombolezaji wote
3:00 usiku- waombolezaji wote hitimisho la shughuli ya Mzee wetu

Tunawashukuru sana Kwa ushiriki wenu wa Hali na mali katika wakati huu mgumu
Mungu awazidishie
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe🙏

Omary A kimbau( Mwenyekiti wa kamati ya mazishi)

 Facebook  Twitter  Google+  Pinterest  Linkedin
Newer Post Older Post
POPULAR
TAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017
TAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017
Breaking News:NECTA wanatangaza matokeo ya Kidato cha Nne
Breaking News:NECTA wanatangaza matokeo ya Kidato cha Nne
VIDEO: Ifahamu Dini Ya Kingunge Na Mengine Usioyajua
VIDEO: Ifahamu Dini Ya Kingunge Na Mengine Usioyajua
Ufafanuzi wa Serikali kuhusu uhamisho wa walimu
Ufafanuzi wa Serikali kuhusu uhamisho wa walimu
Mama afunguka kuhusu Nabii Tito na Kanumba
Mama afunguka kuhusu Nabii Tito na Kanumba
VIDEO: EXCLUSIVE Katambi aichana CHADEMA Amtaja LISSU
VIDEO: EXCLUSIVE Katambi aichana CHADEMA Amtaja LISSU
VIDEO: Aunty Ezekiel ahaidi kuwalipa shilawadu
VIDEO: Aunty Ezekiel ahaidi kuwalipa shilawadu
Serikali yafuta kifungu umri wa kustaafu
Serikali yafuta kifungu umri wa kustaafu
Dalili Hizi Zinaashiria Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI
Dalili Hizi Zinaashiria Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI
BREAKING: Mzee Kingunge Ngombale Mwiru Amefariki Dunia
BREAKING: Mzee Kingunge Ngombale Mwiru Amefariki Dunia

Zidane:kumtoa Ronaldo lilikuwa ni suala la kiufundi sio kumpumzisha

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema kitendo cha kumtoa Cristiano Ronaldo kwenye mchezo wa jana dhidi ya Levante dakika ya 82 haikuwa kwasababu ya kumpumzisha.

''Kumtoa Ronaldo lilikuwa ni suala la kiufundi wala si kumpumzisha kwaajili ya mchezo dhidi ya PSG kama inavyodaiwa, tulikuwa tunaongoza kwa 2-1 na hatukuweza kuongeza bao licha ya kushambulia, hivyo tulitaka kuingiza kiungo Marco Asensio ili tumiliki mpira'', amesema.

Zidane amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa mashabiki ambao wanadai kutoka kwa Ronaldo kulisababisha Levante kushambulia na kusawazisha bao la pili dakika ya 89 na kufanya mchezo umalizike kwa sare ya 2-2.

Baada ya sare ya jana Real Madrid imesalia katika nafasi ya nne ikiwa na alama 39 huku vinara Barcelona wakiwa na alama 57 kileleni.