Thursday, 25 January 2018

Audio | Mr Paul ft. Sharon Searle – Turn Me On | Mp3 Downlaod

Audio | Mr Paul ft. Sharon Searle – Turn Me On | Mp3 Downlaod

Audio | Mr Paul ft. Sharon Searle – Turn Me On | Mp3 Downlaod

DOWNLOAD Mp3

New VIDEO: Stella Mwangi – KUCHIZI

New VIDEO: Stella Mwangi – KUCHIZI
New VIDEO: Stella Mwangi – KUCHIZI

Iyobo azungumzia ishu ya Aunt kumnyima penzi




DANSA maarufu Bongo, Moses Iyobo, amesema kuwa kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa amenyimwa penzi na mzazi mwenzie Aunt Ezekiel hajaona kama kuna tatizo ingawa aliandika kama utani.

Akizungumza na gazeti hili, Iyobo alisema kuwa yeye na Aunt ni watu ambao wanataniana sana japokuwa tayari ni wazazi kwa hiyo hata alipoandika juzikati Instagram, alikuwa kwenye kuendeleza utani japo mashabiki wao wameipokea vibaya.

“Unajua watu wanashindwa kuelewa lakini mimi na mama Cookie (Aunt) tunataniana sana kwa hiyo hata kuandika vile ni kumtania tu sasa watu hawakuelewa naona wametoa povu kweli,” alisema Iyobo.

Iyobo alikomenti kwenye video aliyoposti Aunt ikimuonesha akitembea akisindikiza na ujumbe wa neno ‘fresh’:

“Umeninyima penzi halafu uposti fresh?” alikomenti Iyobo.

Chuchu afunguka ishu ya kumtoboa sikio mtoto wake



MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Chuchu Hans amefungukia madai ya kumtoboa sikio mtoto wao wa kiume Jaden mwenye umri wa mwaka mmoja akidai kuwa suala hilo limepokelewa ndivyo sivyo.

Akizungumza na gazeti la Global publishers, Chuchu alisema kuwa hakumtoboa kabisa sikio bali baba yake (muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’) ndiye aliyemvalisha kihereni cha kubandika na siyo kumtoboa moja kwa moja.

“Watu hawajatuelewa jamani hatuwezi kumtoboa sikio mtoto kwenye umri alionao tena wa kiume bali baba yake alimvalisha hereni ya kubandika tu, wasituzungumzie vibaya bwana,” alisema Chuchu.




Kadja Nito kwenye bifu zito na Mama yake


MREMBO wa Bongo Fleva, Natasha Lisimo ‘Kadja Nito’ ambaye aliingia kwenye bifu zito na mama yake baada ya kubadili dini na kuwa Mkristo na kumsamehe kipindi alipokuwa mahututi akijifungua, amemtibua tena mzazi wake huyo kutokana na kukomaa kwenye dini hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, kitendo cha mama yake Kadja kumsamehe alipokuwa mahututi leba, aliamini baada ya kurejea kwenye hali yake ya kawaida huenda angemtii na kurudi kwenye Uislamu lakini ndiyo kwanza, dini ya Kikristo imemkolea na sasa anajianika waziwazi hadi mitandaoni, jambo linalomchefua mzazi wake huyo.

Kutokana na ishu hiyo Kadja alipoulizwa alisema; “Kuna vitu sipendi kuviongelea sana kwa sasa, hususan mambo yangu na mama yangu ni masuala ya kifamilia, kama mnaona najianika kwenye Ukristo na nilibadili dini nikawa huko, sioni kama kuna haja ya kuzungumzia hilo kwa kina.


Watumishi wa Idara ya Uhamiaji wapewa siku tatu kuhama mjini



o

IDARA ya Uhamiaji katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetoa siku tatu kwa watumishi wake walioripoti Dodoma kuhamia katika nyumba zake zilizopo eneo la Iyumbu, nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma, badala ya kung’ang’ania kuishi katikati ya mji.

Nyumba hizo 63 zenye thamani ya Sh. bilioni 3.8 zimekabidhiwa jana kwa Idara hiyo na Shirika la Nyumba (NHC).

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Kamishna wa Fedha wa Idara hiyo, Peter Chogero, kwa niaba ya Kamshina Mkuu alisema serikali imeshanunua nyumba kwa ajili ya watumishi hao hivyo hakuna sababu ya wao kuendelea kuishi katikati ya mji wa Dodoma.

“Uhamiaji imenunua nyumba 63 eneo la Iyumbu ambazo zimejengwa na NHC, tutashangaa kuona watumishi wengine waendelee kuishi mjini wakati nyumba zao zipo hapa Iyumbu,” alisema.

Alitoa siku tatu kuanzia jana kila mtumishi aliyepangwa kuhamia kwenye nyumba hizo awe ameingia kwa kuwa hakuna sababu ya kung’ang’ania kuishi nje ya nyumba hizo wakati zimelipiwa na serikali.

Chongero alisema kabla ya manunuzi ya nyumba hizo, Idara hiyo ilikuwa na nyumba 10 mjini Dodoma ambazo hazikuweza kutosheleza watumishi wote, ikiwamo waliohamia kutoka Makao Makuu Dar es Salaam.

Alibainisha waliamua kuongeza idadi ya nyumba ili kila mtumishi wa Uhamiaji aishi kwenye nyumba ya serikali na kwamba wanatarajia kuongeza nyingine 40.

Naye, Meneja Masoko wa NHC, Itandula Gambalagi alisema ujenzi wa nyumba za Uhamiaji ulianza Desemba, 2016 katika eneo lenye ukubwa wa ekari 234 na ni moja ya sehemu ya mji uliopangiliwa kitaalamu kwa kuzingatia sheria na kanuni za mipango miji.

Alisema nyumba zilizokabidhiwa Uhamiaji ni sehemu ya nyumba 150 zilizojengwa katika mradi wa Iyumbu na tayari nyumba zilizobaki zote zimepata wanunuzi.

Gambalagi alisema nyumba hizo zina miundombinu yote inayotakiwa.

Kwa upande wake, mthamini wa mali za serikali, Joseph Maliti aliagiza Uhamiaji kuingiza nyumba hizo katika daftari la mali za serikali mara moja, ikiwa ni pamoja na thamani kwa kila nyumba.

Maduka 95 ya kubadilisha Fedha yasitisha Biashara


MADUKA 95 kati ya 297 ya kubadilishia fedha yaliyokuwepo nchini kufikia katikati ya mwaka jana, yamesitisha biashara katika zoezi la uandikishwaji na utoaji upya wa leseni.

Kwa mujibu wa taarifa ya ufafanuzi kwa Nipashe iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uzimamizi wa Mabenki wa Benki Kuu (BoT), Kened Nyoni, maduka 64 hayakuomba leseni kama ilivyotakiwa kisheria Juni, mwaka jana.

Kwa mujibu wa ufafanuzi huo wa juzi, maduka 233 yaliwasilisha nyaraka muhimu kwa ajili ya maombi ya leseni na 64 yaliruhusiwa kuendelea na biashara, huku 31 yakiamua kufunga, na 138 BoT inafanya mapitio ya taarifa zake.

"Kati ya maduka 297 yaliyotakiwa kuomba upya leseni zao, maduka 64 hayakuwasilisha nyaraka yoyote... baada ya kupitia nyaraka za maduka 233, maduka 31 yaliamua kufunga biashara," alibainisha.

Taarifa ya BoT Juni, mwaka jana, ilionyesha kuwa maduka hayo yamepewa miezi mitatu kukamilisha usajili mpya kwa lengo la kuboresha usimamizi na kuweka mfumo wa kisasa utakaoleta tija katika mabadiliko ya uchumi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, BoT iliongeza mtaji wa maduka hayo kutoka Sh. milioni 100 hadi Sh. milioni 300 kwa yale ya daraja A.

Aidha, BoT ilipandisha mtaji kutoka Sh. milioni 250 hadi Sh. bilioni moja kwa maduka ya daraja B na kuongeza amana zisizo na faida kutoka dola za Marekani 50,000 hadi 100,000 (sawa na Sh. milioni 112 hadi Sh. milioni 224).

Aidha, Benki Kuu katika masharti yake kwa biashara hiyo ya kubadilisha fedha za kigeni ilizuia wenye hisa, wakurugenzi, mmoja wa mameneja au mfanyakazi kuwa kwenye duka zaidi ya moja.

Maduka yote yalitakiwa kufunga kamera maalum za ulinzi za CCTV, masharti hayo yalitaka, "ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zote muhimu za ulinzi na usalama kama zilivyoanishwa kwenye kanuni za mwaka 2015".

Aidha, wamiliki wa maduka hayo kwenye usajili wanatakiwa kutoa taarifa zao binafsi, ikiwamo chanzo cha mapato yaliyowezesha kuwepo kwa duka husika, na kueleza kwa undani kila kilichojazwa kwenye fomu mahali kilipo kwa kuwa kitafuatiliwa kwa kina.

Nyoni alisema Januari 2, mwaka huu, BoT ilitoa notisi kwa wafanyabiashara ambao hawajakamilisha nyaraka za usajili na walioshindwa kufikia vigezo vilivyotakiwa.

"Kwa kuzingatia kuwa maombi mengine yaliletwa dakika za mwisho (kelekea Desemba 31, mwaka jana), tumeongeza siku 30 kwa ajili ya mapitio kwa ambao hawakuwa wamekamilisha nyaraka za mwisho wafanye hivyo kuruhusu leseni kutolewa Januari 31, mwaka huu," alifafanua.

Alisema kwa kipindi cha kusubiri leseni maduka yaliyo kwenye utaratibu wa kupata leseni yanaruhusiwa kuendelea na kazi za kila siku.

MWAKA 1992Maduka ya kubadilishia fedha za kigeni yana historia fupi nchini kutokana na kuanzishwa na Sheria ya Fedha za Kigeni ya mwaka 1992 ambayo inampa Gavana wa BoT mamlaka ya kuanzisha maduka ya kuuza na kununua fedha za kigeni na pia mamlaka ya kutunga kanuni, taratibu, miongozo na maelekezo ya kusimamia maduka hayo.

Kanuni za kwanza zilitungwa na Gavana mwaka 1999, lakini kwa kuwa maduka hayo hayakuwa mengi hakukuwa na masharti magumu mpaka mabadiliko ya kanuni ya mwaka 2015 ambayo yalichangiwa pamoja na mengine, serikali kutambulisha mfumo mpya wa ukusanyaji kodi kwa kupitia mashine za kodi za kielektroniki (EFD).

Ndipo likaja tangazo la Juni 30, mwaka jana kwenye gazeti la serikali ambalo lilitata mchakato huo wa usajili upya kumalizika Septemba kabla ya kuongezwa muda mara mbili mpaka Januari 31, mwaka huu.

Habari zinadai masharti mapya ya Serikali yanatokana na BoT, kwa kushirikiana na vyombo vingine, kubaini maduka mengi yalikuwa yanaficha mitaji halisi.

Imeelezwa vitabu vya mahesabu vya maduka mengi vilionyesha mitaji ambayo siyo halisi, na baadhi kudai kupata hasara kila mwaka.

Mzee Majuto amelazwa Muhimbili



Mchekeshaji Amri Athuman aka Mzee Majuto Jumatano hii amelazwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es saalam kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Habari wa Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni.

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii Asifa Habari huyo, Masoud kaftany, amesema muigizaji huyo alipelekwa hospitali hapo siku ya jana baada ya kuzidiwa.

“Ni kweli Mzee Majuto anaumwa na sasa hivi tupo naye hapa Muhimbili anaendelea na matibabu,” alisema Masoud kaftany. Kusema anaumwa nini ni mapema zaidi lakini baadae tutatoa taarifa rasmi baada ya kupokea taarifa ya madaktari,”

Afisa huyo amekiomba Chama cha Waigizaji, wadau wa filamu Tanzania na wa Tanzania wote wamuombee muigizaji aweze kupona haraka

Source: Bongo 5

DC ashtakiwa na Wenyeviti wa mitaa




  Dar es Salaam. Wenyeviti wa serikali za mitaa ya Kimara Baruti, Mavurunza na Makoka wamemshtaki katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Makori Kisare kwa madai ya kukiuka maadili ya utumishi wa umma kwa kutumia mamlaka yake kuwaweka ndani bila sababu za msingi.

Wenyeviti hao wameliambia gazeti hili kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuona vitendo hivyo vinazidi kukithiri, wanaitaka Tume ya Maadili iingilie kati.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mavurunza, Josephat Nehemia alisema mkuu huyo wa wilaya amekuwa akiwanyanyasa wenyeviti wa mitaa kwa kuagiza askari kuwakamata bila kuwaeleza makosa yao.

Nehemia alisema kwa muda mrefu amevumilia uonevu huo ila kwa sasa ameona awasilishe malalamiko yake katika sekretarieti ya maadili ili yaweze kushughulikiwa.

“Anachokifanya DC ni ukiukwaji wa maadili ya uongozi, kiongozi huwezi kuwa unasikiliza maneno bila kuyafanyia uchunguzi unaagiza mwenyekiti awekwe ndani, tunawekwa mahabusu bila kuambiwa makosa yetu, suala hili sasa basi,” alisema.

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Kimara Baruti, Aloyce Kinyonga alidai kuwa DC huyo alimtukana hadharani kwa kumuita mtu asiye na maana.

“DC akiwa kwenye mkutano mtaa wa Kilungule A alitamka mbele ya wananchi kuwa mimi sina nidhamu, ni mtu wa hovyo kosa langu likiwa ni kuandika barua kuhusu suala la umeme, nimeona nami nilete malalamiko yangu tume ili waone viongozi wasiozingatia maadili,” alisema.

Akizungumzia suala hilo, mwenyekiti wa mtaa wa Makoka, Emmanuel Akyoo alisema kitendo cha kuwekwa ndani bila kuambiwa kosa alilofanya kinamsababishia kushindwa kutekeleza majukumu yake.

“Nashindwa kufanya kazi vizuri, muda wote nakuwa na wasiwasi na ninaamini hatuwezi kuendelea kwa mtindo huu, lazima viongozi tufanye kazi kwa uhuru,” alisema.

Kauli ya DC

Kisare alisema wenyeviti wote waliowekwa ndani walikuwa na makosa na kwamba hafahamu sababu za kumtuhumu.

Alisema wenyeviti wote ambao amewachukulia hatua walikuwa na makosa mbalimbali ikiwamo ubadhirifu, ukiukwaji wa taratibu na uonevu kwa wananchi.

“Hao ni watu wanaotaka kufanya siasa, sisi hatuna muda wa porojo lengo letu ni kuleta maendeleo hivyo hatuwezi kuvumilia wanaotumia nafasi zao kama mtaji,” alisema.

Akitoa mfano mtaa wa Golani ambako mwenyekiti wake aliwekwa ndani kwa kosa la kukiuka mwongozo uliotolewa na manispaa kwa ajili ya kufanya urasimishaji.

“Manispaa imeweka mwongozo kwa kila kata kuwe na urasimishaji wa makazi na gharama ya mpimaji isizidi Sh260,000 yeye akaenda kuleta mtu wa kufanya kazi hiyo kwa Sh450,000, akawa anawaweka ndani watu waliokuwa wanapinga gharama hizo,” alisema. 

Mensen Selekta na DJ Tito wamshambulia Man Fongo




Msanii na mtayarishaji muziki kutoka studio ya Defatality Mensen Selekta pamoja na DJ Tito wamemshambulia kwa maneno muimbaji wa singeli Man Fongo kutokana na tabia yake ya kutafuta kiki kwa kutumia majina yao kila anapotaka kutoa kazi zake mpya.

Mensen na DJ Tito wameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya msanii huyo kusema 'biti' anayolalamikiwa kuwa ameiba kwamba amepewa na DJ Tito ambae yupo chini ya Mensen.

"Mimi naomba tu, nimekanye Man Fongo maana naona muziki wake hawezi kuufanya bila ya Mensen kwa sababu haiwezekani kila anapotaka kuachia ngoma au 'video' amzungumzie Mensen ameenda amerudi kwa nini hawezi kuwazungumzia watu wengine ?. Kwa hiyo inaonesha kabisha Man Fongo bila ya Mensen hamna kitu, suala la kutoa 'instrument' ninavyojua mimi 'biti' sikutoa mimi bali alitengeneza kijana wangu", alisema Mensen.

Aidha, Mensen Selekta aliendelea kufafanua baadhi ya mambo na kusema siyo kweli kama anavyodai Man Fongo kuwa mdundo huo unaolalamikiwa amemuibia Sholo Mwamba kuwa umetolewa na DJ Tito.

"Cha kwanza akanushe kauli yake, DJ Tito hajagawa 'biti' kwa sababu yeye siyo 'producer' halafu ninavyojua mimi hawana mahusiano ya karibu ya kihivyo na Man Fongo", alisisitiza Mensen Selekta.

Kwa upande wake DJ Tito alisema alifuatwa na Man Fongo ili aweze kutengeneza 'kiki' kupitia mdundo huo kwa kumtaka aseme yeye ndio aliyempatia ili Sholo Mwamba akasirike.

"Mimi siwezi kupenda kumwambia kitu kizuri Man Fongo, sema namuelekeza kimazingira tu lakini yeye anayumba halafu kigege 360 kipo kwa ajili ya kazi na kupambana ili mambo yaende, muziki haufanywi hivyo anakiuka mazingira ya kimuziki", alisema DJ Tito.

DJ Tito aliendelea kwa kusema "Man Fongo yeye afanye kazi nzuri tu mbona watanzania watampokea vizuri, halafu hichi kigege 360 ndicho kilichomlea ila yeye ameleta dharau kwa Mensen na kwangu mimi ambaye niliyemtoa Tandale kwa hiyo Man Fongo ana laana na laana siyo lazima upewe na Baba au Mama hata masela kama sisi tunakuachia laana na hausongi mbele".

Malaika afungukia udhaifu wake



MWIMBAJI anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Diana Exavery ‘Malaika’, amefunguka kuwa, udhaifu wake mkubwa kwenye maisha ni kusimama mbele za watu na kujielezea yeye ni nani.

Akipiga stori na Showbiz-Xtra, Malaika alisema, katika maisha amekuwa na udhaifu tofauti tofauti lakini mkubwa kuliko wote ni kutokuwa na ujasiri wa kuweza kusimama mbele za watu na kujieleza.

“Nimewahi kufeli kwenye interview nyingi kwa sababu ya kutakiwa kujielezea, kwa kweli huu ni udhaifu wangu mkubwa, hali hii ni tofauti na nikiwa jukwaani niki-paform, kuimba jukwaani mbele ya mashabiki ni tofauti na kujielezea,” alisema Malaika

HOME AFYA BIASHARA MAHUSIANO KILIMO MAKALA TECNOLOG UREMBO CONTACT US Asilimia 75 waendao kupima JKCI wanakutwa na maradhi ya moyo




WATU 15 kati ya 20 wanaokwenda  kwa uchunguzi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), sawa na asilimia 75, wanakutwa na maradhi mbalimbali ya moyo, imefahamika.

Akizungumza  na waandishi wa habari jana, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo katika taasisi hiyo, Dk. Peter Kisenge, mbali na watu hao, alisema asilimia mbili hadi tatu  ya watoto wanaozaliwa nchini wana tatizo la moyo.

Kutokana na takwimu hizo, alisema ni vyema Watanzania wakafika katika taasisi hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati kwa ajili ya uchunguzi, ikiwa ni pamoja na kujiunga na bima ya afya kwa kuwa huduma za matibabu ni kubwa.

Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo, alisema JKCI kwa kushirikiana na taasisi za Israel na Ujerumani, wameokoa Sh. milioni 800 ambazo zingetumika kuwapeleka nje ya nchi watoto 30 kwa matibabu ya moyo.

 Taasisi hizo ni Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto ya Israel na Kituo cha Moyo cha Berlin, Ujerumani, ambao hadi sasa wamewafanyia upasuaji wa bila kufungua kifua watoto 15.

 “Upasuaji unatumia mtambo wa Cathlab umefanyika katika kambi maalumu iliyoanza Januari 20, mwaka huu na itamalizika kesho (leo). Matibabu yaliyofanyika ni kuzibua matundu kwenye moyo na kutanua mishipa ya moyo kwa watoto wenye umri wa kuanzia mwezi mmoja hadi miaka 18,” alisema.

 Kwa mujibu wa Kisenge, kambi hiyo ilikwenda sambamba na uchunguzi wa moyo kwa watoto 32 ambao kati yao 20 watafanyiwa matibabu katika kambi hiyo na wengine 12 watatibiwa na madaktari hapa nchini kuanzia wiki ijayo.

 “Tumepanga kufanya matibabu kwa watoto 20, tunaamini hadi kambi itakapomalizika watakuwa wamepata matibabu. Watoto 15 waliopata matibabu wamesharuhusiwa na waliobaki wanaendelea vizuri,” alisema.

 “Tumetoa elimu ya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa watoto, jinsi ya kuwahudumia waliofanyiwa upasuaji. Waliopata mafunzo ni madaktari, wauguzi, wataalamu wa kutoa dawa za usingizi na wataalamu wengine wa chumba cha upasuaji,” alifafanua.

 Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, asilimia 90 ya matibabu bila kufungua kifua yanafanywa na madaktari wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

 Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo, Naiz Majani, alisema wanawake wanapaswa kufanya uchunguzi wakiwa na mimba ya miezi minne, ili watakapojulikana na tatizo wajifungue katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, hivyo kuwa rahisi kupata matibabu.

 Alisema kuna wanawake 35 wenye tatizo la moyo, kati yao watano wamejifungua mmoja mwanawe alifariki dunia kwa ugonjwa mwingine, wawili wana matundu makubwa kwenye moyo na mmoja limeanza kupungua.

 “Tunawashauri wazazi na walezi wasisahau kupima afya zao watoto wao watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto kwani magonjwa mengi yanaanzia utotoni,” alisema.

 Kwa mujibu wa Dk. Majani, mtoto akianza kuugua magonjwa ya moyo, wazazi wengi  wanadhani ni matatizo ya kifua, lakini baada ya kuwafikisha hospitalini na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulika.

Tangu mwaka 2015 hadi sasa, watoto 46 wamefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel na kwamba gharama zimekuwa zikitolewa na taasisi za Israel na Ujerumani kwa makubaliano ya kirafiki na JKCI.

 Watoto 79 walitibiwa kwenye kambi maalumu kuanzia mwaka 2015 hadi 2017 na kwamba huduma hizo ni bure kwa watoto wenye matatizo hayo.

 Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), watu milioni moja wanakadiriwa kuwa na tatizo la moyo.

Wema amfungukia Mke wa Nabii Tito


 Wema Sepetu.

Katika hali isiyotarajiwa, imeelezwa kuwa msanii nyota wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu, amemlipua mke wa ‘Nabii’ Tito baada ya mwanamke huyo kumshawishi kupitia mitandaoni aolewe na nabii huyo.

Chanzo chetu makini kilisema kuwa, msanii huyo amekasirishwa na kitendo cha mke huyo kumshawishi kuolewa na mumewe anayeitwa Onesmo Machija ‘Nabii Tito’ (44).

“Wema Sepetu nakupenda sana hata Nabii Tito anakupenda sana, kwanza mzuri, una shepu nzuri hata katika mambo ya Kiafrika unaongoza kwa uzuri.

“Nabii Tito huyo kwa watu wasiomfahamu wanasema sio nabii lakini kwa mimi ninayemfahamu na kuishi naye naona mambo ya kinabii anayofanya, nakuomba ukubali hata mimi nakupenda sana, kwanza una shepu nzuri.

“Uwe mke mwenzangu, ukubali kuwa mke wa Nabii Tito. Sikia kilio cha mke wa nabii,” amesikika kwenye video mke huyo wa Nabii Tito akimbembeleza Wema.

Naye Nabii Tito kwenye video hiyohiyo amechombeza kwa kubembeleza kwamba Wema akubali kuwa mkewe ili kanisa lao likuwe.

Alipotafutwa Wema na kuulizwa kuhusiana na video hiyo alisema, ameiona na amekasirishwa na kile walichokifanya nabii huyo na mkewe.

“Kiukweli wameniudhi sana kwa kunidhalilisha. Nawasiliana na mwanasheria wangu ili nimburuze mahakamani mwanamke huyo,” alisema Wema.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, mapema wiki hii lilimkamata nabii huyo na kumfanyia mahojiano kutokana na mahubiri ya kidini anayoyafanya na limesema mtu huyo ana matatizo ya akili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Gillesi Muroto amesema Juni 23, 2014, mtu huyo aliwahi kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu ya akili chini ya daktari aliyejulikana kwa jina moja la Dk. William ambapo aliporuhusiwa alitakiwa kurejea hospitalini hapo Julai 9 mwaka huohuo lakini hakurejea.

Kamanda Muroto aliendelea kusema kwamba, baada ya hapo Machija ambaye kanisa lake halijasajiliwa popote, aliibukia mkoani Dodoma katika Kijiji cha Nong’ona kilicho karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) akifanya mahubiri ya kidini yaliyodaiwa kuwa hayakuwa na maadili ya kidini.

“Kwa msingi huo, jeshi la polisi limempeleka Hospitali ya Rufaa ya Milembe iliyoko mkoani Dodoma kwa ajili ya kumpima tena matatizo hayo ya akili na baada ya majibu kutolewa, Dk. Dixon Philipo aliyemshughulikia alithibitisha kwamba bado ana matatizo hayo ya akili,” alisema kamanda Muroto juzi na kusisitiza kuwa wanaendelea kumshikilia kutokana na matendo yake aliyoyafanya ili kufanya uchunguzi zaidi.

Nabii Tito na mkewe pamoja na mfanyakazi wake wa ndani.