Thursday, 18 January 2018

Davido kuwaanika anaowadai



Unaweza ukasema ugumu wa mwezi Januari kwa upande wa uchumi ni kwa watu wakawaida lakini kumbe haipo hivyo hili ni janga hata kwa watu maarufu, Hii ni baada ya msanii wa muziki kutoka Nigeria, Davido kutangaza kuwa ataweka hadharani majina ya watu wote anaowadai kama hawatarudisha fedha zake kuanzia leo.

Davido kupitia ukurasa wake wa Snapchat amesema ametoa siku ya leo Jumatano kwa watu wote anaowadai ambao wapo jijini Lagos kutii amri hiyo la sivyo atatangaza majina hayo bila kuogopa ukubwa wa majina yao.

“Kupitia posti hiyo Davido amesema “Nitaweka orodha ya majina ya watu wote ninao wadai hapa Lagos, Watu wengi nimewakopesha pesa lakini hawataki kunilipa mimi sio serikali, Kama hutanilipa leo jina lako nitaliweka hadharani,” ameandika Davido.

Hata hivyo, watu wengi wanasema huenda hasira hizo zimekuja kutokana na Mamlaka ya mapato jijini Lagos kumtaka Davido atoe risiti za malipo ya kodi aliyolipa kwenye tamasha lake la 30 Bilioni Concert.


Pluijm awafungukia Simba




KUELEKEA mchezo wa Alhamis hii dhidi ya vinara Simba, kocha mkuu wa timu ya Singida United, Hans van der Pluijm amesema anawachukulia mabingwa hao wa zamani kama washindani wake wengine katika ligi na atakiingiza kikosi chake katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa ‘tahadhari’ kubwa licha ya ukweli haihofii timu hiyo iliyofunga magoli 12 katika michezo 12 iliyopita.

“Naichukulia Simba kama timu nyingine. Siwezi kuweka akili yangu yote kwao.” Anasema Hans nilipofanya naye mahojiano Jumanne hii. Inatakiwa tuwe makini na tucheze mchezo wetu kwa kujitambua na kuimarisha morali ya timu nzima. Inatakiwa tufanye kazi yetu vizuri katika kila nafasi na katika uchezaji wa mpira pia.”

Singida wamepanda daraja msimu huu lakini namna timu hiyo inavyoendeshwa imesaidia kwa  kiasi kikubwa kusajili wachezaji mahiri kutoka ndani na ng’ambo, ikiwemo kumtwaa kocha Hans ambaye aliipa Yanga mataji mawili mfululizo ya ligi kuu.

Mudathir Yahya, Ken Ally, Deus Kaseke, Kiggy Makassy, Daniel Lyanga, golikipa Peter Manyika ni baadhi ya nyota wazawa ambao wamesajiliwa na klabu msimu huu. Mzimbabwe, Tafadzwa Kutinyu, Mganda, Shafiq Batambuze,  Wanyarwanda, Michael Rusheshangoga, Danny Usengimana wamefanya kikosi hicho kuwa imara na ushindi wowote utawafanya kuwa pointi sawa na Simba.

Hans ni kocha mwenye uzoefu mkubwa sasa hadi katika soka la Tanzania. Amewahi kuishinda Simba katika michezo yote miwili ya ligi kuu msimu wa 2015/16 ameendeleza aina ya soka lake la kushambulia katika kikosi cha Singida. Atawavaa Simba kwa mara ya kwanza akiwa nje ya kikosi cha Yanga huku akiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo mmoja tu vs Simba.

“Mpira hautabiriki. Kila kitu kinawezekana, Simba bado ni timu kubwa na nawaheshimu lakini siwaogopi. Tunajiandaa vizuri na timu ipo katika morali, natumaini tunaweza kuwashangaza siku ya mchezo. Hii mechi wachezaji wanatakiwa wawe makini wao wenyewe ili tupate matokeo mazuri. Ni mechi yetu muhimu.” Anasema Hans ambaye atamkosa mfungaji wake namba moja Usengimana.

Singida wamekusanya alama 23 katika michezo 12 iliyopita. Wakiwa nafasi ya nne ya msimamo pointi  tatu nyuma ya Simba, timu hiyo kutoka mkoani Singida imeonyesha mwanga kuwa huenda wakawa washindani wa kweli katika mbio za ubingwa msimu huu kutokana na uimara wa timu yao.

“Njia bado ngumu, chochote kinaweza kutokea muda wowote. Tunaichukulia ligi ‘mchezo kwa mchezo’ mwishoni tutajua tulipofika. Inatakiwa tufanye kazi yetu vizuri.” Anamaliza kusema Hans.



Meli zilizokamatwa na madawa ya kulevya zafutiwa usajili




picha ya Mtandao

Serikali ya Tanzania imezifutia usajili meli mbili zilizokamatwa zikiwa na shehena ya madawa ya kulevya na silaha, huku ikikana kuhusika na mzigo uliokamatwa nao.

Taarifa hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu, na kusema kwamba meli hizo zilisajiliwa chini ya mamlaka ya usajili wa usafiri wa baharini, lakini hata hivyo zilishasajiliwa kinyume na sheria.

“Tanzania haihusiki na shehena za silaha wala mdawa ya kulevya yaliyokamatwa ndani ya meli hizo, bali ilitoa usajili wa meli hizo chini ya mamlaka za usajili ambao ni utaratibu wa kawaida wa kimataifa wa kusajili meli duniani, kwa hiyo kufuatia tukio hilo, tumezifutia usajili meli zote mbili, usajili ulitolewa chini ya taasisi ambayo ilishanyimwa kibali cha kusajili meli, na sasa meli zote zimeshusha bendera ya Tanzania ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa”, amesema Mama Samia Suluhu

Sambamba na hilo serikali imesema kuanzia sasa mamlaka husika inapitia taarifa za meli zote zilizosajiliwa nchini ili kuhakiki taarifa zake, na kutoa mapendekezo ya ushauri kwa serikali.

Meli hizo zenye namba za usajili IMO 6828753 ikiwa na kilo 1600 za dawa za kulevya kutoka Jamhuri ya Dominika, na nyingine yenye namba IMO 7614966 iliyokamwa ikiwa na silaha zilizokuwa zikisafirishwa kwenda Libya kinyume na sheria za kimataifa, zilikamatwa Desemba, 2017.

Theo Walcott atuma Ujumbe kwa mashabiki wa Arsenal


Inauma ukiondoka sehemu ambayo umeizoea kwa muda mrefu. Theo Walcott ametuma ujumbe kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal baada ya kuhamia Everton.

Mchezaji huyo ambaye amesajiliwa na Everton kwa ada ya uhamisho wa paund milioni 20 na kukabidhiwa jezi namba 11, amedumu Arsenal kwa miaka 12 na ameichezea jumla ya michezo 397 na kushinda magoli 108.

Huu ndio ujumbe ambao Walcott amewatumia mashabiki wa Arsenal:

Ninataka tu kusema shukrani kubwa kwa mashabiki wote wa Arsenal. Nimekuwa nimesumbuliwa na ujumbe ambao nimepata leo kheri na siwezi kukushukuru kwa kutosha, na hasa kwa miaka 12 iliyopita. Nataka tu kuwatakia kila mmoja katika klabu kila la kheri kwa siku zijazo




Amber Rose anatarajia kufanya upasuaji wa matiti



Mwanamitindo wa kimataifa Amber Rose anatarajiwa kufanya upasuaji wa matiti yake hivi karibuni.

Mrembo huyo ambaye alitangaza kuchoshwa na ukubwa matiti hayo ameamua kutilia mkazo suala lake la kuyapunguza ili yaweze kuendana na mwili wake kama yeye mwenyewe alivyodai.

Kwa mujibu wa mtandao wa Page Six imeelezwa kuwa baby mama huyo wa Wiz Khalifa na girlfriend wa rapper 21 Savage, atafanyiwa upasuaji wa kifua chake na Dr. Garth Fisher mapema leo.

Dkt. Fisher ameeleza kuwa Amber anahitaji kupunguza matiti hayo ili aweze kuwea huru “She wants to downsize so she can have more freedom.” Na kwa upande wa mrembo huyo ameeleza kuwa akipunguza matiti hayo atakuwa huru na ataweza kuvaa nguo zake amabzo hajazivaa takribani miaka 10 iliyopita.

MAGAZETI YA LEO 18/1/2018














Daktari wa kienyeji akamatwa na Polisi kwa kuwalaghai wanawake kuwa watashika mimba



Polisi nchini Guinea wanasema kuwa wamemkamata daktari mmoja wa kienyeji kwa kuwalaghai mamia ya wanawake na kuwafanya kuamini kuwa wao ni wajawazito.

N'na Fanta Camara aliwapa wanawake ambao hawakuwa na uwezo wa kuwa wajawazito , dawa ya kienyeji ambayo ilisababisha tumbo zao kufura na kuonekana kuwa wao ni wajawazito.

Kutokana na huduma hizo wagonjwa walilipa dola 33 kwenye nchi ambayo kipato cha kila mwezi kinakadiriwa kuwa dola 48.

Polisi wanaamini kuwa Bi Camara alipata maelfu ya dola kila mwezi licha ya yeye kusema kuwa alijaribu tu kusaidia.

Siku ya Jumanne zaidi ya wanawake 200 waliandamana nje ya kituo cha polisi kwenye mji mkuu wa Guinea Conakry ambapo Bi Camara alikuwa akizuiliwa.

Zaidi ya wanawake 700 walio na kati ya umri wa miaka 17 na 45 wanaamiwa kuathiriwa na matibabu ya Bi Camara.

Idadi hiyo kubwa inaashiria jinsi Guinea na nchi zingine za Afrika zinawategemea madaktari wa kienyeji

Mwaka 2006 shirika la afya duniani lilisema kuwa asilimia 80 ya waafrika walitumia matibabu ya kienyeji

Baadhi ya wanawake walisema kuwa walionekana kuwa wajawazito kwa kati ya miezi 12 na 16.
Wanawake hao walisema kuwa Bi Camara aliwashauri wasimuone daktari, na mara alipothibitisha kuwa wamekuwa wajawazito walistahili kumpa kuku na vitambaa kama njia ya kumshukuru.

Baadhi ya wanawake walisema kuwa walionekana kuwa wajawazito kwa kati ya miezi 12 na 16.

Daktari aliyewachunguza 47 kati ya wanawake walioathiriwa alisema wako kwenye hatari ya kukumbwa na matatizo ya kiafya ya muda mrefu kutokana na matibabu hayo.

Bi Camara hata hivyo anasema kuwa hajafanya lolote baya.

"Ninafanya kazi ngumu sana kuwasaidia wanawake kuweza kutimiza ndoto zao lakini mengine yako mikononi mwa Mungu, aliwambia waandishi wa habari mjini Conakry.

Nini amkana Ney wa Mitego




MSANII chipukizi wa Bongo Fleava, Nini amefunguka kuhusu uhusiano wake na Nay wa Mitego na kueleza kuwa hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapper huyo.

Kauli ya Nini anakuja baada ya hapo awali kuwepo taarifa kuwa sababu ya kutimuliwa MJ Record ni kuwa na mahusiano na Nay.

“Sina mahusiano ya kimapenzi na Nay, halafu hata kama ningekuwa nayo, kiupande wangu I don’t real think hiyo ni sababu ambayo ingeweza kumfanya yeye afanye kile alichokifanya,” amesema.

“Seriously sidhani kama mahusiano ya kimapenzi yanaweza kuathiri muziki, sina uhakika may be according to me navyofikiria lakini sidhani kama hiyo it can be specific reason,” amesisitiza.

Anusurika Kifo akipambana na Mamba kwa zaidi ya saa moja


MKAZI wa Kijiji cha Mkombe Kata ya Kabwe wilayani Nkasi, John Mwipungi (30), amenusurika kifo baada ya kupambana na mamba kwa zaidi ya saa moja.

Mwipungi akikumbana na mkasa huo alipokwenda mtoni kunawa miguu baada ya kutoka shambani.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 11 baada ya Mwipungu kufika mtoni  kisha kuanza kunawa miguu kutoa tope baada ya kutoka katika shamba lake alikokuwa aking’oa majani katika  mpunga.

Diwani wa Kabwe, Asante Lubisha, alisema majeru huyo alifika mtoni hapo na kuanza kunawa huku akiwa ameinama bila kuona kama kuna mamba katika eneo hilo.

Alisema wakati akiendelea kunawa miguu, ghafla aliibuka mamba mkubwa na kumvutia ndani ya mto, lakini kwa kuwa alikuwa anajua  kuogelea alipambana naye ndani ya maji.

Alisema ujuzi wa kuogelea ulimsaidia Mwipungi kwa sababu  aliamua kuvutana na mambo huyo eneo ambalo lina kina kirefu, hali iliyosababisha mamba huyo kushindwa kumuua na  ilichukua saa nzima kupambana majini huku akipiga kelele za kuomba msaada.

Diwani huyo alisema Mwipungi alijeruhiwa na mamba huyo katika mguu wake wa kulia.

Aliongeza kuwa kutokana na kelele alizokuwa akipiga za kuomba msaada, wanakijiji walifika na kumtoa majini akiwa amejeruhiwa kisha kumkimbiza katika Zahanati ya Kabwe kupatiwa matibabu ya jelaha la mguu.

Diwani huyo alisema wananchi wamekuwa wakiuawa na mamba katika mto huo na kuwa mwaka jana mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kabwe wa darasa la sita aliliwa na mamba wakati  akivuka katika mto Mkombe.

Alisema Kijiji cha Kabwe kimapakana na Pori la Akiba la Lwafi, hali inayosababisha wanyama wa hatari kama mamba, tembo, viboko na nyati kuingia kijijini hapo, hivyo kuhatarisha maisha ya wakazi wa kijiji hicho.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kabwe, Gwira Aron,  alisema majeruhi huyo alipatiwa matibabu na anaendelea vizuri.



Sanchez rasmi Man United



Alexis Sanchez amekubali kujiunga na Manchester United, hii sasa ni rasmi. Kikubwa kinachosubiriwa ni uamuzi wa kiungo Henrikh Mkhitaryan ambaye Arsenal inamtaka kama sehemu ya mauzo ya Sanchez.

Mkhitaryan alionekana kuwa anasita kujiunga na Arsenal lakini yuko katika hatua za mwisho kwa kuwa Kocha Jose Mourinho ameonekana kumruhusu aondoke.

Katika makubaliano, Sanchez amekubali kuwa Shetani Mwekundu kwa dili la miaka minne na nusu likiwa na thamani ya pauni milioni 14 kwa kila msimu.


Rais Magufuli amteua Dk Mwinuka kuwa Mkurugenzi wa Tanesco



Dar es Salaam.Rais  John Magufuli amemteua Dk Titus Mwinuka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco).

Kabla ya Utendaji huu Dk Mwinuka alikuwa akikaimu Nafasi hiyo.

Awali Dk Mwinuka alikuwa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).

Na pia alikuwa ni Mkuu wa Idara ya Mekanika na Uhandisi wa Viwanda Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

TFF yaishukia Yanga madai kuibeba Simba



OFISA WA HABARI WA TFF, CLIFFORD NDIMBO.

BAADA ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, kutoa malalamiko kuhusiana na matumizi ya Uwanja wa Taifa, Shirikisho la Soka Nchini (TFF) limetoa ufafanuzi kuhusiana na matumizi ya uwanja huo unaomilikiwa na serikali.

Yanga kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Boniface Mkwasa, ilisema kuwa TFF inaependelea Simba na kuipanga itumie Uwanja wa Taifa na wao ikiwapangia mechi zao kwenye Uwanja wa Uhuru.

Ofisa wa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, alisema jana katika taarifa yake kuwa Bodi ya Ligi ndiyo inayosimamia ligi na hupanga mechi kwa kuzingatia viwanja vilivyochaguliwa na klabu.

Ndimbo alisema katika taarifa yake kuwa katika upangaji wa ratiba hizo pamoja na viwanja, Kaimu Mwenyekiti wa Yanga ambaye ni Mwenyekiti wa klabu hiyo ni mmoja wa watendaji wa bodi hivyo hakuna suala la upendeleo kwenye upangaji wa matumizi wa Uwanja wa Taifa.

"TFF hatuamini kama Mkwasa anaweza kuzungumza maneno hayo kwa sababu anaujua utaratibu na anafahamu kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga (Clement Sanga) ndiye Mwenyekiti wa Bodi ambaye angempa sababu kwa nini Simba wameruhusiwa kucheza kesho (leo) na Yanga wataruhusiwa kucheza mechi ijayo," ilisema sehemu ya taarifa.

Afisa huyo aliongeza kuwa TFF inasisitiza kufuatwa na kuheshimiwa kwa kanuni na taratibu za mpira wa miguu huku ikiendelea kufanya kazi kwa karibu na Yanga kwenye mambo mbalimbali na kuhakikisha inaisaidia kukabiliana na changamoto zinazotokea kwenye klabu hiyo.

Nafasi za kazi leo Jan 18