Thursday, 18 January 2018

Meli zilizokamatwa na madawa ya kulevya zafutiwa usajili




picha ya Mtandao

Serikali ya Tanzania imezifutia usajili meli mbili zilizokamatwa zikiwa na shehena ya madawa ya kulevya na silaha, huku ikikana kuhusika na mzigo uliokamatwa nao.

Taarifa hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu, na kusema kwamba meli hizo zilisajiliwa chini ya mamlaka ya usajili wa usafiri wa baharini, lakini hata hivyo zilishasajiliwa kinyume na sheria.

“Tanzania haihusiki na shehena za silaha wala mdawa ya kulevya yaliyokamatwa ndani ya meli hizo, bali ilitoa usajili wa meli hizo chini ya mamlaka za usajili ambao ni utaratibu wa kawaida wa kimataifa wa kusajili meli duniani, kwa hiyo kufuatia tukio hilo, tumezifutia usajili meli zote mbili, usajili ulitolewa chini ya taasisi ambayo ilishanyimwa kibali cha kusajili meli, na sasa meli zote zimeshusha bendera ya Tanzania ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa”, amesema Mama Samia Suluhu

Sambamba na hilo serikali imesema kuanzia sasa mamlaka husika inapitia taarifa za meli zote zilizosajiliwa nchini ili kuhakiki taarifa zake, na kutoa mapendekezo ya ushauri kwa serikali.

Meli hizo zenye namba za usajili IMO 6828753 ikiwa na kilo 1600 za dawa za kulevya kutoka Jamhuri ya Dominika, na nyingine yenye namba IMO 7614966 iliyokamwa ikiwa na silaha zilizokuwa zikisafirishwa kwenda Libya kinyume na sheria za kimataifa, zilikamatwa Desemba, 2017.

Theo Walcott atuma Ujumbe kwa mashabiki wa Arsenal


Inauma ukiondoka sehemu ambayo umeizoea kwa muda mrefu. Theo Walcott ametuma ujumbe kwa mashabiki wa klabu ya Arsenal baada ya kuhamia Everton.

Mchezaji huyo ambaye amesajiliwa na Everton kwa ada ya uhamisho wa paund milioni 20 na kukabidhiwa jezi namba 11, amedumu Arsenal kwa miaka 12 na ameichezea jumla ya michezo 397 na kushinda magoli 108.

Huu ndio ujumbe ambao Walcott amewatumia mashabiki wa Arsenal:

Ninataka tu kusema shukrani kubwa kwa mashabiki wote wa Arsenal. Nimekuwa nimesumbuliwa na ujumbe ambao nimepata leo kheri na siwezi kukushukuru kwa kutosha, na hasa kwa miaka 12 iliyopita. Nataka tu kuwatakia kila mmoja katika klabu kila la kheri kwa siku zijazo




Amber Rose anatarajia kufanya upasuaji wa matiti



Mwanamitindo wa kimataifa Amber Rose anatarajiwa kufanya upasuaji wa matiti yake hivi karibuni.

Mrembo huyo ambaye alitangaza kuchoshwa na ukubwa matiti hayo ameamua kutilia mkazo suala lake la kuyapunguza ili yaweze kuendana na mwili wake kama yeye mwenyewe alivyodai.

Kwa mujibu wa mtandao wa Page Six imeelezwa kuwa baby mama huyo wa Wiz Khalifa na girlfriend wa rapper 21 Savage, atafanyiwa upasuaji wa kifua chake na Dr. Garth Fisher mapema leo.

Dkt. Fisher ameeleza kuwa Amber anahitaji kupunguza matiti hayo ili aweze kuwea huru “She wants to downsize so she can have more freedom.” Na kwa upande wa mrembo huyo ameeleza kuwa akipunguza matiti hayo atakuwa huru na ataweza kuvaa nguo zake amabzo hajazivaa takribani miaka 10 iliyopita.

MAGAZETI YA LEO 18/1/2018














Daktari wa kienyeji akamatwa na Polisi kwa kuwalaghai wanawake kuwa watashika mimba



Polisi nchini Guinea wanasema kuwa wamemkamata daktari mmoja wa kienyeji kwa kuwalaghai mamia ya wanawake na kuwafanya kuamini kuwa wao ni wajawazito.

N'na Fanta Camara aliwapa wanawake ambao hawakuwa na uwezo wa kuwa wajawazito , dawa ya kienyeji ambayo ilisababisha tumbo zao kufura na kuonekana kuwa wao ni wajawazito.

Kutokana na huduma hizo wagonjwa walilipa dola 33 kwenye nchi ambayo kipato cha kila mwezi kinakadiriwa kuwa dola 48.

Polisi wanaamini kuwa Bi Camara alipata maelfu ya dola kila mwezi licha ya yeye kusema kuwa alijaribu tu kusaidia.

Siku ya Jumanne zaidi ya wanawake 200 waliandamana nje ya kituo cha polisi kwenye mji mkuu wa Guinea Conakry ambapo Bi Camara alikuwa akizuiliwa.

Zaidi ya wanawake 700 walio na kati ya umri wa miaka 17 na 45 wanaamiwa kuathiriwa na matibabu ya Bi Camara.

Idadi hiyo kubwa inaashiria jinsi Guinea na nchi zingine za Afrika zinawategemea madaktari wa kienyeji

Mwaka 2006 shirika la afya duniani lilisema kuwa asilimia 80 ya waafrika walitumia matibabu ya kienyeji

Baadhi ya wanawake walisema kuwa walionekana kuwa wajawazito kwa kati ya miezi 12 na 16.
Wanawake hao walisema kuwa Bi Camara aliwashauri wasimuone daktari, na mara alipothibitisha kuwa wamekuwa wajawazito walistahili kumpa kuku na vitambaa kama njia ya kumshukuru.

Baadhi ya wanawake walisema kuwa walionekana kuwa wajawazito kwa kati ya miezi 12 na 16.

Daktari aliyewachunguza 47 kati ya wanawake walioathiriwa alisema wako kwenye hatari ya kukumbwa na matatizo ya kiafya ya muda mrefu kutokana na matibabu hayo.

Bi Camara hata hivyo anasema kuwa hajafanya lolote baya.

"Ninafanya kazi ngumu sana kuwasaidia wanawake kuweza kutimiza ndoto zao lakini mengine yako mikononi mwa Mungu, aliwambia waandishi wa habari mjini Conakry.

Nini amkana Ney wa Mitego




MSANII chipukizi wa Bongo Fleava, Nini amefunguka kuhusu uhusiano wake na Nay wa Mitego na kueleza kuwa hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapper huyo.

Kauli ya Nini anakuja baada ya hapo awali kuwepo taarifa kuwa sababu ya kutimuliwa MJ Record ni kuwa na mahusiano na Nay.

“Sina mahusiano ya kimapenzi na Nay, halafu hata kama ningekuwa nayo, kiupande wangu I don’t real think hiyo ni sababu ambayo ingeweza kumfanya yeye afanye kile alichokifanya,” amesema.

“Seriously sidhani kama mahusiano ya kimapenzi yanaweza kuathiri muziki, sina uhakika may be according to me navyofikiria lakini sidhani kama hiyo it can be specific reason,” amesisitiza.

Anusurika Kifo akipambana na Mamba kwa zaidi ya saa moja


MKAZI wa Kijiji cha Mkombe Kata ya Kabwe wilayani Nkasi, John Mwipungi (30), amenusurika kifo baada ya kupambana na mamba kwa zaidi ya saa moja.

Mwipungi akikumbana na mkasa huo alipokwenda mtoni kunawa miguu baada ya kutoka shambani.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 11 baada ya Mwipungu kufika mtoni  kisha kuanza kunawa miguu kutoa tope baada ya kutoka katika shamba lake alikokuwa aking’oa majani katika  mpunga.

Diwani wa Kabwe, Asante Lubisha, alisema majeru huyo alifika mtoni hapo na kuanza kunawa huku akiwa ameinama bila kuona kama kuna mamba katika eneo hilo.

Alisema wakati akiendelea kunawa miguu, ghafla aliibuka mamba mkubwa na kumvutia ndani ya mto, lakini kwa kuwa alikuwa anajua  kuogelea alipambana naye ndani ya maji.

Alisema ujuzi wa kuogelea ulimsaidia Mwipungi kwa sababu  aliamua kuvutana na mambo huyo eneo ambalo lina kina kirefu, hali iliyosababisha mamba huyo kushindwa kumuua na  ilichukua saa nzima kupambana majini huku akipiga kelele za kuomba msaada.

Diwani huyo alisema Mwipungi alijeruhiwa na mamba huyo katika mguu wake wa kulia.

Aliongeza kuwa kutokana na kelele alizokuwa akipiga za kuomba msaada, wanakijiji walifika na kumtoa majini akiwa amejeruhiwa kisha kumkimbiza katika Zahanati ya Kabwe kupatiwa matibabu ya jelaha la mguu.

Diwani huyo alisema wananchi wamekuwa wakiuawa na mamba katika mto huo na kuwa mwaka jana mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kabwe wa darasa la sita aliliwa na mamba wakati  akivuka katika mto Mkombe.

Alisema Kijiji cha Kabwe kimapakana na Pori la Akiba la Lwafi, hali inayosababisha wanyama wa hatari kama mamba, tembo, viboko na nyati kuingia kijijini hapo, hivyo kuhatarisha maisha ya wakazi wa kijiji hicho.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kabwe, Gwira Aron,  alisema majeruhi huyo alipatiwa matibabu na anaendelea vizuri.



Sanchez rasmi Man United



Alexis Sanchez amekubali kujiunga na Manchester United, hii sasa ni rasmi. Kikubwa kinachosubiriwa ni uamuzi wa kiungo Henrikh Mkhitaryan ambaye Arsenal inamtaka kama sehemu ya mauzo ya Sanchez.

Mkhitaryan alionekana kuwa anasita kujiunga na Arsenal lakini yuko katika hatua za mwisho kwa kuwa Kocha Jose Mourinho ameonekana kumruhusu aondoke.

Katika makubaliano, Sanchez amekubali kuwa Shetani Mwekundu kwa dili la miaka minne na nusu likiwa na thamani ya pauni milioni 14 kwa kila msimu.


Rais Magufuli amteua Dk Mwinuka kuwa Mkurugenzi wa Tanesco



Dar es Salaam.Rais  John Magufuli amemteua Dk Titus Mwinuka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco).

Kabla ya Utendaji huu Dk Mwinuka alikuwa akikaimu Nafasi hiyo.

Awali Dk Mwinuka alikuwa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).

Na pia alikuwa ni Mkuu wa Idara ya Mekanika na Uhandisi wa Viwanda Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

TFF yaishukia Yanga madai kuibeba Simba



OFISA WA HABARI WA TFF, CLIFFORD NDIMBO.

BAADA ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, kutoa malalamiko kuhusiana na matumizi ya Uwanja wa Taifa, Shirikisho la Soka Nchini (TFF) limetoa ufafanuzi kuhusiana na matumizi ya uwanja huo unaomilikiwa na serikali.

Yanga kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Boniface Mkwasa, ilisema kuwa TFF inaependelea Simba na kuipanga itumie Uwanja wa Taifa na wao ikiwapangia mechi zao kwenye Uwanja wa Uhuru.

Ofisa wa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, alisema jana katika taarifa yake kuwa Bodi ya Ligi ndiyo inayosimamia ligi na hupanga mechi kwa kuzingatia viwanja vilivyochaguliwa na klabu.

Ndimbo alisema katika taarifa yake kuwa katika upangaji wa ratiba hizo pamoja na viwanja, Kaimu Mwenyekiti wa Yanga ambaye ni Mwenyekiti wa klabu hiyo ni mmoja wa watendaji wa bodi hivyo hakuna suala la upendeleo kwenye upangaji wa matumizi wa Uwanja wa Taifa.

"TFF hatuamini kama Mkwasa anaweza kuzungumza maneno hayo kwa sababu anaujua utaratibu na anafahamu kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga (Clement Sanga) ndiye Mwenyekiti wa Bodi ambaye angempa sababu kwa nini Simba wameruhusiwa kucheza kesho (leo) na Yanga wataruhusiwa kucheza mechi ijayo," ilisema sehemu ya taarifa.

Afisa huyo aliongeza kuwa TFF inasisitiza kufuatwa na kuheshimiwa kwa kanuni na taratibu za mpira wa miguu huku ikiendelea kufanya kazi kwa karibu na Yanga kwenye mambo mbalimbali na kuhakikisha inaisaidia kukabiliana na changamoto zinazotokea kwenye klabu hiyo.

Nafasi za kazi leo Jan 18

Waombolezaji wasambaratika baada ya mtu aliyedhaniwa amekufa kuibukia msibani


Kenya: Wakazi wa kijiji cha Marindi huko Kaunti ya Migori walipaniki na kuchanganyikiwa baada mwanaume wa miaka 35 ambaye aliaminika kuwa amefariki kuibukia msibani nyumbani kwake ghafla

Familia ya mwanaume huyo walikuwa wakimalizia mipango ya mazishi ndipo Okelo Nyamwaga alipojitokeza

Kufika kwake huko kusikotarajiwa kulileta hofu na furaha katika familia yake na marafiki na waombolezaji wengine kukimbia

Nyamwaga alikuwa amepotea kwa miezi miwili na familia yake ilipoteza matumaini ya kumpata akiwa hai

Wiki moja iliyopita marafiki wa Nyamwanga walisema mwili wake ukiwa umeharibika ulikuwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Migori

Mwili huo uliokotwa mtoni ukiwa umeharibika na kupelekwa mochwari


Kimbitor kugombea Ubunge jimbo la Kinondoni



Dar es Salaam. Diwani wa kata ya Hananasifu (Chadema), Ray Kimbitor amepitishwa na mkutano mkuu wa wilaya ya Kinondoni kugombea ubunge jimbo la Kinondoni.

Akitangaza matokeo hayo jana usiku mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kinondoni, Waziri Muhunzi amesema matokeo hayo watayawasilisha Kamati Kuu Taifa ya chama hicho kwa ajili ya kupata baraka.

Amesema Kimbitor amepata kura 40 na kuwashinda wagombea wengine sita.

Amesema wajumbe wa mkutano huo walikuwa 102 na kura zilizoharibika ni tano.

“Kimbitor amepata kura 40 na kufuatiwa na Mustapher Muro (diwani Kinondoni) aliyepata kura 33,” amesema.

Amesema Rose Moshi amepata kura 5, Nicolas Mkwama kura 16, David Asey kura 2, Moza Ally kura moja huku Juma Uloleulole ambaye ni diwani kata ya Kijitonyama akipata kura sifuri.

Hata hivyo, jana Katibu wa Mambo ya Nje na Itifaki wa Chadema, John Mrema alilieleza Mwananchi kuwa chama kingetoa msimamo huo jana baada ya kuunda kamati ndogo kufanya utafiti, lakini akasema Chadema haikutoa baraka za kufanyika kwa mchakato wa ndani wa kuchukua fomu na kupitisha wagombea.