Tuesday, 12 December 2017

Hili ndilo Kombora jipya la korea Kaskazini Linaloweza Kuitandika Marekani


Korea Kaskazini imetoa picha za jaribio la kombora lake jipya ambalo inadai kuwa linaweza kushambulia popote pale nchini Marekani.

Picha hizo zinaonyesha kiongozi wa Korea Kaskazini Ki Jong un na maafisa wengine kadha ya ngazi za juu jeshini wakisherehekea kombora la Hwasong-15 wakati likipaa.

Wengi wameshangazwa na ukubwa wa kombora hilo. Picha hii ambayo haijulikanai ilichukuliwa lini na iliyotolewa na vyombo vya habari vya taifa inaonyesha Kim akilikagua kombora hilo.

Michael Duitsman, mtafiti katika kituo kimoja alisema kuwa kombora hilo ni kubwa kuliko kombora la kwanza la Hwasong-14 "ni nchi chache tu zinaweza kuunda kombora kama hilo na Korea Kaskazini imejiunga nazo."

Pia linaonekana kuwa na kichwa kikubwa ikimaanisha kuwa linaweza kubeba bomu zito la nyuklia kwenye kichwa chake.

Yote haya yanaashiria kuwa kombora hilo lina uwezo kwa kusafirisha bomu la nyuklia kwa muda mrefu.

Lilisherehekewa kwa sigara

Kim mwenye furaha anaonekana akicheka kwa furaha  wakati kombora hilo linapaa. Linaaminiwa kuwa kombora la kwanza la Korea Kaskazini lililopaa mbali zaidi katika kilomita 4,475.

Bw Kim na wenzake walionekana wakisherehekea  mafanikio ya jaribio hilo kwa sigara.

Credit: BBC


Askari wa usalama Barabarani wazuia magari zaid ya 10 kusafiri




Dar es Salaam. Askari wa usalama barabarani wamezuia magari zaidi ya 10 kufanya safari za mikoani kwa ajili ya ukaguzi katika kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Usalama Barabarani Ubungo, Said Ibrahimu akizungumza na MCL Digital leo Jumanne Desemba 12,2017 amesema wanaendelea na ukaguzi na kwamba magari yaliyozuiwa ni mabovu.

Katika kituo hicho idadi ya abiria imeongezeka ikielezwa ni kutokana na sherehe za mwishoni mwa mwaka.

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) jana Jumatatu Desemba 11,2017 kupitia taarifa kwa umma imetangaza kutoa leseni za muda mfupi katika kipindi cha mwisho wa mwaka.

Sumatra imewaalika wamiliki wenye mabasi ya ziada kuwasilisha maombi ya leseni za muda mfupi kwa ajili ya kuongeza huduma katika njia za mikoani zenye mahitaji zaidi kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Mamlaka hiyo pia imewakumbusha wananchi wanaotarajia kusafiri kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kupanga safari mapema ili kuepusha usumbufu unaotokana na changamoto za usafiri.

Ofisa Mtendaji Mkuu NMG kujiuzulu



  Dar es Salaam. Bodi ya kampuni ya Nation Media Group (NMG) imetangaza kujiuzulu kwa Ofisa Mtendaji Mkuu, Joseph Muganda kuanzia Januari 31, 2018.

Taarifa iliyotolewa jana na mwenyekiti wa Bodi ya NMG, Wilfred Kiboro inaeleza kuwa kutokana na kuondoka kwake, Mkurugenzi wa Fedha wa NMG, Stephen Gitagama atakaimu nafasi hiyo wakati bodi ikitafuta mtu atakayemrithi Muganda.

Muganda alijiunga na NMG Julai, 2015 na amefanikiwa kuongoza mkakati wa kuifanya kampuni ikue vizuri katika safari mpya ya kidigitali.

“Muganda ameongoza kwa ujasiri kutathmini biashara ya bidhaa zetu, ameongoza kufanya mageuzi ya kimfumo na kuielekeza tena kampuni katika kutumia fursa zilizojitokeza kutokana na mitandao ya jamii kuvuruga sekta ya habari,” anasema Kiboro katika taarifa yake.

“Ataiacha kampuni ikiwa inawaelewa wateja na iliyobadilika kwa haraka na ambayo mafanikio yake kibiashara tayari ni dhahiri kwa kuangalia matarajio ya faida kutokana na uwekezaji katika mikakati ya kidigitali. Tunamtakia mafanikio katika mipango yake ya baadaye.”

Kiboro amewahakikishia wanahisa na wadau wote wa NMG na umma kwamba kwamba kipindi cha mpito cha mabadiliko ya uongozi hakitakuwa na matatizo na kitafanyika kwa haraka.

NMG, ambayo inamilikiwa na umma, ni kampuni yenye mafanikio makubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na inajivunia mafanikio ya kidigitali, ikiwa na watu milioni 30 wanaotembelea kurasa zake.

NMG inachapisha magazeti ya Nation na Taifa Leo nchini Kenya, The EastAfrican ambalo ni la kanda ya Afrika Mashariki na Kati, Daily Monitor la Uganda, na Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti ya Tanzania na pia matoleo ya kielektroniki.

Pia inamiliki vituo vya televisheni vya NTV Kenya, na NTV na Spark pamoja na vituo vya redio vya KFM na Dembe nchini Uganda. Pia inamiliki kituo cha redio cha Nation FM cha Kenya.

NMG imejisajili katika masoko ya hisa ya Kampala, Dar es Salaam na Kigali.

Idara ya Uhamiaji yamuhoji Askofu wa Katoliki kuhusu uraia wake



Askofu Severine Niwemugizi.

ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Rulenge, Wilaya ya Ngara, mkoani Kagera, Severine Niwemugizi (61), amehojiwa na Idara ya Uhamiaji kuhusiana na uraia wake. Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Askofu Niwemugizi alisema mara ya kwanza alihojiwa Novemba 28 mwaka huu na mara ya pili alihojiwa Desemba 4, mwaka huu.

“Mara ya kwanza niliitwa na kufika ofisi za uhamiaji Ngara, Novemba 28 na mara ya pili niliitwa Desemba 4.

“Niliombwa kibali kinachoniruhusu kuwa nchini, nikashangaa, nikasema mimi ni Mtanzania, nikaambiwa nilete document (nyaraka).

“Nilipeleka hati ya kusafiria, kitambulisho cha kupigia kura na cheti cha kuzaliwa, wakasema wataniita tena.

“Baada ya kuitwa mara ya pili, nilipewa fomu ya kujaza ambayo bado naendelea kuijaza hadi sasa.

“Waliniita tena wakasema bado wanataka kujiridhisha ndio maana wanataka nijaze fomu,
ninaendelea kuifanyia kazi mpaka nitakapokuwa nimeikamilisha yote,” alisema Askofu Niwemugizi ambaye amewahi kuwa Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC).

Mahojiano kati yake na Mwandishi wa Mtanzania yalikuwa hivi.

Swali: Je, ulizaliwa wapi?

Jibu: Nilizaliwa katika Kitongoji cha Kayanza, Kijiji cha Kabukome, Kata ya Nyarubungo, Wilaya ya Biharamulo.

Swali: Ulizaliwa tarehe ngapi?

Jibu: Nilizaliwa Juni 3, mwaka 1956.

Swali: Ulibatizwa wapi?

Jibu: Nilibatizwa katika Parokia ya Katoke, Biharamulo.

Swali: Elimu ya Msingi na Sekondari ulisoma wapi?

Jibu: Nilisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo na Shule ya Sekondari Nyakato Bukoba (O-level).

Baada ya kumaliza ‘O-level’ niliingia Seminari Kuu ya Ntungamo Bukoba halafu nikatoka hapo nikaenda Kipalapala Tabora.

Swali: Wazazi wako walizaliwa wapi?

Jibu: Walizaliwa sehemu mbalimbali, mama alizaliwa Lusahunga na baba alizaliwa katika Tarafa ya Nyarubungo, Kijiji cha Kabukome Kitongoji cha Kayanza.

Swali: Katika maisha yako yote je, ulishawahi kuhisiwa kuhusu uraia wako?

Jibu: Sijawahi kuulizwa, muda wote nimetumia passport (hati ya kusafiria) ya Tanzania na hakuna aliyewahi kuniuliza suala la uraia.

Swali: Je, unafikiri kwanini hili linajitokeza sasa?

Jibu: Baada ya hivi karibuni kutoa ushauri, kwamba ni vizuri mchakato wa Katiba ukarejewa, watu wali-react, sasa naweza kupata picha nini kimesababisha nianze kuhojiwa.

Swali: Je, Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC) wana taarifa kwamba umeitwa uhamiaji?
Jibu: Sijawataarifu kwa sababu suala hili lilionekana bado liko chini chini, lakini nafikiri nitatafuta namna ya kuwafahamisha juu ya jambo hili.

Swali: Je, mbali na kuwa Askofu, uliwahi kushika nafasi gani katika Kanisa Katoliki?

Jibu: Niliwahi kuwa Rais wa TEC, kuanzia mwaka 2000 hadi 2006 na baadaye nikawa Mkamu wa Rais kuanzia mwaka 2012 hadi 2015.

Swali: Je, una hofu yoyote juu ya usalama wako?

Jibu: Mimi sina hofu na usalama kwa sababu ninajua kufa ni mara moja. Kwa hiyo, ninabaki kivulini, ninazungumza tu ninavyowajibika kama askofu.

UHAMIAJI

MTANZANIA lilizungumza na Msemaji Mkuu Idara ya Uhamiaji, Mrakibu Ally Mtanda, ambaye alikiri askofu huyo kuhojiwa.

“Ni kweli anahojiwa na ofisi yetu ya Wilaya ya Ngara, ni suala tu la tuhuma si kwamba ni kweli au la, hivyo itakapothibitika basi itajulikana,” alisema Mtanda.

Peter Msigwa awajia juu CCM



Mbunge wa Iringa Mjini  CHADEMA, Peter Msigwa amewavaa baadhi ya viongozi wa CCM ambao wamekuwa wakisema upinzani Tanzania unakufa na kuwahoji kuwa endapo upinzani ukifa ndiyo maendeleo ya nchi yatapatikana.

Msigwa amesema hayo jana kupitia ukurasa wake wa Facebook baada ya juzi baadhi ya viongozi wa CCM waliokuwepo kwenye Mkutano Mkuu UVCCM wa 9 ambao ulifanyika mjini Dodoma Disemba 10, 2017 ambapo wapo baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho walikuwa wakisema kuwa kwa sasa upinzani nchini unakufa.

"Mkutano wa UVCCM ulibebwa na kibwagizo cha upinzani kuwa unakufa ! Fine, tukubaliane kuwa upinzani unakufa! Ukifa upinzani zitaongezeka ajira ngapi! Umaskini utapungua kwa kiwango gani?

Haki za binadamu zitalindwa kwa kiwango gani? Utawala bora utaimarika kwa kiwango gani ?

Demokrasia itaimarishwa kwa kiwango gani? Uhuru wa kutoa mawazo na vyombo vya habari utaimarika kwa kiwango gani! Haya yote hayana chama! Nilitegemea CCM mje na majibu ya haya sio upinzani unakufa" alisisitiza Msigwa

Mpanda majengo marefu China afariki akionyesha ujuzi wake



Mpanda mijengo mirefu ambaye ni maarufu sana nchini China amefariki akionyesha moja ya ujuzi wake hatari.

Wu Yongning alikuwa amejizolea maelfu ya mashabiki kwenye mtandao ya kijamii wa Weibo, kutokana na video zake fupi za kutisha akiwa juu ya majengo marefu bila ya kuchukua tahadhari zozote za kiusalama.

Wasi wasi uliwaingia mashabiki wake wakati aliacha kuchapisha video zake mwezi Novemba.


Jiwe kubwa linalocheza nchini Tanzania
Mzee mwenye watoto 70 na wajukuu 300 Tanzania
Pacha waliotungwa siku tofauti Australia


Sasa imeibuka kuwa alikufa baada ya kuanguka kutoka jumba la ghorofa 62 kwenye mji wa Changsha.

Vyombo vya habari nchini China vinasema kuwa alikuwa akishiriki kwenye mchezo wa kushinda pesa nyingi


























 Facebook  Twitter  Google+  Pinterest  Linkedin
Newer Post Older Post
POPULAR
Mama Mzazi wa Diamond: "Nimeolewa na Diamond asubiri mdogo Wake"
Mama Mzazi wa Diamond: "Nimeolewa na Diamond asubiri mdogo Wake"
Jeshi la Malaysia lipo tayari kuukomboa mji wa Jerusalem
Jeshi la Malaysia lipo tayari kuukomboa mji wa Jerusalem
FULL VIDEO: Babu Seya na Papi Kocha wakitoka Gerezani
FULL VIDEO: Babu Seya na Papi Kocha wakitoka Gerezani
Breaking News: Rais Magufuli afanya uteuzi kwa watu 6
Breaking News: Rais Magufuli afanya uteuzi kwa watu 6
Sababu ya kuaachiwa Babu Seya yatajwa
Sababu ya kuaachiwa Babu Seya yatajwa
MAGAZETI YA LEO 10/12/2017
MAGAZETI YA LEO 10/12/2017
Kisa Babu Seya mashabiki wamvaa Zitto
Kisa Babu Seya mashabiki wamvaa Zitto
Rais Kenyatta amuandikia barua Rais Magufuli
Rais Kenyatta amuandikia barua Rais Magufuli
Walimu wapigana ofisini
Walimu wapigana ofisini
MAGAZETI YA LEO 8/12/2017

Rais Magufuli anataraji kufungua mkutano wa jumuiya ya Wazazi



Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais John Magufuli anatarajiwa kufungua mkutano mkuu wa Taifa wa tisa wa Jumuiya ya Wazazi mjini Dodoma.

Mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete pia umehudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan; Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa; Mama Maria Nyerere; na viongozi wengine wa CCM.

Katika mkutano huo, mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo atakabidhi mikoba kwa kiongozi mpya atakayechaguliwa.

Imeelezwa mkutano huo utakuwa na mambo mawili; moja ni kutathmini utendaji wa jumuiya hiyo kwa miaka mitano iliyopita na ijayo na pili; uchaguzi wa viongozi wakiwamo mwenyekiti, makamu wake na wajumbe.

Uchaguzi ndani CCM na jumuiya zake ni sehemu ya utekelezaji wa kalenda ya chama hicho kwa mwaka 2017. Umefanyika kuanzia ngazi ya tawi hadi Taifa.

Alichokisema Mpinzani wa Mwenyekiti mpya UVCCM



Baada ya uchaguzi wa Umoja wa Vijana CCM ( UVCCM) kumalizika Dodoma, aliyekuwa mpinzani wa karibu wa mshindi wa UVCCM Thobias Mwesiga Richard, amezungumza baada ya kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Mwesigwa amesema anashukuru  Halmashauri ya Kamati Kuu na chama chake cha CCM, kwa kumpa nafasi ya kugombea Uenyekiti wa UVCCM, kati ya vijana 113 waliochukua fomu lakini pia kupata uteuzi kati ya vijana saba waliopitishwa na Halmashauri Kuu kugombea nafasi hiyo.

"Nimempigia simu Mwenyekiti aliyeshinda kumpongeza kwa kupata ushindi lakini pia kumuahidi kwamba nitampa ushirikiano wangu kwenye majukumu yake mbalimbali, pamoja na pongezi hizo yapo matendo ambayo hayakuridhisha katika uchaguzi wetu ikiwemo vitendo vya rushwa vilivyojitokeza kwa baadhi ya wagombea", amesema  Mwesigwa.

Mgombea huyo pia amesema vitendo vya rushwa katika chama chao sio jambo jema kwani linashusha heshima ya chama na linakipunguzia nguvu chama, lakini anamshukuru mheshimiwa Rais kwa kukemea vikali vitendo hivyo vya rushwa  na kuvipongeza vyombo vya dola kwa kuwakamata wale wote walioonekana wakijihusisha.

Katika uchaguzi huo wa UVCCM, Kheri James aliibuka mshindi kwa kupata kura 319 wakati Tobias Mwesiga aliibuka mshindi wa pili kwa kupata kura 127, Simon Kipala alipata kura  67, Kamana Juma alipata kura 27, Juma Mwaipaja naye alipata kura19, na Seif Mtoro aliambulia kura 16,  huku Mganwa Nzota akipata kura 1.

Rais Kenyatta ampa masharti haya Odinga


SIKU chache baada ya Baraza la Magavana nchini Kenya kuunda Kamati ya Watu 10, kuongoza mazungumzo ya usuluhishi ili kumaliza mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo, Rais Uhuru Kenyatta amesema yupo tayari kukutana na kuzungumza na Raila Odinga, lakini si kwa mambo ya siasa.

Kenyatta amesema mwishoni mwa wiki kuwa, muda wa siasa umekwisha, na kwamba, Wakenya wanasubiri maendeleo na si mazungumzo yasiyokwisha ya mambo ya siasa. Alitoa msimamo huo katika Shule ya Msingi Kinyona Kaunti ya Muranga wakati wa mazishi ya Susan Chege, ambaye ni mama mzazi wa mwakilishi wa wanawake Muranga, Sabina Chege.

Amesema, yupo tayari kuzungumza kuhusu namna ya kuwaendeleza Wakenya na si vinginevyo, hivyo wapinzani wasubiri awamu nyingine ya siasa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2022 watakapochuana na mgombea urais mtarajiwa wa chama cha Jubilee, Naibu Rais wa sasa, William Ruto.

Odinga, Kiongozi wa Muungano wa Vyama vya Upinzani (NASA), anadai hamtambui Uhuru Kenyatta kuwa ni Rais halali. NASA inaundwa na vyama vya The Orange Democratic Movement (ODM), Wiper Democratic Movement-Kenya (WDM-K), Amani National Congress (ANC) na Forum For the Restoration of Democracy- Kenya (FORD-K).

Viongozi wakuu wa muungano huo ni Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi, na Moses Wetangula. Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), ilimtangaza Kenyatta kuwa ni mshindi wa uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26, aliapishwa Novemba 28 kwenye uwanja wa Kasarani jijini Nairobi.

NASA walitangaza kuwa Odinga angeapishwa siku hiyohiyo kuwa Rais wa watu lakini mpango huo ulisitishwa. Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, akatangaza angeapishwa leo, lakini pia kambi yake imetangaza kuahirisha hadi hapo itakapotangazwa tena.

Wajumbe wa kamati ya usuluhishi ni Gavana wa Turkana, Josephat Nanok ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Magavana hao, Gavana wa Siaya Cornell Rasanga, Gavana wa Makueni Kivutha Kibwana na Gavana wa Kakamega, Wycliffe Oparanya.

Wajumbe wengine ni Gavana wa Bomet Joyce Laboso, Gavana wa Uasin Gishu, Jackson Mandago, Gavana wa Kitui, Charity Ngilu, Gavana wa Nyandarua, Francis Kimemia, Gavana wa Meru, Kiraitu Murungi na Gavana wa Kwale, Salim Mvurya.

Kwenye mkutano wao jijini Nairobi, magavana hao walisema kamati hiyo itafanya kazi ya kuzipatanisha pande zinazopingana na ‘kuiponya’ nchi kutokana na mgawanyiko uliojitokeza wakati wa uchaguzi.

Kati ya Agosti na Oktoba mwaka huu, Kenya imefanya uchaguzi wa Rais mara mbili. Kwanza, Wakenya walipiga kura Agosti 8, mwaka huu na IEBC ilimtangaza Kenyatta mshindi, NASA wakapinga mahakamani, na Septemba Mosi Mahakama ya Juu zaidi ikabatilisha matokeo hayo na kuamuru uchaguzi mwingine ufanyike ndani ya siku 60.

Wakenya walipiga kura tena Oktoba 26, IEBC ikamtangaza Kenyatta mshindi. Odinga alitangaza kujitoa kwenye uchaguzi huo ingawa jina lake lilikuwa miongoni mwa wagombea wanane.

Magavana wanasema umefika wakati kwa viongozi wenye mapenzi mema kutekeleza kwa vitendo azma ya kupunguza joto la kisiasa ili nchi iwe na umoja. “Tunaamini kwamba kuna haja kwa sisi magavana kujitolea kuwa nyenzo ya amani nchini kwa kuzingatia hali ya kisiasa ilivyo sasa.

Kwa nafasi yetu sisi ni viongozi na kwa hiyo tunatoa mwito kwa viongozi wote kuungana na kutafuta njia ya kupooza joto la siasa,” alisema Gavana Nanok. Magavana waliwataka viongozi kuacha ajenda zisizo na tija, na badala yake wazingatie maendeleo ya taifa hilo.

Muda mfupi baada ya kupiga kura kwenye kituo kilichopo katika Shule ya Msingi Mutomo, Jimbo la Gatundu Kusini, Kaunti ya Kiambu Oktoba 26 mwaka huu, Kenyatta alisema, baada ya uchaguzi anaweza kuzungumza na Odinga ili kuondoa mgawanyiko nchini humo.

Mwanasiasa huyo aliyegombea urais kupitia chama cha Jubilee alikiri kuwa, Kenya imegawanyika kwa misingi ya ukabila. “Kama kiongozi unayewajibika lazima umtafute na hilo ndiyo lengo langu,” alisema Kenyatta.

“Kama nchi lazima tupambane na ukabila kwa kuwa hatuwezi kufanikiwa kwenye malengo yetu kama tunaendelea na ukabila,” alisema Kenyatta. Wakati wa kampeni, Kenyatta alisema hakuwa tayari kujadiliana na Odinga na pia alikataa kusuluhishwa na mtu kutoka nje ya nchi hiyo kwa maelezo kuwa nchi hiyo haina mgogoro wa kisiasa.

Siku hiyo hiyo ya uchaguzi Spika wa Bunge la Kenya, Justin Muturi alisema, mamlaka hiyo ipo tayari kusimamia mazungumzo kuwasuluhisha Kenyatta na Odinga. Muturi alimuonya Odinga afanye mambo yake kwa kuzingatia sheria na kwamba, Serikali haitaona vema kujadiliana na NASA ambayo inabadili mwelekeo wake na kuwa kitu kinachoendeshwa kinyume cha sheria.

Alisema, kama NASA wanaamua kuwa wapiganaji wa msituni serikali itapambana nao. Odinga alisema, anaweza kujadiliana na Kenyatta kama majadiliano hayo yatakuwa kwa ajili ya kufanyika kwa uchaguzi mwingine, unaoaminika ndani ya siku 90 (tangu Oktoba 26 mwaka huu).

Alisema wakati akihojiwa na kituo cha television cha CNN cha Marekani kuwa, hata kama Kenyatta akitangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika Oktoba 26, haitakuwa rahisi kwake kuingoza nchi hiyo.

Alisema, wataipinga Serikali kwa amani, na kwamba, kinaanzishwa kikundi kingine ndani ya Nasa kiitwacho National Resistance Movement. Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo, wataipinga serikali kwa amani, si kwa maandamano. Odinga amekataa ushauri wa Wamarekani kumwelekeza cha kufanya.


Watoto 2,400 waliokosa Shule wamepata fursa kujifunza kwa kutumia Tableti


Watoto takribani 2,400 waliokosa shule wamepata fursa ya kujifunza wenyewe kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayotumia Tableti, ikiwa ni mradi wa majaribio wa miezi 15 ambao umezinduliwa mkoani Tanga.

Mradi huo umezinduliwa katika kijiji cha Zenith ya Kati, wilayani Muheza mkoani Tanga ukiwa ni sehemu ya mradi mkubwa wa miaka mitano wa majaribio duniani chini ya Global Learning Xprize wenye lengo la kutatua matatizo ya kujifunza.

Mpango huo utagusa watoto 2,400 wa miaka kuanzia 9 hadi 11 kutoka katika vijiji 167 vya wilaya za Handeni, Korogwe, Lushoto, Muheza, Mkinga na Pangani. Timu ya wabunifu itahakikisha inawawezesha watoto waliokosa elimu ya darasani kujifunza stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa kutumia Tableti.
Mradi huo hapa nchini unaendeshwa kwa pamoja na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na XPrize ambao wametoa tableti husika.

Mwakilishi wa UNESCO anayesimamia mradi huo Faith Shayo amesema mradi huo umewezekana kuwepo kutokana na makubaliano kati ya serikali ya Tanzania kupitia Wizara yake ya elimu na TAMISEMI na mashirika husika.

Audio | Beka Flavour – Najima | Mp3 Download

Audio | Beka Flavour – Najima | Mp3 Download

Audio | Beka Flavour – Najima | Mp3 Download

DOWNLOAD

"Dada yangu hajataka niolewe sijui ananiona Bikra bado?" - SHILOLE

"Dada yangu hajataka niolewe sijui ananiona Bikra bado?" - SHILOLE

MAGAZETI YA LEO 12/12/2017