Tuesday, 12 December 2017

Alichoongea Thobias Mwisiga baada ya kuukosa Uwenyekiti UVCCM

Alichoongea Thobias Mwisiga baada ya kuukosa Uwenyekiti UVCCM


Kauli ya Waziri Mwijage juu ya wanaohama vyama vyao


MAGAZETI LIVE: Siri nzito Babu Seya, Aliyesamehewa na Magufuli, alifutiwa kifo na Nyerere


Audio | Tunda Man – Toto | Mp3 Download

Audio | Tunda Man – Toto | Mp3 Download
Audio | Tunda Man – Toto | Mp3 Download

Shamsa Ford ampa somo Shilole kuhusu ndoa


 STAA wa Filamu nchini, Shamsa Ford amefungukia uamuzi wa msanii mwenzake wa Muziki, Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole kwa kuamua kufunga ndoa tena ya Kidini na mpenzi wake, Uchebe ndoa iliyoshuhudiwa hivi karibuni na kutikisa kwenye mitandao na vyombo vya habari huku ikiwaacha midomo wazi kwa wale walidhani kuwa angerudiana na mpenzi wake wa zamani, Nuh Mziwanda.

Shamsa ambaye pia alifunga ndoa mwaka huu na mpenzi wake, Chidi Mapenzi ametumia ukurasa wake wa Instagram kumsihi Shilole atulie, aweke umaarufu pembeni, aitunze ndoa yake na hatimaye atafaidi matunda ya ndoa iliyo bora.

Shamsa ameandika;
“Hongera sana mamy. Umefanya maamuzi sahihi ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.Cha muhimu uwe mke bora wa Kitanzania kwa mumeo na ustar uweke pembeni.

“Mumuweke Mungu mbele, uvumilivu na kuheshimiana inshaallah mtazikana.Karibu kwenye Chama mama….Sasa nyie mnao subili matajiri wawaoe wakati hao matajiri wana wake zao wameanza nao moja mtasubili sana mpaka uso uote sugu.Uzuri na Ustar una mwisho wake. Iitafika muda hata inzi hakusogelei……HONGERA MAMA @shilolekiuno_badgirlshishi,” ameadika Shamsa.






Zanzibar: Bei mpya ya mafuta kwa mwezi wa Disemba kuanzia Kesho



MAMLAKA ya udhibiti wa huduma za nishati na maji Zanzibar (ZURA) imetoa taarifa juu ya bei mpya ya mafuta itakayoanza kutumika rasmi kuanzia kesho Jumanne tarehe 12-12-2017. Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake Maisara, Kaimu Mkurugenzi masuala ya wateja, Mussa Ramadhani Haji  alisema kuwa bei hizo Zura imepanga kufuatia mambo yafuatayo;-

Wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta Duniani (Platts Quatations) katika mwezi wa Novemba 2017 , kwa lengo la kupata kianzio cha kufanyia mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi wa Disemba 2017.

Pia thamani ya shillingi ya  Tanzania , gharama za usafiri , Bima na’ Premium ‘hadi Zanzibar  . Kodi za serikali  na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja.

Alisema bei za rejereja ya mafuta ya Petroli kwa mwezi wa Disemba, 2017 imepanda kwa shillingi (100) kwa lita kutoka shilling 2,130 Mwezi wa Novemba , 2017 hadi shilling 2,230 kwa lita katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.5%.

Pia alisema bei ya rejereja ya mafuta ya Dizeli kwa Mwezi wa Disemba , 2017 imeshuka kwa shilling (90) kwa lita kutoka shilling 2,280 kwa lita katika mwezi Novemba hadi shilling 2,190 kwa lita katika mwezi wa Disemba, 2017 sawa na  asilimia 4%.

Aidha alisema bei ya reja reja ya mafuta ya Taa kwa mwezi wa Disemb 2017 imepanda kwa shilling (80)  kwa lita kutoka shillingi 1.539 kwa lita katika mwezi wa Novemba , 2017 hadi shilling 1,619 katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.9%

Vilevile bei ya reja reja ya mafuta ya Banka kwa mwezi waDisemba,  2017 imeshuka kwa shilling (90) kwa lita kutoka shillingi 2,122 kwa lita katika mwezi wa Novemba, 2017 hadi shilling 2,032 katika mwezi wa Disemba , 2017 sawa na ongezeko la asilimia 4.4%.

Handeni: Wauzaji wa nyama wagoma kufungua maduka ya kuuzia bidhaa hiyo.



Wauzaji wa nyama pamoja na wachinjaji wanaofanya shughuli zao kwenye machinjio yaliopo wilayani Handeni mkoani Tanga wameendesha mgomo wa kutokuchinja na kuuza nyama mpaka pale viongozi wa halmashauri watakaposikiliza kero zao na kuzitatua ikiwemo ya kulazimiswa kutumia gari maalum la kusambaza nyama hali ambayo wamesema kuwa hawakushirikiswa ipasavyo kwenye swala hilo.

Kamera ya ITV imefika machinjio ya wilaya na kukuta yakiwa meupe bila kuwepo dalili ya kupatikana huduma hiyo na ilifanikiwa kuongea na mwenyekiti wao na hapa anaelezea sababu.

Hata hivyo mkurugenzi wa halmashauri ya mji alifika machinjioni hapo na kukiri kuwa kweli ushirikishwaji haukufanyika huku wafanya biashara hao wakimkataa daktari wa machinchio hayo mbele ya mkurugenzi.

Rais wa Korea Kaskazini ampinga Trump kuhusu Jerusalem



Rais wa Korea-Kaskazini Kim Jong Un amesema kuwa uamuzi wa Trump kutangaza kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel hauna maana yeyote.

Mpango wa Marekani kuamisha ubalozi wake Tel Aviv na kuhamia Jerusalem ni jambo la kukemewa.

Kim Jong Un anapinga uamuzi wa Trump kuhusu jiji la Jerusalem.

Rais wa Korea-Kaskazini amesema kwa kejeli kuwa iwapo kuna taifa linaitwa Israel basi mji wake mkuu uwe Jerusalem.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Ufaransa cha AFP ni kwamba  msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Korea-Kaskazini amesema kuwa Marekani i natishia amani na utulivu  ulimwenguni .

Ujumbe wake ulimalizia kwa kusema kuwa  Korea-Kaskazini ipo bega kwa bega na wapalestina  na waarabu wanaopigania haki yao.

Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa miaka 3000 - Netanyahu



Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa wapalestina ni lazima wakubali kuwa Jurusalem ndio mji mkuu wa Israel ili amani iweze kupatikana.

Netanyahu alisema Jerusalem umekuwa mji mkuu wa Israel kwa miaka 3,000 na haujakuwa mji mku wa watu wengine.

Aliongea huku maandamano yakiendelea kwenye ulimwengu wa kiislamu kufuatia hatua ya Marekani kuutambua Jurusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Ghasia zilizuka karibu na ubalozi wa Marekani nchini Lebanon na kwingineno siku ya Jumapili.

Jerusalem kwenyewe, mpalestina mmoja alikamatwa kwa kumdunga kisu na kumjeruhiwa vibaya afisa wa usalama wa Israel karibu na kituo kimoja cha basi.

Akiongea mjini Paris baada ya mazungumzo na rais wa Ufaransa Emmauel Macron, Bw Netanyahu alisema kuwa jitihada za kuwanyima wayahudi mji wa wa Jerusalem ni kitu kibaya.

"Unaweza kusoma katika kitabu kizuri zaidi, kinaitwa Biblia, alisema. Unaweza kuyaskia katika historia ya jamii wa wayahudi kote duniani… Ni wapi tena kuna mji wa Israel, isipokuwa Jerusalem?



Kamanda alieiba matunda ya wapalestina asimamishwa kazi



Kamanda wa jeshi la Israel alieonekana  katika  operesheni ya kusambaratisha waandanaji el Halil Palestina akiiba matunda « aple » amesimamishwa kazi kwa muda.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya jeshi kuthibitisha tukio hilo.

Wauza  matunda  katika Ukingo wa Magharibi  walilazimika kuondoka katika vibanda vyoa wakikimbia ghasia ndipo kamanda huyo alionekana kuiba matunda.

Video  inayomuonesha kamanda huyo akiiba matunda imezagaa katika mitandao ya kijamii.

Simba yaachana na Mrundi


Baada ya Simba kuhusishwa na kutaka kumsajili Mrundi, Nahimana Shassir anayeichezea Rayon Sport, dili hilo limekufa rasmi baada ya Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma kusema hawatamsajili.

Djuma ambaye ni raia wa Burundi, alipendekeza kusajiliwa kwa mchezaji huyo, lakini baada ya kumuangalia zaidi, amejiridhisha kwamba hata akija hatakuwa na msaada wowote.

Djuma amesema: “Nilipendekeza asajiliwe lakini mpaka sasa tumesitisha dili hilo kwa sababu ameshuka kiwango, nimemuangalia kwenye michuano ya Chalenji nimeona hajaisaidia chochote timu yake, hivyo hatutamsajili tena.

“Hatuwezi kumsajili mchezaji wakati uwezo wake ni mdogo kuliko wale waliopo ndani ya kikosi chetu cha sasa.”


Hata Kama Mambo Yanakwenda Vibaya, Fanya Hivi



Ni rahisi sana kuwa na hasira, kukatishwa tamaa na hata msongo wa mawazo. Hiki ni kiu ambacho kila mtu anaweza akawa nacho kwenye maisha yake.

Nikiwa na maana kila mtu akikasirishwa, anaweza akakasirika sana au mtu akikatishwa tamaa anaweza akakata tamaa pia sana.

Lakini yote hiyo haiwezi kusaidia kitu. Busara na ukomavu wako wa kimaisha unakuja pale hasa unapokwenda kinyume na mambo hayo.

Ni kweli unaweza ukawa umekasirishwa na ukatamani upige mtu sana, sasa je, kwani ni lazima ifike mahali ukakakasirika kwa kiasi hicho?

Ni kweli unaweza ukawa umekatishwa tamaa, lakini kwa wewe haina haja kuendelea kufanya mambo ambayo yanakukatisha tamaa zaidi.

Unachotakiwa kufanya au kujifunza ni kuweza kugeuza mambo ya hovyo na yakawa bora zaidi hata kama imetokea hali ya kukasirishwa au kukatishwa tamaa.

Kufanya hali mbaya ambayo tayari naweza kusema umeshapewa na ikawa ni nzuri, huo ni ukomavu wa hali ya juu utakaokufanya uishi vizuri sana duniani.

Mtu amekuuzi sana na wewe huhitaji kuendelea kufoka au kuumia zaidi. Unatakiwa kutuliza akili yako na kufanya mambo ili yawe mazuri.

Kufanya mambo yawe mazuri hasa pale yanapokuwa yameharibika ni kitu ambacho unatakiwa ujifunze nacho sana karibu kila siku.

Kila siku na kila wakati endelea kuweka juhudi za kuwa mtu chanya, mpaka maisha yako yalete utofauti mkubwa na kwa wengine.

Ni watu wachache sana ambao wako tayari kubadilisha hali mbaya ya msongo wa mawazo walionayo, kukatishwa tamaa na kukasirishwa kuwa nzuri.

Wengi wakikasirishwa na wengine hukasirika na kukasirisha zaidi. Hivyo, unatakiwa usiwe miongoni mwao. Unatakiwa uwe mtu wa kubadilisha hali.

Kufanya hali yoyote iwe bora ni zoezi ambalo unaweza ukalifanya karibu kila siku kwenye maisha yako pale ambapo unakuwa unaona mambo hayajakwenda sawa.

Unatakiwa uelewe hili, pale mambo yako yanapokwenda hovyo, fanya mambo hayo yawe bora. Jitahidi kubadili hali hiyo kwa busara na ikawa bora.

Matunzo Ya Kuku Wanaotaga



Hapa tunaangalia majogoo na mitetea yenye umri wa kuanzia miezi minne na kuendelea.

Matunzo mengi wanayopewa ni sawa na ya kuku wanaokua (tafadhali rejea kwenye somo la matunzo ya kuku wanaokua).

Matunzo mengine ya ziada:-
1. Watenge majogoo na matetea kwa idadi inayofaa.

Kama unafuga huria, jogoo mmoja kwa mitetea 6.

Kama unafuga kwenye vyumba, jogoo mmoja kwa mitetea 4-5.

2. Wape chakula cha ‘layers’ chenye virutubisho vya kutosha.

3. Endelea kuchanja Newcastle kila baada ya wiki 10.

 4. Endelea kuwapa dawa ya minyoo kila baada ya wiki 10.

5. Walishe majani na mboga mboga kwa wingi, ili mayai watakayotaga yawe na kiini cha njano.

6. Kuwa makini sana na sehemu ya kifua na eneo la chini la mitetea, ambapo ndipo mayai yanapohifadhiwa kwa ndani. Kuku akigongwa au akijigonga eneo hilo,  yai linaweza kupasuka kwa ndani, na tetea huyo atanyong'onyea, na baada ya siku kadhaa atakufa.

7. Okota mayai mara nyingi iwezekanavyo, ili kuzuia kuku kula mayai au wasiyavunje au kuyawekea ufa.

8. Kuku wanapoanza kutaga nunua daftari ya kutunza kumbukumbu za mayai yanayotagwa kila siku. Hii itakusaidia kujua siku wanapopunguza kutaga, ili kutafuta chanzo, na kama ni ugonjwa, watibiwe haraka.

Kila la kheri katika ufugaji wako, na endelea kuwa pamoja nasi katika masomo mengine ya ufugaji wa kuku.