Tuesday, 28 November 2017

Matumizi ya Mkaa husababisha Uharibifu wa Misitu




Taarifa za wataalamu wa misitu zinaonyesha kuwa uharibifu wa misitu kutokana na matumizi ya mkaa ni hekta 372,000 kwa mwaka.

Kiwango hicho ni sawa na asilimia 1.1 ya eneo lote lenye miti na katika Jiji la Dar es Salaam pekee zaidi ya magunia 500,000 ya mkaa huingizwa kila mwezi.

Uvunaji na usafirishaji haramu na holela wa mazao ya misitu hususan mkaa kwa kutumia pikipiki na baiskeli ndani ya misitu ya hifadhi, mapori ya akiba na hata ndani ya hifadhi za Taifa unatajwa kuwa chanzo kikuu cha baa hili.

Inaelezwa kuwa pikipiki 20 zikisafirisha mkaa ni sawa na lori moja lililojaa mkaa. Aidha, njia hii ya usafirishaji inachangia ukwepaji wa makusanyo ya maduhuli ya Serikali.

Kufuatia changamoto mbalimbali za usafirishaji wa mazao ya misitu nchini Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) mwaka huu iliunda kikosi kazi kwa kushirikisha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) na Kikosi cha Usalama Barabarani  ili kutekeleza sheria na kanuni za usafirishaji wa mazao ya misitu.

Kikosi kazi hicho kinalenga kudhibiti usafirishaji wa mazao ya misitu kwa baiskeli na pikipiki katika barabara za mikoa ya Dar es Salaam, Iringa, Morogoro na Pwani.

Mkurugenzi wa mipango na matumizi endelevu ya misitu na nyuki nchini, Mohamed Kilongo anasema TFS imekuwa ikitoa elimu inayohusu usafirishaji wa mazao ya misitu hususan mkaa baada ya kubaini kuwa ndio kichocheo kikubwa cha uharibifu wa mazingira.

Anasema mazao ya misitu huvunwa kinyume na taratibu na kusafirishwa kwa kutumia pikipiki na baiskeli, jambo ambalo pia ni kinyume na sheria.

“Usafirishaji wa mazao ya misitu kwa baiskeli na pikipiki unakiuka Mwongozo wa Uvunaji Endelevu wa Mazao ya Misitu, 2015 unaoeleza kuwa vyombo vya usafiri vinavyoruhusiwa kusafirisha mazao ya misitu ni vile vyenye magurudumu manne,” anasema Kilongo.

Anasema mwongozo huo ulizingatia pia sheria nyingine za nchi zikiwemo Sheria za Usalama wa Barabarani na Sumatra, lakini pia kubana mianya ya wizi na ukwepaji mkono wa sheria za usimamizi wa maliasili nchini.

“Kwa upande wa Sumatra kupitia Kanuni ya Leseni za Usafirishaji ya Mwaka 2010, inatambua pikipiki kama chombo cha kusafirisha abiria na si vinginevyo na Sheria ya Usalama Barabarani Sura Namba 168 iliyorejewa mwaka 2002 inatambua pikipiki na baiskeli kama chombo cha usafirishaji kwa ajili ya abiria na si mizigo,” anasema mkurugenzi huyo.

Aidha, anasema kwa mujibu wa tathmini iliyofanyika Novemba mwaka jana hadi Januari mwaka huu, katika barabara kuu za Bagamoyo, Kisarawe, Morogoro na Kilwa zinazoingia jijini Dar es Salaam, jumla ya pikipiki 582 zimebainika kubeba mazao ya misitu kinyume cha sheria kila siku.

Hata hivyo, katika eneo la Visakazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kunaonekana kuwa na usafirishaji hatari zaidi wa mazao ya misitu kwa kutimia pikipiki.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wanaeleza kuwa, biashara ya mkaa imekithiri kwa sababu ndiyo njia pekee ya kuwapatia kipato na usafirishaji wa mazao ya misitu kutoka maeneo mbalimbali ni ajira inayowaingizia kipato.

“Tunalazimika kusafirisha kwa njia ya pikipiki na baiskeli kwa kuwa mtaji wetu mdogo na hivyo tunashindwa kumudu gharama za kukodi magari kwa shughuli hiyo,” anasema mfanyabiashara wa mkaa pembezoni mwa barabara aliyejitambulisha kwa jina la mama Khadija.

Anayataja maeneo maarufu ya uvunaji wa mazao ya misitu hususan mkaa kuwa ni pamoja na Lukwambe, Mkono wa Tembo, Ubena na Chamlugwa yote ya wilayani Chalinze.

Ukwepaji makusanyo ya Serikali

Kuhusu ukwepaji wa makusanyo ya maduhuli ya Serikali, Khadija anasema wanalipa ushuru wa Serikali ya kijiji pamoja na halmashauri, lakini hawamudu kulipa ushuru wa Wakala wa Huduma za Misitu kwa kuwa gharama zake ni kubwa.

Anasema wamekuwa wakilipa ushuru wa kijiji wa Sh500 kwa gunia moja kwenye vijiji wanavyovuna na wanapoufikisha pembezoni mwa barabara mteja anayenunua mkaa anawajibika kulipa ushuru wa halmashauri wa Sh1,800 kupitia wakala wa ushuru wa halmashauri.

Ofisa wa Wakala wa Ushuru wa halmashauri hiyo, Afrikanus Silvanus anakiri kuwa wafanyabiashara wa Visakazi hufanya biashara na kusafirisha mazao ya misitu kwa nyakati zote, mchana na usiku.

Anasema kuwa yeye binafsi hupokea ushuru wa halmashauri hadi nyakati za usiku, pale ambapo kuna uhitaji jambo ambalo ni kinyume na sheria.

DC alia usimamizi wa sheria

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ni miongoni mwa watu walioshuhudia usafirishaji wa mazao ya misitu kwa njia ya pikipiki anasikitika kuona sheria zipo na wanaozisimamia wapo, lakini hawatekelezi wajibu wao hali inayosababisha misitu kuendelea kuteketea.

“Inawezekanaje vyombo vinavyosafirisha mazao ya misitu kinyume na sheria, hususan baiskeli na pikipiki vinapita mbele ya askari wa usalama barabarani na hachukuliwi hatua? Inawezekanaje hawa wanapita na magunia yenye uzito zaidi ya unaostahili?” anahoji Mjema na kuongeza:

“Inawezekana vipi halmashauri inaukatia ushuru mzigo huo? Inawezekanaje anapita kwenye vizuizi vyenye watu wa usalama baada ya giza kuingia ili hali hairuhusiwi? Kila mtu na atimize wajibu wake misitu yetu itapona.”

Mei 26, 2016 Wizara ya Maliasili na Utalii na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) walisaini makubaliano kuimarisha ushirikiano katika usimamizi wa misitu kwa pamoja, malengo ambayo kila upande  ukitekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika makubalino hayo usimamizi endelevu wa  misitu    utaimarika  kwa faida ya Taifa.

RC Ndikilo atoa agizo

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo akifungua mkutano wa siku moja wa Kanda ya Mashariki kuhusu utekelezaji wa randama ya makubaliano ulioandaliwa na TFS na kufanyika katika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (Tafori) mjini Morogoro wiki iliyopita alisema kwa kuzingatia umuhimu wa hifadhi za misitu, ni vyema kila mwananchi akazingatia maagizo ya Serikali.

Ndikilo anawataka wananchi kufuata sheria za nchi zinazohusiana na uhifadhi wa maliasili na kuachana na tabia ya uharibifu wa miti kwa kuwa huko ni kuhatarisha vizazi vilivyopo na vijavyo.

“Naagiza, wale wote wanaofanya biashara ya mkaa kuzingatia sheria na taratibu ikiwamo uzito wa gunia la mkaa uliowekwa (kilo 50). Ni marufuku mazao ya misitu kusafirishwa na vyombo visivyoruhusiwa kisheria, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakaesafirisha, kununua au kuuza mazao yaliyovunwa kinyume na sheria,”anasema.

Anaongeza kuwa zaidi ya asilimia 70 ya mkaa unaozalishwa mikoani huingia Dar es Salaam kwa njia zisizo halali kama vile magari yaliyofunikwa, baiskeli na pikipiki, na endapo hatua madhubuti za kudhibiti uharibifu huo hazitachuliwa haraka nchi itakuwa jangwa siku za karibuni.

Nafasi za kazi leo November 28

IGP Sirro amefanya Ziara Bandarini Kukagua magari ya Polisi



MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro, amefanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam, ili kufanya ukaguzi wa magari 31 ya Jeshi hilo ambayo Rais John Magufuli, alielekeza kukabidhiwa kwa Jeshi hilo ili kurahisisha utendaji wao wa kazi.



Akiwa Bandarini hapo IGP Sirro amekutana na kufanya mazungumzo na askari wa Jeshi hilo Kikosi cha Bandari ambapo amewataka kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ipasavyo pamoja na kutenda haki ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wateja.

Hata hivyo IGP amewataka Polisi wasaidizi wanaofanya kazi bandarini hapo kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuendelea kudhibiti vitendo vya kihalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.


Haya ndio yatakayojiri kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta



Leo Novemba 28, Rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta anaapishwa ili kuweza kuiongoza nchi hiyo kwa mujibu wa sheria za Kenya, baada ya ushindi alioupata kufuatia uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26, 2017.

Uhuru Kenyatta ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa nchi hiyo David Maraga ambayendiye yule aliyetengua matokeo ya ushindi wake baada ya uchaguzi wa Agosti 8 kwa amri ya mahakama, huku akiwa ameshikilia biblia ambayo ilitumiwa na marehemu baba yake Mzee Jomo Kenyatta alipoapishwa kwa mara ya kwanza kuiongoza nchi hiyo 1964 baada ya kupata uhuru wao kutoka kwa wakoloni, Desemba 12, 1963, na meza ambayo itatumika kukaa wakati wa kutia saini, ni ile iliyotumika na rais wa tatu wa nchi hiyo Mwai Kibaki wakati wa kuapishwa kwake.

Kutokana na Uhuru Kenyatta tayari alikuwa madarakani kama Rais kwa wamu yake ya kwanza, hatakabidhiwa jamvia ambao ni kama alama ya kuwa na kamanda mkuu wa nchi na Majeshi yote ya nchi hiyo.

Pia sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa na mataifa mengine ya Afrika, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. JOhn Pombe Magufuli, Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Rwanda Paul Kagame na wengineo.

Sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa Taifa wa Moi Kasarani na zinataraijwa kuhudhuriwa na maelfu ya watu, huku upande wa upinzani wakiwa wamegomea kuhudhuria sherehe hizo, wakidai hawamtambui Uhuru Kenyatta kama rais wa nchi hiyo.

Yanga yasajili straika huyu



YOHANA MKOMOLWA.

SIKU moja baada ya kumsainisha mkataba wa miaka miwili beki wa kati raia wa Kongo, Fiston Kayembe, Yanga jana ilimnasa mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Vijana 'Serengeti Boys' Yohana Mkomolwa.

Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, imemsainisha nyota huyo mkataba wa miaka miwili na ataanza kuitumikia timu hiyo pale ligi itakapoendelea baada ya kupisha michuano ya Kombe la Chalenji.

Mkomolwa ambaye alifanya vizuri na Serengeti Boys kwenye michuano ya Afrika iliyofanyika, Gabon mwaka huu,anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Yanga kwenye dirisha hili dogo.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, akizungumza na gazeti hili jana, alithibitisha 'kinda' huyo kusajiliwa na Yanga.'Ni kweli Mkomolwa amejiunga na sisi..., na hii ni katika kuboresha kikosi chetu," alisema Saleh.

Katika hatua nyingine, Saleh, aliema kuwa kocha wa timu hiyo, George Lwandamina, ametoa mapumziko ya wiki moja kwa wachezji wake.

Alisema wachezaji wa timu hiyo wataendelea na mazoezi Jumatatu ijayo kwenye Uwanja wa Uhuru.

"Unajua baada ya ligi kusimama, kocha ameamua kuwapa wachezaji ambao hawamo kwenye vikosi vya timu za Taifa mapumziko ya wiki moja, tutaanza mazoezi Jumatatu ijayo,"alisema Saleh.

Yanga inawachezaji kwenye vikosi vya timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' na ile ya zanzibar 'Zanzibar Heroes' ambazo zote zitashiriki michuano ya Chalenji inayoanza Desemba 5, mwaka huu nchini Kenya.

Wabunge wa CUF wamvaa Ndugai

  Dar es Salaam. Wabunge wanane wa viti maalumu CUF waliovuliwa ubunge wamemwandika barua Katibu wa Bunge amjulishe Spika Job Ndugai kuhusu uamuzi wa Mahakama Kuu ili achukue hatua stahiki ikiwamo kuwafahamisha utaratibu utakaotumika kuwarejesha kwenye nafasi zao.

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam katika uamuzi iliyoutoa Novemba 10, imeizuia CUF kujadili na kuwafukuza uanachama wabunge hao na madiwani wawili wa viti maalumu.

Wakati Mahakama ikitoa uamuzi huo, tayari chama hicho kikiwa kinachoongozwa na mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kilishawavua uanachama hivyo kupoteza ubunge wao.



Wabunge hao wanaomuunga mkono katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ni Miza Bakari Haji, Saverina Mwijage, Salma Mwasa, Raisa Mussa, Riziki Mngwali, Hadija Salum Al-Qassmy, Saumu Sakala na Halima Mohamed.

Hatima yao

Akizungumza jana kwa niaba ya wenzake, Mngwali alisema waliandika barua Novemba 20 na tayari imepokewa katika ofisi ya Bunge.

“Kisheria sisi bado ni wanachama halali wa CUF tuna sifa za kuendelea kuwa wabunge kutokana na uamuzi wa Mahakama Kuu, ndiyo maana tumemwandikia Spika ili kujua utaratibu utakaotumika kuturejesha bungeni kwa spidi ileile iliyotumika kutuengua katika chombo hicho Julai 25,” alisema.

Mngwali aliyeambatana na Mwasa na Mwijage, alisema wameona ni vyema kuwajulisha wanachama wa CUF na Watanzania hatua walizochukua baada ya uamuzi wa Mahakama.

Alisema wana imani Spika Ndugai atatenda haki katika jambo hilo. Julai 25, Spika Ndugai aliridhia barua ya Profesa Lipumba ya kuwavua uanachama wabunge hao.

Baadaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ilitangaza wabunge wapya baada ya kupata taarifa ya Bunge.

Wabunge walioteuliwa kuchukua nafasi zao ni Sonia Magogo, Kiza Mayeye, Shamsia Mtamba, Zainab Mndolwa, Hindu Mwenda, Alfredina Kahigi, Nuru Bafadhili na Rukia Ahmed Kassim.

Kabla ya kuapishwa, Hindu alifariki dunia Septemba mosi na NEC ilimteua Rehema Migira kuchukua nafasi yake.

Kaimu naibu mkurugenzi wa habari, mawasiliano kwa umma wa CUF, Mbarala Maharagande alisema uamuzi wa Mahakama umeshatoka hivyo wanasubiri busara za Ndugai za kuwarejesha wabunge hao.

Hata hivyo, Ndugai alipotafutwa kuzungumzia suala hilo hakuwa tayari kujibu lolote zaidi ya kumweleza: “ Mwananchi mmeanza.”   


Enock Bella Afunguka Aslay Kuiba Daftari la Nyimbo za Yamoto Band

Enock Bella Afunguka Aslay Kuiba Daftari la Nyimbo za Yamoto Band




Audio | Ainea – Nikuite Nani.| Mp3 Download

Audio | Ainea – Nikuite Nani.| Mp3 Download

Audio | Ainea – Nikuite Nani.| Mp3 Download



                                                 DOWNLOAD HERE

Video | K.O Ft Runtown – Call Me’ Enjoy | Mp4 Download

Video | K.O Ft Runtown – Call Me’ Enjoy | Mp4 Download

K.O Ft Runtown - Call Me’ Enjoy

Video | K.O Ft Runtown – Call Me’ Enjoy | Mp4 Download



                                                                DOWNLOAD HERE

Video(Lyrics) | Diamond Platnumz Ft Morgan Heritage – Hallelujah | Mp4 Download

Video(Lyrics) | Diamond Platnumz Ft Morgan Heritage – Hallelujah | Mp4 Download

Diamond Platnumz Ft Morgan Heritage – Hallelujah

Video(Lyrics) | Diamond Platnumz Ft Morgan Heritage – Hallelujah | Mp4 Download



                                                 DOWNLOAD HERE

Video | Fifi Cooper – Take Me Back | Mp4 Download

Video | Fifi Cooper – Take Me Back | Mp4 Download

Fifi Cooper – Take Me Back

Video | Fifi Cooper – Take Me Back | Mp4 Download


                           DOWNLOAD HERE

Audio | Diamond Platnumz – Niache | Mp3 Download

Audio | Diamond Platnumz – Niache | Mp3 Download

Diamond Platnumz - Niache

Audio | Diamond Platnumz – Niache | Mp3 Download



                                                            DOWNLOAD HERE

Audio | Diamond Platnumz – Sikomi | Mp3 Download

Audio | Diamond Platnumz – Sikomi | Mp3 Download

Diamond Platnumz - Sikomi

Audio | Diamond Platnumz – Sikomi | Mp3 Download


                                                   DOWNLOAD HERE