Sunday, 26 November 2017

Yanga yamsajili kimya kimya straika Mkomola



STRAIKA wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 'Ngorongoro Heroes', Yohana Mkomola, amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuichezea Yanga, kuanzia mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Mkomola ambaye ni tegemeo ndani ya Ngorongoro Heroes, alijiunga na Etoile Du Sahel  mwezi Agosti, klabu iliyomchukua kwa makubaliano maalumu ya kumlea kwa sababu alikuwa na miaka chini ya 18 na baada ya hapo, wangemsajili jumla.

Hata hivyo, licha ya tetesi hizo kujulikana, uongozi wa Yanga na Mkomola mwenyewe, wamegoma kuthibitisha na wakidai kama suala hilo lipo, litajulikana tu.

Huo utakuwa usajili wa pili wa Yanga, awali walimsajili Mcongo Fiston 'Festo' Kayembe Kanku kwa mkataba wa miaka mwili.

Hizi ndio sababu za Dk Shika kualikwa Kahama




Kahama. Mkurugenzi wa Chuo cha Tiba ya Binadamu Kahama, Yona Bakungile amesema alimualika Dk Louis Shika kwenye mahafali ya kwanza ya wanachuo wake kwa sababu ya ahadi zake za shaka za ununuzi wa nyumba, alizoshinda kwenye mnada zitasaidia kutangaza chuo hicho.

Novemba 9, Kampuni ya Udalali ya Yono kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), iliendesha mnada wa nyumba mbili za Lugumi zilizopo Mbweni JKT na moja ya Upanga jijini Dar es Salaam ambazo zote Dk Shika alifikia bei ya kuzinunua kwa Sh3.2 bilioni lakini alishindwa kulipa asilimia 25 ya mwanzo.

Akizungumza na Mwananchi mjini Kahama juzi, Bakungile alisema aliona atumie nafasi hiyo kumwita Dk Shika Kahama na hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kwenda wilayani humo.

Baada ya kuulizwa na Mwananchi kwanini alitumia gharama kubwa kumsafirisha kwa ndege Dk Shika huku akijua wazi kwamba Dar es Salaam alishinda mnada na hakuwa na fedha za kulipa, Bakungile alidai kushindwa kulipa kwa fedha za mnada ndilo jambo lililompa umaarufu.

“Najua wazi Dk Shika alishindwa kulipa Sh900 milioni kwenye mnada wa nyumba za Lugumi hivyo katika chuo changu ameahidi kutoa kila mwaka Dola 1 milioni za Marekani (sawa na Sh2.2 bilioni) ambazo akishindwa kuzilipa ataendelea kutangazwa kwamba ameshindwa kulipa hiyo itakuwa fursa ya chuo changu kuendelea kutangazwa,” alisema Bakungile.

Alhamisi iliyopita Dk Shika aliingia mjini Kahama akiwa mgeni mwalikwa wa chuo hicho na baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza alitoa ahadi hiyo ya fedha akisema ataziwasilisha baada ya miamala ya kuhamisha fedha zake kutoka Urusi itakapokamilika.

Hata hivyo, baadhi ya watu walisema ‘bilionea’ huyo hapaswi kupewa heshima hiyo na badala yake anapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa kuvuruga mnada.

Kiongozi wa ACT Wazalendo atiwa mbaroni



Misungwi. Wakati upigaji kura katika Kata ya Kijima wilayani Misungwi likiendelea vema, mratibu wa shughuli za kampeni za ACT Wazalendo katika kata hiyo, John Mbozu anashikiliwa polisi kwa tuhuma za kupiga picha eneo la kituo cha kupiga kura bila kibali.

Mbozu ambaye pia ni Katibu wa Mambo ya Nje wa ACT Wazalendo amepelekwa kituo cha Polisi cha Misasi kwa mahojiano zaidi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Eliud Mwaiteleke amesema hadi kufikia saa 4:00 asubuhi leo Jumapili Novemba 26, hakuna tukio lolote lililoripotiwa kukwamisha upigaji kura zaidi ya hilo la mtu mmoja kukamatwa akipiga picha kituo cha kupiga kura bila kibali maalum kutoka ofisini kwake.

Wakazi wa Kata ya Misasi wanapiga kura leo Jumapili kumchagua diwani kutokana na kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Kwabi Pandoji (CCM).

Mwananchi:

Mgombea wa Chadema afunguka kilichosababisha akamatwe



Morogoro. Mgombea udiwani kwa tiketi ya Chadema katika Kata ya Sofi wilayani Malinyi mkoani Morogoro, Riko Venance ambaye aliwekwa chini ya ulinzi kwa takribani saa moja amesema polisi walifanya hivyo baada ya kuhoji sababu za mwananchi mmoja kuzuiliwa kupiga kura.

Alizungumza na Mwananchi leo Jumapili baada ya kuachiwa amesema alipofika katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Mission alipata malalamiko toka kwa mmoja wa wapiga kura aliyejulikana kwa jina moja la Akwilina kwamba amezuiliwa kupiga kura.

“Nilikuwa nahoji kwa nini Akwilina azuiliwe kupiga kura na ndipo nilipoambiwa nasababisha vurugu na kuwekwa chini ya ulinzi," amesema Venance.

Amesema mpiga kura huyo alipoulizwa jina alisema anaitwa Akwilino wakati kwenye kadi imeandikwa Akwilina na hapo ndipo utata ulipoanzia, hata hivyo baadaye aliruhusiwa kupiga kura.

Mgombea huyo ambaye anaendelea kutembelea vituo tayari ameshatembelea vituo 10 kati ya vituo 21 vya kupigia kura vilivyopo katika kata hiyo.

Rais Magufuli aibua mapya bandarini


Magari 50 ambayo mwenyewe hajajulikana yamekamatwa bandarini na Rais Magufuli alipofanya ziara bandarini hapo, akitokea kwenye meli ya madaktari bingwa kutoka China.

Magari hayo amabyo yameelezwa kuletwa mwezi wa 6 mwaka 2015 yakiwa na magari ya jeshi la polisi, mpaka leo hayajatolewa bandarini hapo, yameelezwa kuwa na siri kuba ambayo Rais mwenyewe anaifahamu, huku mizgo wa lawama ukienda kwa Jeshi la Polisi.

“Inakuwaje rais nipate taarifa za magari kufichwa lakini Waziri, TRA, TPA msijuie? Mnatakiwa muwe na informer wenu sio hadi mimi nije ndo mnaaza kusema sijui. Nafahamu hata mletaji namfahamu, nataka mniletee ninyi ili nione kama tunaenda uelekeo mmoja au hatuendi", amesema Rais Magufli.

Raius Magufuli ameendelea kwa kusema ..."Kule Polisi kuna mambo ya hovyo. Polisi Mnadai hizi gari ni zenu, kwanini hamzifuatilii tangu 2015? Kuna magari yamekaa miaka 10 lakini sheria inasema gari likikaa zaidi ya siku 21 yapigwe Mnada, kwanini hampigi mnada? IGP kwenye Majambazi upo safi lakini huku kwenye Ufisadi bado sana. Kama mtu anakunanihii mtwange. Nilikuchagua ulikua such good guy lakini unaniangusha. Polisi kuna Uchafu mwingi sana".

Kufuatia tukio hilo Rais Magufuli ametoa siku saba kwa TAKUKURU, Polisi na Wizara ya Uchukuzi kumpatia taarifa kamili juu ya magari hayio, ambayo mpaka sasa mmiliki wake hajajulikana.

Waziri Mhagama aiagiza Halmashauri ya Bahi kukamilisha Ujenzi wa Soko la Kigwe


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kuhakikisha inamaliza ujenzi wa soko la Kigwe kwa kuhakikisha wanajenga vyoo na vibanda vidogo vitakavyo saidia soko hilo lililojengwa na Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).

Ameyasema hayo alipofanya ziara yake Wilayani Bahi Novemba 21, 2017 kwa lengo la kujionea namna uboreshaji wa soko hilo ambalo tayari limekamilika kwa asilimia 90 na kukabiliwa na changamoto za vibanda na vyoo vya kudumu.

“Ninaiagiza Halmashauri hii kuhakikisha inaleta timu ya wataalamu kupima viwanja na kuvigawa kwa wananchi pamoja na kumalizia ujenzi wa Vyoo vya soko ili lianzae utekelezaji wake haraka na kuhakikisha umeme unafungwa ndani ya soko hili”.

Kwa upande wake Mbunge wa Bahi Mhe. Omary Badwel alieleza ujenzi wa soko ni jambo ja muhimu linalogusa wanakigwe wote kwani tangu enzi za mkoloni kumekuwa na changamoto ya soko na kuwataka wananchi kulitunza na kuhakikisha linakuwa msaada kwao wote.

“Soko hili toka utawala wa mkoloni kulikuwa na soko bovu hivyo hatua ya kulikamilisha litavutia wengi na kukuza uchumi wa wana Kigwe wote.”Alisisistiza Badwel

Alichokifanya Kassim Mganga kwa Vanessa Mdee jukwaani

Alichokifanya Kassim Mganga kwa Vanessa Mdee jukwaani



FiestaDar2017: AliKiba na Ommy Dimpoz walivyowasha moto Fiesta

FiestaDar2017: AliKiba na Ommy Dimpoz walivyowasha moto Fiesta



FiestaDar2017: Aslay awashika pabaya mashabiki wake



FiestaDar2017: Aslay awashika pabaya mashabiki wake


Audio | Single Sally – Asuu | Mp3 Download

Audio | Single Sally – Asuu | Mp3 Download

Single Sally - Asuu

Audio | Single Sally – Asuu | Mp3 Download



                 DOWNLOAD HERE

Audio | Crazy Ninja – Komaa Na Mziki | Mp3 Download

Audio | Crazy Ninja – Komaa Na Mziki | Mp3 Download


Crazy Ninja - Komaa Na Mziki

Audio | Crazy Ninja – Komaa Na Mziki | Mp3 Download







                                                DOWNLOAD HERE

Video | Stino Ft Beka Flavour – Shokamoo Pesa | Mp4 Download

Video | Stino Ft Beka Flavour – Shokamoo Pesa | Mp4 Download

Stino Ft Beka Flavour - Shokamoo

Video | Stino Ft Beka Flavour – Shokamoo Pesa | Mp4 Download


                                                  DOWNLOAD

Singeli Audio | Mc Sudy Ft S Kide – Usitoe Mimba | Mp3 Download

Singeli Audio | Mc Sudy Ft S Kide – Usitoe Mimba | Mp3 Download

Mc Sudy Ft S Kide – Usitoe Mimba

Singeli | Mc Sudy Ft S Kide – Usitoe Mimba | Mp3 Download



                                                       DOWNLOAD HERE