Dodoma. Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limepitisha sera ya haki miliki za kitaaluma.Imeelezwa sera hiyo inalenga kuwabana wezi wa kazi za kitaaluma, kuboresha utafiti na uvumbuzi kwa kutoa uhakika wa haki za watafiti.Akizungumza katika mahafali ya nane ya chuo hicho leo Jumatano Novemba 22,2017 mwenyekiti wa baraza hilo, Gaudentia Kabaka amesema sera hiyo itasaidia na kuboresha utafiti na uvumbuzi kwa kutoa haki za watafiti, wanafunzi na wahisaniwengine katika shughuli zinazohusu chuohicho.“Sera hii inalenga kuweka bayana masuala ya ugawanaji wa haki miliki za kitaaluma na kutambua mchango wa watafiti, wanafunzi,wahisani, wadau na chuo utokanao na mauzo ya haki miliki za kazi za uvumbuzi,” amesema.Kabaka amesema baraza pia limepitisha mpango wa kukipandisha hadhi kituo cha afya cha chuo hicho kuwa hospitali. Alisema utaratibu umeanza kuhakikisha azma hiyo inafikiwa.“Tunawakaribisha wananchi waweze kupatiwa huduma katika kituo chetu cha afya kilichopo hapa Udom,” amesema Kabaka.Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula amewaonya wahitimu kuachakuwa sehemu ya walalamikaji na badala yake kutumia fursa zilizopo kujipatia ajira.Mwananchi:
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelewa Ofisini kwake na Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Detlef Waechter na kufanya Mazungunzo.Katika Mazungumzo hayo yalijikita kwenye Mikakati ya pamoja kwenye Maboresho ya Sekta za Afya, Elimu, Usalama na Mapambano dhidi ya Dawa za kulevya.Kuhusu Sekta ya Elimu Balozi huyo ameguswa na kampeni ya Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu kwenye Mkoa wa Dar es Salaam ambapo ameahidi kushirikiana na Rc Makonda katika kampeni hiyo.Aidha Rc Makonda amewasilisha kwa balozi huyo ombi la kujengwa kwa Jengo la huduma ya Dharura (ICU) kwenye Hospital za Mkoa wa Dar es salaam ambapo Balozi amelichukuwa ombi hilo kwaajili ya kulifanyia kazi.Rc Makonda amesema kuwa wamekubaliana kushirikiana katika mapambano ya Biashara ya Dawa za kulevya pamoja na kutoa mafunzo ya namna ya kulinda Jiji kwa kutumia teknolojia.Balozi wa Ujerumani nchini Detlet Waechter amesema watashirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa katika masuala yote ya Maendeleo. Dar yazidi kung"ara Elimu,Afya zazidi kupewa kipaumbele.
Mabasi bila dereva yanatarajia kuanza kufanya kazi mwaka 2022 nchini Singapore.Waziri wa miundombinu Khaw Boon Wan wakati wa ufunguzi wa jaribio la basi la kwanza lisilokuwa na dereva nchini humo,ametangaza kuwa kuanzia 2022 mabasi hayo yataingia barabarani.Ripoti zinaonyesha kuwa huenda miaka mitano ijayo wakazi wa miji tofauti nchini humo wakapendelea zaidi kutumia mabasi yasiyokuwa na dereva hasa kuendea makazini.Teknolojia hiyo itatumika sana katika miji yenye idadi kubwa ya watu.
Unajua unaweza kuwa na mahusiano na mtu unayempenda sana ila yeye hakupendi kama vile umpendavyo lakini anashindwa kukwambia kuwa "sikupendi".Unawakati mzuri sana wa kumtambua mtu ambaye hakupendi na pia kumtambua anayekupenda. Vilevile kukubaliana na hali halisi. Watu wengi hawapendi kutambua kwamba mtu anayempenda yeye hampendi,kwasababu ni maumivu makubwa sana moyoni. Unapokuwa kwenye mahusiano na mtu huyo nae inamuwia vigumu kukwambia "sikupendi" hufanya hivi katika kuzihurumia hisia zako juu yake.Zifuatazo ndizo dalili za mtu ambaye hakupendi kwa dahati1. Anapokuwa nawe inamuwia vigumu sana kukwambia neno NAKUPENDA mara kwa mara, utajikuta wewe ndio unakuwa mtumwa kwake kwa kumwambia nakupenda kila mara. Majibu yake baada ya neno hilo, mara nyingi atakwambia asante kwa kunipenda basi, na akikuhurumia sana atakwambia nakupenda pia ili kukuridhisha wewe na moyo wako.2. Utajikuta una mawazo sana juu yake na kujiuliza "hivi kweli mtu huyu ananipenda?" Utajaribu kumuuliza, "je unanipenda?"Jibu lake kwanza litafikiriwa sana, sababu ya kufanya hivyo ni kwa vile anatambua kwamba hakupendi sasa kukwambia ukweli wa swali lako anahisi utaumia, kwahiyo baada ya swali hilo anaweza kukuuliza swali na wewe "kwani unaonaje?" kwavile unampenda sana utamjibu, "naona kuwa unanipenda" naye atakwambia "basi ndio hivyo".Mara nyingine baada ya wewe kumuuliza swali kuwa je anakupenda kweli, atakujibu "ukweli unaujua ila kwanini unapenda kuniuliza swali hilo kila mara?" kama umeshaingiza dosari juu ya upendo wake utajikuta unamuuliza "ukweli upi?" naye atakujibu "kuwa nakupenda", hapo utajikuta umepata furaha kugundua kuwa anakupenda kumbe mwenzio amekuhurumia tu.5.Huwa hajali mambo yako unayomwambia, ukimueleza muda huu badae anajifanya kusahau ili tu akupotezee mueleleo.6. Unapopanga kukutana nae huwa ni mtu asiyeishiwa na sababu za kushindwa kufika, huwa na aibu ya kukutambulisha kwa watu.Unaweza kufika nae mahali akakwambia kuwa "kuna watu wanafahamiana na mama/baba mahali hapa kwahiyo tusiongozane karibu", hapo anaweza yeye akatangulia mbele au kukuacha wewe utangulie.7. Hufanya tabasamu la kuigiza au kicheko cha kejeli ili wewe uridhike kwamba anafurahishwa na uwepo wako kwake.8. Wakati mwingine inampasa mtu kujitambua na kumpa uhuru huyo umpendaye aweze kuamua mwenyewe labda kuendelea na wewe au kumfata anayempenda yeye.Cha muhimu ni kuwa using'ang'anie mahusiano ambayo yanayoumiza moyo kwani yanaweza pasua moyo wako kwa mawazo.
Lucy Komba.MKONGWE wa filamu nchini anayeishi Denmark, Lucy Komba amemtetea msanii mwenzake Irene Uwoya aliyefiwa na aliyekuwa mumewe, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ na kuwataka watu kumuacha alie
Akizungumza na Za Motomoto News, Lucy alisema watu wanaomponda Uwoya kuhusiana na kifo cha Ndikumana wanakosea kwani hakuna mtu ambaye amewahi kufiwa na mume au aliyekuwa mzazi mwenzake na asilie.“Kiukweli Uwoya mwacheni alie tu hata kama walikuwa wametengana, lakini unaposikia mtu ambaye aliwahi kuwa mume, mpenzi au baba watoto wako amefariki lazima uumie, tena sana kwani kifo ni kitu kingine kabisa, wanaomshambulia wamwache maana wanamuonea tu,” alisema Lucy.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu meneja wa Nyanza Commercial Farm, Dilipkumar Pater, kulipa faini ya Sh milioni 534 ama kutumikia kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na kucha 17 za simba kinyume na sheria.Hukumu hiyo imetolewa leo Novemba 22 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha,Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alisema ameridhika na ushahidi wa mashahidi wanne uliotolewa upande wa mashtaka na vielelezo vitatu kuwa mshtakiwa kweli alitenda kosa hilo Katika kesi hiyo, mshtakiwa Pater alijitetea mwenyewe.Hakimu Mkeha amesema mahakama imemuona mshtakiwa Pater ana hatia baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kesi yao pasipo kuacha shaka.Katika ushahidi, upande wa utetezi waliwasilisha, vielelezo vitatu ambavyo ni kucha za simba, hati ya ukamataji na cheti cha kutathmini kucha hizo.Kabla ya kusomwa hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alimuuliza Wakili wa serikali kama alikuwa na lolote la kusema ndipo, wakili Elia Atanas kwa kushirikiana na wakili Batlida Mushi aliiomba mahakama Kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine.Akijitetea kabla ya kusomewa hukumu hiyo Pater alidai a yeye ni mgonjwa na anategemewa na familia. "Kutokana na ushahidi uliotolewa unaonyesha mshtakiwa alibeba kucha hizo huku akijua ni kosa na akajaribu kuzisafirisha kwenda nchini India kupitia Dubai" amesema Mkeha.Katika kesi hiyo mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Novemba 19, mwaka 2016, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Pater alikutwa na kucha 17 za Simba zenye thamani ya Sh 53,483,500 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Kuonekana kusiko kawaida kwa mamba mweupe mwenye umri mkubwa kumewasisimua wanaofanya shughuli za utalii katika eneo la Kaskazini mwa Australia.Mnyama huyo wa jamii ya wanyama watambaao , aliyepewa jina la bandia -Pearl, alionekana katika ziwa Adelaide River katibu na eneo la Darwin siku ya JumapiliMtu mmoja aliyemuona, ambaye ni mwanaharakati wa hifadhi ya mazingira , alikadiria kuwa mamba huyo alikuwa na urefu wa mita takriban 3 za urefu.Muonekano wa weupe wa rangi wa mnyama huyo umetokana na hali ya hypomelanism - inayosababishwa na ukosefu wa madini ya mwili yanayotengeneza ngozi melanin, kulingana na wataalam wa masuala ya wanyama..Wakazi wa eneo lililo karibu na mto Adelaide wanaamini mnyama huyo ana uhusiano na mamba mwingine anayefahamika kuwa na hali hiyo ya afya ya mwili ambaye aliwahi kumuua mvuvi mnamo mwaka 2014."Kila mmoja anaelezea furaha yake ," alisema rais asiye rasmi wa kikundi cha uhifadhi wa mazingira katika eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja kama Broady."Nilishinda siku nzima nikitokwa na machozi ya furaha nikimtazama."
- Muwindaji alaliwa na kuuwawa na ndovu Zimbabwe
- Mamba mkubwa Big Daddy kufanyishwa ndoa Mombasa
- Alama ya SOS huenda ikapata ufumbuzi Australia
Ni Kwanini mamba ni mweupe?Wengi miongoni mwa mamba nchini Australia wanarangi za kijivu na kijani, jambo linalowawezesha kutoonekana kwa urahisi
Hitilafu ya kimwili ya Mamba Pearlhuenda ilistokea kupitia Jeni ama wakati wa kutengenezwa kwa yai , alisema Adam Britton, mtafiti msaidizi katika chuo kikuu cha Charles Darwin University."Wakati wa kutotoa kama mayai yatakuwa moto zaidi kiasi , inaweza kusababisha hitilafu katika kitengo cha seli na hivyo kusababisha kumeguka ," Alisema Bwana Britton.Alisema matokeo yake yanaweza kuwa ni pamoja na "kuondolewa kwa rangi ya mwili au sehemu nyingine ya magamba kwenye mwili ".Ni hali ya nadra ?Mamba hao si " ni wa kawaida kuonekana'' wakiwa na umri mdogo wanapokuwa na umri mdogo, hususan katika hifadhi ya mamba, kwa mujibu wa Bwana Britton.However, it is difficult for a pale juvenile to steer clear of predators.
"Ni jambo lisilo la kawaida kidogo kumuona mamba mwenye umri mkubwa akiwa na rangi nyeupe kiasi hicho ," Bwana Britton alisema."Nimeisha waona mamba kama huyu kila mara, lakini si mkubwa kiasi hiki mwituni
Makamu wa zamani wa rais wa Zimbabwe, ambaye kufutwa kwake kazi kulishababisha kujiuzulu kwa kiongozi wa muda mrefu Robert Mugabe, ataapishwa rasmi Ijumaa, limesema shirika la utangazaji la Zimbabwe (ZBC)Emmerson Mnangagwa, aliyetorokea nchini Afrika Kusini wiki mbili zilizopita, anawasili leo Jumatano nchini , kulingana na Zanu-PF.
Kuondoshwa kwake madarakani kulisababisha chama na jeshi kwa pamoja kuingilia kati na kulazimisha kumalizika kwa utawala wa miaka 37 wa Bwana Mugabe.Taarifa kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amejiuzulu zilikuja kwa njia ya barua iliyosomwa bungeni Jumanne , bunge likalazimika kuahirisha mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa dhidi yake.Taarifa hiyo iliibua sherehe kubwa kote nchini zilizoendelea hadi usiku wa mananeKatika barua hiyo , Bwana Mugabe alisema kuwa anajiuzulu kwa ajili ya kuruhusu ukabidhianaji wa mamlaka wa amani, na kwamba uamuzi umetokana na utashi wake mwenyewe.Msemaji wa Zanu-PF alisema kuwa Bwana Mnangagwa, mwenye umri wa miaka 71, atahudumu katika kipindi kilichokuwa kimebakia cha utawala wa Mugabe hadi utakapofanyika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Septemba 2018.
Wakati Emmerson Mnangagwa alipofutwa kazi wiki mbili zilizopita hakuwa makamu wa rais wa pekee nchini ZimbabwePhelekezela Mphoko ni makamu wa rais mwengine ambaye anajulikana kwa kumuunga mkono mkewe rais Mugabe na kulingana na sheria anapaswa kumrithi Mugabe.Hatahivyo chama cha Zanu PF kimsema kuwa Mnangagwa ataapishwa kufuatia uamuzi uliochukuliwa na kamati yake kuu siku ya Jumapili.Bwana Mphoko alikuwa ameondoka katika taifa hilo wakati Jeshi lilipochukua mamlaka wiki moja iliopita, na kulingana na gazeti la NewsDay hajarudi nyumbani kwa kuwa anahofia kukamatwa.Gazeti hilo limenukuu duru akisema kuwa amebadilisha mipango yake ya usafiri.Alitarajiwa kurudi nchini zimbabwe kufikia siku ya Ijumaa , kutoka Tokyo Japan.Lakini duru zimesema kuwa anataka tiketi zake za usafiri kubadilishwa ili aelekee Zambia au Msumbiji .Anajua anaogopa kukamatwa kwa sababu anatakikana kwa kuzuia haki na kufanya ufisadi.
Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na wadau waliohudhuria tukio hilo.WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijange, leo ameweka jiwe la msingi eneo la Tabata-Matumbi jijini Dar es Salaam ambapo kiwanda hicho kitakuwa kikisambaza vifaa vya ujenzi.Akizungumza katika hafla hiyo, Mwijage ameipongeza kampuni ya CNBM ya China kwa namna ambavyo imedhamiria kuwekeza hapa nchini kwa kuanzisha kituo cha usambazaji wa vifaa hivyo.Alisema Tanzania na China zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na serikali ya Tanzania itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji wenye nia njema kwa serikali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda.Aliwapongeza pia watu wote wenye nia ya kuwekeza hapa nchini katika miradi mbalimbali ya viwanda kwa upande wa mazao kama vile muhogo, zao ambalo sasa ni muhimu na lenye kuweza hata kuuzika nje ya nchi.Alisisiza kwamba kituo hicho kitawasaidia Watanzania kujipatia ajira na kuongeza ufanisi kwa vijana nchini kwa kunufaika na kituo hicho.Naye Balozi mpya wa China hapa nchini, Bi Wang Ke, alimpongeza Mwenyekiti wa kampuni hiyo ya CNBM, Song Zhiping, kwa kuanzisha kituo hicho ambacho kitakuwa muhimu.
Serikali imesema inampango mkakati mzuri katika kuendeleza sekta ya uvuvi kufika mbele zaidi na kutoa ajira za uhakika kwa Watanzania ambao wanafanya shughuli hiyo.Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta amesma hayo akiwa Soko la Samaki Msasani wakati akifunga maadhimisho ya Siku ya Mvuvi ambayo iliambatana na utoaji wa zawadi kwa wavuvi waliofanya vizuri katika mashindano yakuvua samaki kwa vitumbwi na ngalawa yalioandaliwa na taasisi ya Tuna ambapo mshindi wa kwanza alipata tsh 400,000, wapili tsh 300,000 na wa tatu tsh 200,000.Alisema serikali imesema inampango na mkakati mzuri katika kuliendeleza sekta ya uvuvi kufika mbele zaidi ili sekta hiyo iweze kufanya vizuri na kusonga mbele zaidiMeya alisema wavuvi wanapaswa kuwa wabunifu ili kusaidia sekta hiyo kufanya vizuri zaidiAfisa Uvuvi wa Manispaa Kinondoni Bi Grace Kakama akizungumza katika kilele hicho amesema kama kuwa watahakikisha wavuvi wanafanya kazi katika mazingira mazuri ili waweze kuinuka kwa kipato zaidi.