Wednesday, 22 November 2017

Breaking News: Kafulila ajivua uanachama wa Chadema



Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini mwaka 2010-2015 David Kafulila amejivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Taarifa ya Kafulila kuondoka CHADEMA imetolewa leo kwa vyombo vya habari, na kueleza kwamba hana imani tena na vyama vya upinzani katika kupambana na ufisadi.

David Kafulila anafahamika zaidi kwa kuibua mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa kwa kuibua bungeni suala la Escrow.

VIDEO: Twaweza watoa ripoti ya RUSHWA



Taasisi ya Twaweza imetoa ripoti ya viwango vya rushwa hapa nchini na kuonyesha imepungua kulinganisha na miaka mitano iliyopita. Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Twaweza Aidan Eyakuze.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI... USISAHAU KUSUBSCRIBE



Rais Jacob Zuma awashangaza wengi


Kimya kirefu cha rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma pamoja na chama chake tawala cha ANC kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe kinashangaza.

Kinaonyesha ushawishi wa kisaikolojia aliyokuwa nao kwao na walishangazwa sana na hatua aliyochukua. Kile afisi ya rais Zuma ilichosema ni kwamba hatoweza tena kuelekea nchini Zimbabwe kama alivyokuwa amepanga ili kupatanisha kbal ya rais Mugabe kutangaza kujiuzulu.

Ziara hiyo sasa imeahirishwa hadi tyangazo jingine , taarifa ilisema. Lakini badala yake chma cha upinzani nchini Afrika Kusini DA kilijibu na hivyobasi kuungwa mkono na raia weusi pamoja na wazungu kiliposema:

Huu ni ushindi wa raia wa Zimbabwe ambao wametaabika chini ya uongozi wa Mugabe .Habari ya bwana Mugabe sio geni na kwamba inaendelea katika bara la Afrika.Mtu aliyekuwa shujaa wa taifa lake , Mugabe alisababisha migawanyiko, ukosefu wa udhabiti na kuharibika kwa uchumi wakati alipobadilika kutoka kuwa mpiganiaji wa uhuru hadi kuwa dikteta.Hilo sio tu kwa Mugabe bali hata Zanu -PF chama ambacho amekitawala kwa kutumia nguvu kwa kuchukua mamlaka tangu taifa hilo lijipatie Uhuru.Chama cha ANC kinaonyesha ishara kama zile za Zanu-PF, kimekumbwa na ufisadi mkubwa na ghasia huku pande pinzani zikipigania madaraka katika serikali kwa lengo la kujitajirisha badala ya kuwahudumia wananchi.Baada ya kuchukua madaraka miaka 23 kutoka kwa wazungu ,ANC sasa kinakabiliwa na changamoto ya kujiimarisha au tishio la kuangamiza uchumi wa Afrika kusini kama Zanu-Pf kilivyofanya kwa miaka 37.

Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Kleist Sykes afariki dunia.




Dar es Salaam. Meya wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Kleist Sykes amefariki dunia.

Familia imesema Sykes amefariki dunia leo Jumatano Novemba 22,2017 asubuhi na mipango ya mazishi inaendelea kufanyika.

Skyes aliyekuwa meya mwaka 2000-2005 amefariki dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan.

Mwanamuziki wa kizazi kipya, Dully Sykes ambaye Kleist ni baba yake mkubwa akizungumza na Mwananchi amesema meya huyo wa zamani amefariki dunia leo saa mbili asubuhi.

“ Yaah, kweli amefariki na sasa familia tumeanza kukutana kujua mazishi yatafanyika lini,” amesema.

Meya wa sasa wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza na Mwananchi amesema hivi karibuni alimtembelea hospitalini alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na tatizo la moyo.

Mwita amesema kuna wakati Sykes alimtembelea ofisini kwake na alimpa ushauri kuhusu utendaji kazi.

“Ni mtu tuliyeelewana, amewahi kuja hapa ofisini kwangu kama mara mbili na kunishauri haya na yale kuhusu kazi zangu,” amesema.

Kleist Sykes aliyekuwa diwani wa Kivukoni mwaka 2000 hadi 2005 anatoka katika familia ambayo ni miongoni mwa zenye wanasiasa walioshiriki katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

Mwananchi:

Tshishimbi bado tatizo Yanga, Tambwe aonyesha matumaini



WAKATI mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe amefanya mazoezi kikamilifu kwa mara ya kwanza leo baada ya muda mrefu, kuna uwezekano Yanga SC ikaendelea kumkosa kiungo wake, Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi.

Tshishimbi hakuwepo wakati Yanga SC inaifunga 5-0 Mbeya City Jumapili iliyopita Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Na kuelekea mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Tshishimbi kwa mara nyingine tena leo ameshindwa kuanza mazoezi.

Kocha wa Yanga, Mzambia George ‘GL’ Lwandamina amesema kwamba kati ya majeruhi wake wanne, wengine Wazimbabwe kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji, Donald Ngoma ni Tambwe pekee amefanya mazoezi leo.

Tambwe alifanya mazoezi mepesi ya kukimbia peke yake juzi na jana Uwanja wa Uhuru, kabla ya leo kuungana na wenzake kwa program kamili ya mazoezi.

Lwandamina amesema kwamba inaonekana Tambwe amerudi imara kabisa na leo alionyesha yuko fiti kwa kucheza kwa nguvu na kupiga mashuti ya kusisimua.   

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itaendelea Ijumaa, wenyeji Ndanda FC wakiwakaribisha Njombe Mji FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na Jumamosi, Yanga wataikaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na  Singida United watakuwa wenyeji wa Mbeya City Uwanja wa Namfua, Singida.

Mechi nyingine za jumamosi, Mbao FC wataikaribisha Mwadui FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Kagera Sugar wataikaribisha Stand United Uwanja wa kambarage Shinyanga na Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Maji Maji Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Jumapili Simba SC watakuwa wenyeji wa Lipuli ya Iringa Uwanja wa Azam, Complex na mzunguko wa 11 wa Ligi Kuu inayoonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Azam TV utakamilishwa Jumatatu ijayo kwa mchezo mmoja kati ya wenyeji, Azam FC na Mtibwa Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

UEFA yataja wachezaji 50 wanaowania kuingia kwenye kikosi cha wachezaji 11 bora



Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, leo limetangaza majina ya wachezaji 50 wanaowania kuingia kwenye kikosi cha wachezaji 11 bora mwaka 2017.

Kikosi hicho kimejumuisha wachezaji kutoka vilabu mbalimbali ambao wamefanya vizuri mwaka huu. Waliotajwa ni makipa Gianluigi Buffon, David De Gea, Keylor Navas, Manuel Neuer na Jan Oblak.

Walinzi waliotajwa ni Dan Alves, Bonucci, Carvajal, Chiellini, Camil Glik, Goddin, Kimmich, Marcelo, Mendy, Meunier, Pique, Ramos, Sanchez, Sandro na Valencia.

Kwa upande wa viungo ni Delle Alli, Ansensio, Casemiro, De Bruyne, Eriksen, Fabinho, Hazard, Iniesta, Isco, Kroos, Modric, Mkitharyan, Pyanic, Pogba, na Saul Niguez.

Wengine ni washambuliaji Karim Benzema, Aubamayeng, Aguero, Cavani, Dybala, Falcao, Griezman, Kane, Lewandowski, Mbappe, Mertenes, Messi, Neymar, Ronaldo na Suarez.

Rais mtarajiwa wa Zimbabwe akutana na rais Jacob Zuma Afrika Kusini



 Rais mtarajiwa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amekutana na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati ambapo anasubiriwa kurudi nyumbani leo.

Bwana Zuma alitarajiwa kuwasili atika mji mkuu wa Harare leo ili kuwa mpatanishi wa mgogoro uliokuwa ukiendelea lakini akafutilia mbali zaiara hiyo baada ya rais Mugabe kujiuzulu.

Afisi ya rais Zuma ilituma ujumbe wa Twitter wa picha za mkutano wao.





Dully Sykes: wasanii wa Bongo Fleva wamekuwa kama Kaa




Msanii wa Bongo Fleva, Dully Sykes amewalalamikia wasanii wadogo kiumri kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa kukosa upendo na umoja baina yao kwa kutokupeana sapoti kwenye kazi zao.

Dully amesema Wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa kwenye muziki ambao amewaita madogo hawana upendo wala umoja katika kusapotiana na kudai kuwa sio tu kwa wasanii wakongwe bali hata hao wenyewe kwa wenyewe na kuwafananisha na mdudu Kaa.

“Vijana wa sasa hivi wanatakiwa wajifunze kupendana, vijana wa sasa hivi hawapendani yaani hawana mapenzi, hawana ule upendo wamekuwa kama Kaa, Mimi nilijaribu kutuma posti yangu (ya wimbo mpya) juzi nikitegemea kupata nguvu nyingi kutoka kwa vijana lakini imekuwa tofauti na nilivyofikiria kwani wazee wenzangu ndio wamenipa sapoti akina Rich One, akina Mwana FA ndio walinisapoti na ndio walikuwa na furaha, kuna vijana wengine mpaka wanasema  kwamba nimetoa wimbo lakini hawajui  kama mimi nimetoa wimbo, wengine wanasema nitakupostia lakini hawaposti.“amesema Dully Sykes kwenye mahojiano yake na Radio Free Afrika Kwenye kipindi cha New Chapter na kuwapa ushauri wasanii hao

“Sasa mimi naomba tu kuwambia wale vijana ambao wanahisi labda muziki ni wa kwao peke yao hapana.. Unajua Mungu sisi wengine sisi ametupa utofauti mimi nakula majani kama Twiga wakae watulie, hao watakula majani chini kama Mbuzi, mimi nitakula ya juu, Wakae watambue kuwa wasishindane na Tembo wataumiza makalio.”

Rais mtarajiwa wa Zimbabwe awasili mjini Harare



Rais mtarajiwa wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amerudi nchini humo kutoka Afrika Kusini.

Anatarajiwa kutoa hotuba yake katika makao makuu ya chama cha Zanu-PF mjini Harar

Marekani yatangaza kuwaua magaidi 100 nchini Somalia



Jeshi la Marekani latangaza kuwaua wanamgambo 100 wa kundi la kigaidi la al Qaida  katika kambi ya al Shabaab nchini Somalia.

Jaeshi la Marekani katika kÅŸtengo chake kwa ajili ya Afrika limefahamisha kuwa jeshi la anga la Marekani limeshambulia kambi ya wanmagmbo wa al Shabaab inayopatikana katika umbali wa kilomita 200 na jiji la Mogadishu.

Zaidi ya magaidi 100 wa kundi hilo wameuawa katika shambulizi hilo.

Kundi la al Shabaab kwa ushirikiano na kundi la al Qaida na Daesh  yanashukiwa kuendesha shambulizi la bomu mjini Mogadishu na kusababisha maafa makubwa.

Watu zaidi 350 walifariki katika shambulizi hilo lilitokea mjini Mogadishu.

Kim Jong Un: Marufuku pombe na muziki Korea Kaskazini

Kim Jong Un: Marufuku pombe na muziki Korea Kaskazini




Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amepiga marufuku mashirika ya burudani yakiwemo yale ya pombe na muziki.

Kwa mujibu wa habari,Korea Kaskazini imefanya hivyo kwa nia ya kudhibiti uchumi wa nchi hiyo hasa baada ya vikwazo vilivyowekwa na Umoja wa mataifa,

Korea Kaskazini imewekewa vikwazo vingi kutokana na kukiuka masharti na kuendelea kutengeneza makombora ya nyuklia.

Wananchi nchini humo wamekuwa wakijaribu kuishi ndani ya matakwa ya serikali.

Mbali na kuwa vigumu kwa wananchi wa Korea Kaskazini kusafiri nje ya nchi,utumiaji wa mitandao ya kijamii bila idhini ya serikali nao umedhibitiwa vilivyo.

Hata hivyo Pyongyang haionyeshi dalili zozote za kaucha kufanya majaribio ya makombora ya nyuklia.

Katambi amjibu Mbowe, amwambia hanunuliki

Katambi amjibu Mbowe, amwambia hanunuliki


Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrobas Katambi amesema tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba amenunuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hazina ukweli.

Katambi ambaye jana alitangaza kujiunga na CCM ametoa kauli hiyo kipindi ambacho kumekuwa na tuhuma zinazoelekezwa kwake  ikiwamo ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwamba ameshawishiwa na akakubali.

Akizungumza na Mwananchi leo Novemba 22, Katambi amesema hakuna mtu yoyote anayeweza kumnunua huku akisema Chadema kimepoteza dira hivyo wenye uelewa wataondoka.

“Nimesikia mengi, nitafanya mkutano na waandishi wa habari, nilidhani wangejitathimini katika ukweli ili kusaidia vijana, chama na taifa lakini kama wanaamua kushambulia mtu kwa uongo bila ushahidi, nitasema ukweli waziwazi,” amesema Katambi

Kuhusu tuhuma za rushwa, Katambi amesema ‘’Katambi hanunuliki wala hana bei naishi katika Principle…kwa wenye akili wangejua dira imepotea watafute upya masafa.”

Awali leo asubuhi, Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni akizungumza  na Mwananchi kuhusu kuondoka kwa Katambi amesema;

"Badala ya nguvu na fedha kuzielekeza kujenga viwanda wao nguvu wamezielekeza kushawishi viongozi wetu, wamewashwishi wengi na Katambi ni miongoni ingawa wengine wamekataa."

Mwananchi:

DIAMOND PLATNUMZ FT MORGAN HERITAGE _HALLELUJAH COVER