Wednesday, 22 November 2017

VIDEO:Ruge afunguka baada ya Jengo la Clouds kuwaka moto full Video.



Moto uliozuka katika ofisi za Clouds Media Group na kusababisha Television na Radio Clouds kutokuwa hewani kwa muda, Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group amesema bado huduma ya vipindi nitaendelea kama kawaida.

Moto huo ulianza saa 4 asubuhi katika chumba kimoja kwenye ghorofa ya kwanza uliosambaa kwenye jengo la kampuni hiyo.


Hata hivyo hadi sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana.

Magari ya Zimamoto yapatayo manne yalifika eneo la tukio kwa ajili ya kuzima moto huo.

Aidha  Ruge Mutahaba amewashukuru Zimamoto kwa kuweza kuokoa vifaa na kuzima moto huo.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE







ais Magufuli afanya uteuzi huu



 Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amemteua Bw. Edwin Novath Rutageruka kuwa Mkurugenzi wa TANTRADE.

Mr. Nice afunguka haya



Msanii Mr. Nice ambaye siku nyingi amekuwa kimya kwa kutotoa kazi mpya, amejitapa na kusema kwamba kazi zake za mwanzo zilimpa faida kubwa na kuwekeza kiuchumi, kitendo ambacho kimemfanya aishi maisha ya raha sasa hivi.

Akipiga stori na Big Chawa wa Planet Bongo kwenye East Africa Radio, Mr. Nice amesema kutokana na fedha alizopata alijenga nyumba yake mwenyewe, na kwamba mpaka sasa yuko vizuri kiuchumi kani hata kufua hafui kwa mkono bali hutumia mashine, na hata akienda chooni habebi kopo na kusindikizwa na mbwa kama ilivyo kwa watu wengi wa kipato cha chini.

Mdogo wa Ndikumana awapa makavu bongo movie




Mdogo wa marehemu Hamadi Ndikumana ambaye alikuwa mume wa muigizaji wa filamu Tanzania Irene Uwoya, anayeitwa  Laddy Ndikumana, amesema waigizaji wa filamu wa bongo (bongo movie ) ni wajinga, kutokana na mambo yao wanayoyafanya.

Laddy ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba waigizaji hao ni wajinga na wanafiki kwa kuwa wameshindwa kufika kwenye msiba wa kaka yake Ndikumana, ambaye wakati wa uhai wake walijifanya kuwa rafiki yao na kumpenda.

Laddy ameendelea kwa kusema kwamba wakati marehemu Ndikumana alipokuwa na pesa, wasanii hao walikuwa marafiki na kula naye bata, lakini wameshindwa kujitokeza kwenye msiba, na kumuacha Irene Uwoya peke yake kwenda Rwanda.

Lowassa akanusha taarifa za kutaka kurejea CCM



Arusha. Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema hana mpango wa kurejea CCM kama ambavyo taarifa zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na Mwananchi  leo Jumanne,  Lowassa amesema amepata taarifa za uvumi unaosambazwa kuwa kuna watu amewatuma kuomba arudi CCM jambo ambalo ni uongo.

"Huu ni uongo wa kutunga, wamekuwa wakitunga vitu vingi juu yangu, mimi sina mpango wa kurejea CCM," amesema Lowassa,ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema  .

Amesema uongo mwingine ambao unasambazwa ni kuwa Serikali imezuia watu kumtembelea nyumbani kwake jambo ambalo anaamini ni maneno yanayotungwa.

"Watu wanazuiwa kuja nyumbani kwangu, eti Serikali imezuia hivyo wanakuwa wanaogopa huu ni uongo Serikali haiwezi kuzuia watu kutembeleana," amesema.

Tuesday, 21 November 2017

BREAKING NEWS: Ajali ya moto iliyotokea ofisi za Clouds Media


KUTOKA AFRIKA : Mastaa wa Kike wanaokimbiza Hollywood


Watanzania kukutwa na heroini Swaziland



  Dar es Salaam. Watanzania watatu wamekamatwa nchini Swaziland kwa tuhuma za kukutwa na kilogramu 30 za dawa za kulevya aina ya heroini zilizokuwa zinapelekwa Afrika Kusini.

Kamishna mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Rogers Sianga alisema jana kuwa Watanzania hao walikamatwa mpakani mwa nchi ya Msumbiji na Swaziland wakiwa na mzigo huo.

“Kinachofanyika sasa ni kwamba tunashirikiana na nchi ya Swaziland ili kujua watanzania hao wanashirikiana na akina nani na mtandao wao kwa ujumla,” alisema Sianga.

Taarifa zinadai kuwa Watanzania hao walikamatwa juzi na maofisa wa polisi wa Swaziland wakiwa na dawa za kulevya zilizofichwa ndani ya buti la gari.

Maofisa hao baada ya kufanya upekuzi walibaini mifuko ya plastiki miwili ya rangi nyeusi.

Inadaiwa kuwa kila pakiti yenye dawa hizo iliwekwa pilipili ili kuzuia mbwa waliokuwa wanatumiwa kupekuwa wasibaini harufu za dawa hizo za kulevya.

“Kwa kuwa sasa hivi tumewabana wafanyabiashara hao haramu wa dawa za kulevya, wameamua kukimbilia Msumbiji kwa ajili ya kufanya biashara hiyo. Soko kuu lipo Afrika Kusini na mara nyingi wanawawekea dhamana (bond) vijana kusafirisha na wanapofanikiwa wanalipwa fedha zao,” alisema.

Alifafanua kuwa kutokana na kushamiri kwa wafanyabiashara hao, Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imefanyiwa marekebisho ya sheria mpya kifungu cha 15 ikiwamo kuongezea kosa la kuweka mtu rehani kwa minajili ya kufanikisha biashara hiyo, huku adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.

Kamishna wa Kitengo cha Huduma za Sheria, Edwin Kakolaki alisema makosa mengine chini ya kifungo hicho ni kusafirisha dawa za kulevya na kuchepusha, kusafirisha isivyo halali kemikali bashirifu.

Kakolaki aliongeza kwamba marekebisho mengine ya sheria hiyo ni kuipa uwezo mamlaka hiyo kushughulikia makosa mengine yenye uhusiano wa moja kwa moja na biashara na matumizi ya dawa za kulevya kifungu cha 4(2)(f).

Zaidi ya hilo pia alisema kwamba marekebisho mengine yanampa uwezo kamishna jenerali kushikilia akaunti za benki za mtuhumiwa kwa muda, kwa mujibu wa kifungu kipya cha 50A kwa wauzaji wa dawa za kulevya za kiwandani.

“Pia, adhabu kwa makosa hayo itakuwa kifungo miaka 30 bila faini, ikumbukwe kuwa adhabu hii haiwahusu watumiaji wa dawa za kulevya ambao sheria inawachukulia kama wagonjwa endapo kutakuwa na uthibitisho wa daktari kwamba ni watumiaji na wameathirika na dawa hizo,” alisema Kakolaki. 

Nape afunguka kuhamia upinzani



Mtwara. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nauye amesema hana mpango wa kuhama CCM kwenda upinzani na badala yake ametaka vyama hivyo visipoteze muda kudhania atahama.

Nape ametoa kauli hiyo jana Jumatatu jioni wakani wa kampeni za kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Reli, Genfrid Mbunda katika uwanja wa Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Alisema wapinzani wasipoteze muda wakimsubiri kuwa atahama CCM kutokana kwamba CCM ni chama bora kuliko vyama vyote vya siasa hivyo hawezi kutoka ndani ya chama hicho.

“Unajuwa wapinzani wasipoteze muda wa kusubiri mimi lini nitahama CCM badala yake wafanye kazi ya kuvijenga vyama vyao kwa sababu walitamani sana muziki huu uhamie kwao ndio maana wanabaki wanapiga kelele za kuwapa presha wanaCCM hivyo sitahama kwa sababu ukinikata mwili wangu damu yangu unakuta CCM,” alisema Nape.

Alisema kuwa CCM hakwenda kwa bahati mbaya kutokana kwamba anakijua chama hicho hivyo hakuna namna yoyote itakayoweza kumtenganisha na chama hicho.

“Kupitia changamoto katika mabonde na mawimbi ndio unaandaliwa kuwa mkomavu na kupanda juu kwa sababu ukikimbia mapema unaonekana haufahi lakini ukibaki na kuvulimia milima na mabonde ndio unaokana ni mkomavu na ukizingatia ndani ya chama hiki kuna fursa za kutosha,” alisema.

“Kupitia mabonde na milima bila kuyumba nitaendelea kusimama imara ndio maana nikaaminiwa sasa wanaodhani Nape anapitia milima na mabonde kwa sababu hata mbegu ili iote ni lazima upande chini ili iweze kuota na hiyo ndio fomula ya maisha sasa wakati mbegu inaoza watu wanaanza kuongea siji ng’o,” aliongeza Nape.

“Mimi bado sijaona mawimbi yanayoweza kumkimbiza  CCM bado nimesimama imara kwa ajili ya kupambana na mawimbi hakuna mabadiliko yasiyo na machungu hata mama mjazito hupata machungu lakini hufurahi kupata mtoto baada ya kuvumilia kwa muda mrefu,” alisema Nape.

Mourinho aandaa mpango mpya Man United



Hakuna bata! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kocha wa Manchester United, Jose Mourinho kukipangia kikosi chake programu ya kufanya mazoezi Siku ya Krismas kwenye Uwanja wa Old Trafford kutoka uwanja wao wa kawaida wa mazoezi, Carrington.

Mourinho, amewapangia programu hio mpya wachezaji wake kuelekea kwenye mchezo wa Siku ya Kupeana Zawadi (Boxing Day) dhidi ya Burnley itakayoanza saa 11 jionii  ndani ya dimba hilo.

Maamuzi hayo ya kuhama Carrington, ndani ya Krismas yanatarajia kuwahusisha wafanyakazi wengine 50 au zaidi ambao watakua kwenye majukumu mbali mbali siku hio huku wakikosa kuutumia muda huo kujivinjari na familia zao.

Mazoezi ndani ya viwanja vya Carrington hujumuisha wafanyakazi 20 lakini kufuatia mabadiliko hayo, idadi ya wafanyakazi inatarajiwa kufikia hadi 70 watakaoshughulikia masuala mbali mbali ikiwemo ulinzi na uandaaji wa dimba hilo.

Profesa Kitila, Katambi, Msando waingia CCM


Dar es salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo ametangazwa rasmi leo Jumanne mbele ya mkutano wa NEC, CCM unaoendelea Ikulu jijini Dar es salaam.

Mbali na Profesa Kitila ambaye alikuwa kada wa ACT, pia kuna Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Kitambi ambaye ni Mwenyekiti wa Bavicha, Lawrence Masha, Samson Mwigamba na Albert Msando.

Akizungumza mbele ya mkutano huo, Profesa Kitila amesema: "Nguvu ya CCM zipo tano, moja ni kwamba ni chama cha watu, ni chama pekee chenye nguvu siyo chama kuogopa watu, tulijaribu huko tulipokuwa lakini yalishindwa."

Kwa upande wake, Masha amesema alipoamua kuondoka, baba yake alisikitishwa na uamuzi huo lakini baada ya kutafakari ameamua kurejea nyumbani.

Amesema yeye ni mwanaCCM na kijana alilelewa ndani ya chama hicho.

"Mwenyekiti wewe ni mfugaji, ng'ombe akiingia zizini amekatwa mkia unamwangalia mara mbili mbili, mimi sijakatwa mkia ni mwaminifu, ukinihitaji nitumie, kudumu Chama cha Mapinduzi," amesema Masha.

Kwa upande wake Mwigamba amesema hoja zote walizopigania Rais John Magufuli kwa sasa anazitekeleza. Kutokana na hali hiyo analazimika kumuunga mkono.

"Lakini ni bahati mbaya wapo wanaoamini upinzani ni kama, tumeamua kuwa moto, wanaposema huyo amenunuliwa, mie ndiyo naendelea kuwa moto.”

Yeye Msando amesema  baada ya kutoka Chadema kwenda ACT amejitambulisha rasmi kujiunga na chama hicho.

Amesema anafarijika kuona chama hicho na haoni aibu kuwa karibu na CCM tofauti na ilivyokuwa miaka ya zamani kwani wanachama walihofia kuvaa mavazi ya chama hadharani kwa kuogopa kuzomewa.

"Kwa sasa chini ya uongozi wako, mtu anajivunia kuwa mwanachama wa CCM, tukaona juhudi zinazoendelea," amesema Msando.

Nafasi za kazi leo November 21

BoT imeeleza hali ya uchumi wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeeleza  kuwa, Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika katika kipindi cha muongo mmoja uliopita yaani kuanzia mwaka 2007  hadi  2016


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchumi BoT, Johnson Nyella jana jumatatu kwenye sherehe ya Siku ya Takwimu Afrika (2017), iliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam ambapo alieleza kuwa  uchumi wa Tanzania ulikua kwa wastani wa asilimia 6.7 mwaka 2016, wakati pato la taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 7, sawa na ilivyokuwa mwaka 2015 na 2014.

Bw. Nyella amesema  kwa miaka minne mfululizo, mfumuko wa bei wa Taifa umeendelea kupungua na kubaki katika kiwango cha tarakimu moja.

“Mwaka 2016 mfumuko wa bei ulipungua na kufikia wastani wa asilimia 5.2 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 5.6 mwaka 2015 na asilimia 6.1 mwaka 2014.” amesema Nyella huku akielezea umuhimu wa Takwimu bora.

Takwimu bora za uchumi zinahitajika katika kupanga mipango ya maendeleo na utungaji wa sera kwa ajili ya kuboreshamaendeleo endelevu ya mwaka 2030.

Kwa mujibu wa Nyella, takwimu bora za kiuchumi zinasaidia kuongeza tija serikalini katika kupanga mipango ya maendeleo na kukabiliana na changamoto kadri zinavyojitokeza.

Amesema takwimu bora pia zinawasaidia watunga sera na watekelezaji wa programu mbalimbali na kupanga mikakati mipya ya kuboresha maisha ya wananchi.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa amesema kwenye sherehe hizo kuwa, takwimu bora za uchumi ni muhimu katika kufikia ajenda ya Bara la Afrika ya mwaka 2063 inayosisitiza ukuaji wa uchumi.

Katika kufikia ajenda hiyo, baadhi ya mambo yanayosisitizwa ni amani, utulivu, kuboresha uchumi wa Afrika, kukusanya mapato ya Afrika ili Afrika iweze kujitegemea.

Dk Chuwa, amesema Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi ya Afrika (UNECA) kwa kushirikiana na Ofisi za Takwimu za Afrika, ina kaulimbiu isemayo “Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora” ikisisitiza umuhimu wa takwimu za kiuchumi katika kuleta maendeleo endelevu hivyo kuboresha maisha ya wananchi.

Kaulimbiu hiyo inaakisi juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli kwa kuwa na dhamira ya kutengeneza uchumi wa viwanda. Amesema kwa sababu hiyo, takwimu rasmi za uchumi za serikali lazima zitolewe kwa weledi na kwa kufuata kanuni na sheria.

“Takwimu bora za uchumi kwa nchi yetu ni za muhimu sana, hasa wakati huu ambao Serikali yetu inaimarisha uchumi wa viwanda ili Tanzania iweze kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 na kuboresha zaidi maisha ya wananchi. Takwimu hizi za uchumi ni pamoja na takwimu za kilimo, viwanda, ujenzi, usafirishaji, nishati, biashara, mazingira, mfumuko wa bei na uwekezaji.”amesema Dkt. Chuwa.

Dkt. Chuwa amesema takwimu bora ni takwimu zilizo sahihi, zinazotolewa kwa wakati, linganifu na za kina, zinazozalishwa mara kwa mara na zenye ufanisi. Dk Chuwa alisema, sifa hizo zote zinaendana na kanuni za msingi za takwimu rasmi za Umoja wa Mataifa na Mkataba wa Takwimu wa Afrika, ambazo maisha ya wananchi, hasa kutekeleza ajenda.