Sunday, 19 November 2017

MAGAZETI YA LEO 19/11/2017

MAGAZETI YA LEO 19/11/201                           


Msuva atemwa kwenye kikosi cha Challenge



KOCHA Ammy Ninje hajamjumuisha winga Simon Msuva wa Difaa Hassan El-Jadida ya Morocco katika kikosi cha Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kuanzia Desemba 3, mwaka huu Jijini Nairobi, Kenya.

Badala yake, Ninje amemchukua winga wa Fanja ya Oman, Daniel Lyanga kwenye kikosi chake cha wachezaji 20 aliowataja leo mjini Dar es Salaam.

Katika kikosi hicho, Ninje mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameita makipa wawili tu, Aishi Manula wa Simba na Peter Manyika wa Singida United. 

Mabeki ni Boniphace Maganga, Gardiel Michael, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Kennedy Wilson.

Viungo ni Himid Mao, Hamisi Abdallah, Muzamil Yassin, Raphael Daudi, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Ibrahim Ajib na Abdul Hilal, wakati washambuliaji ni Elias Maguri, Mbaraka Yusuph, Yohana Nkomola na Daniel Lyanga.

Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi A pamoja na ndugu zao, Zanzibar, wenyeji Kenya, Rwanda na waalikwa Libya, wakati Kundi B lina timu za Uganda, Zimbabwe, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.

Kilimanjaro Stars itafungua dimba na Libya Desemba 3, mwaka huu mchezo ambao utafuatiwa na mechi kati ya wenyeji, Kenya dhidi ya Rwanda.

Kili Stars itarudi uwanjani Desemba 7 kumenyana na Zanzibar Heroes, Desemba 9  na Rwanda kabla ya kumaliza mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na wenyeji, Kenya Desemba 11.

Mechi za makundi zinatarajiwa kukamilishwa Desemba 12 na Nusu Fainali zitachezwa Desemba 14 na 15, wakati Desemba 16 itachezwa mechi ya kusaka mshindi wa tatu ikifuatiwa na fainali.

CECAFA Challenge ndiyo michuano mikongwe zaidi ya soka barani Afrika ambayo ilianza mwaka 1926 ikijulikana kama Kombe la Gossage hadi mwaka 1966, ilipobadilishwa na kuwa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati hadi mwaka 1971 ilipobadilishwa tena na kuwa CECAFA Challenge.

Wadhamini tofauti wamekuwa wakiingia na kutoka kwa kipindi chote hicho, lakini taarifa zinasema kuanzia mwaka huu Televisheni namba moja Afrika Mashariki na Kati, Azam TV ndiyo wanakuwa wadhamini wapya ambao pia watakuwa wanarusha moja kwa moja michuano hiyo.

Uganda ndiyo mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo tangu mwaka 1971, wakiwa wamelitwaa mara 14, wakifuatiwa na Kenya mara sita, Ethiopia mara nne na Tanzania mara tatu.

Uganda, The Cranes pia ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa taji la michuano hiyo mwaka 2015 nchini Ethiopia wakiwafunga Rwanda 1-0 kwenye fainali mjini Addis Ababa, wakati mwaka jana michuano hiyo haikufanyika kwa sababu ya kukosa nchi mwenyeji.

Alietajwa kufariki ajali ya ndege kumbe yupo hai



Mfanyakazi wa hoteli za kitalii za andBeyond Serengeti, Moses Muhina aliyetajwa kuwa ni miongoni mwa abiria waliofariki dunia katika ajali ya ndege ya Shirika la Coastal Aviation, imebainika alibadili ndege muda mfupi kabla ya safari ili kuwahi kazini.

Muhina ambaye ni mwongozaji watalii katika hoteli hiyo, alikuwa aondoke na ndege ya Coastal Aviation saa nne asubuhi lakini viongozi wa hoteli walimbadilishia ndege, hivyo aliondoka na Air Exel iliyofika salama Serengeti.

Akizungumza na gazeti hili, meneja uendeshaji wa Hoteli ya andBeyond Serengeti Under Canvas, Mussa Matala alisema Muhina ambaye anasomeka kwenye orodha ya ndege kama Maina alikuwa apande ndege hiyo lakini walimbadilishia.

Alisema waliomba aondolewe kwenye orodha ya wasafiri wa ndege hiyo lakini kwa bahati mbaya hadi ndege ilipoondoka jina lake lilikuwapo.

Wakati huohuo, raia watano wa kigeni ambao walifariki dunia katika ajali hiyo, akiwamo rubani Dewald Raubenheimer raia wa Afrika Kusini, ambaye kwenye orodha ya awali ya waliofariki jina lake halikuwapo anatarajiwa kusafirishwa leo.

Mhudumu wa chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya mkoa ya Mount Meru, Francis Costa alisema miili mitatu kati ya 11 imechukuliwa na ndugu zao.

Alisema miili iliyochukuliwa ni ya ndugu wawili waliokuwa wakurugenzi wa Masai Wondering, Nasibu na Shatri Mfinanga.

Mwingine ni wa Joyce Mkama ambaye alikuwa mfanyakazi wa Hoteli ya Serena.

“Uchunguzi wa miili ya wageni kutoka nje ya nchi unaendelea na ukikamilika itasafirishwa kwa mazishi katika nchi za Afrika Kusini, Ujerumani na Italia,” alisema.

Ndege hiyo namba 5H-EGG aina ya Cessna Grand Caravan ilianguka baada ya kugonga kingo za creta ya Empakai, umbali wa mita 3,250 kutoka usawa wa bahari ikitoka Kilimanjaro kwenda Hifadhi ya Serengeti.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema uchunguzi unaendelea kuhusu ajali hiyo.

Chelsea yaitwanga West Bromwich 4-0

Chelsea imeshangilia ushindi mwingine wa EPL kwa kuichapa Wes Borm kwa mabao 4-0.

Wakati inashinda kwa idadi hiyo, kiungo wake Eden Hazard anaonekana kuamka baada ya kufunga mabao mawili.

Wengine waliofunga ni Alvaro Morata na Alonso ambao kila mmoja alifunga bao moja.

Msafara wa Lowasa wapigwa mabomu Moshi



Polisi Mkoa wa Kilimanjaro wamelazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi kumwezesha mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kupata nafasi ya kupita mjini Moshi.

Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi waliokuwa wamefunga barabara.

Takriban mabomu manne ya kutoa machozi yalifyatuliwa saa 10:30 jana jioni ya  Jumamosi Novemba 18,2017  katika eneo la Soko la Manyema ambako Lowassa na msafara wake alikuwa apokewe ili kuelekea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za udiwani eneo la Pasua Relini.

Kabla ya Lowassa kufika, vijana madereva wa bodaboda walipita katika Barabara ya J.K. Nyerere.

Vijana hao walipopita mzunguko wa magari wa Coca Cola saa 10:15 jioni, gari la polisi aina ya Toyota Land Cruicer likiwa na polisi wenye mabomu ya machozi lilionekana likiwafuata.

Haikupita dakika 15, ndipo kulisikika milio ya mabomu katika eneo la Manyema ambalo ni njia panda ya kuelekea eneo la mkutano.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema ambaye yuko katika msafara wa Lowassa, alisema eneo la Manyema lilikuwa halipitiki kutokana umati wa watu.

Lema alisema ni kutokana na hali hiyo, ili kumwezesha Lowassa na msafara wake kupita, FFU walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alisema mabomu hayo yamepigwa ili kupunguza idadi ya watu waliokuwa wamefurika kwenye eneo hilo na kumuwezesha Lowassa kupita.

“Alikuwa hana njia ya kupita, watu walifurika kiasi kwamba hata Lowassa mwenyewe asingeweza kupita, tulifanya hivyo kuwapunguza na ameshapita ameenda zake kwenye mkutano,” alisema.

Lema : Nipo tayari kuuza figo yangu kugharamia matibabu ya Lissu




Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amesema hata kama gharama za  matibabu ya Tundu Lissu yakifika Trilioni  moja, watakuwa tayari kuuza figo zao.

Akizungumza jana  Novemba 18 katika kata ya Siuyu iliyopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Lema alisema utekelezaji wa  majukumu ya kisiasa ukiwa upinzani wakati huu ni ngumu kutokana na kuwindwa kila uchao.

Alisema  pamoja na ugumu huo hawajarudi nyuma na kisasi cha wasiopenda mabadiliko na wanaochukia kukosolewa   kimedhihirika  kwa vitendo alivyotendewa Lissu.

"Lissu yupo kitandani risasi mwili mzima, gharama za matibabu yake ni kubwa, lakini hata ikifika trilioni moja na tukawa hatuna fedha tutauza figo zetu kuendelea kugharamia matibabu yake" alisema Lema.

Alisema Lissu amekuwa alama ya haki katika taifa kutokana na kuamua kuwa upande wa haki.

Mama huyu avunja rekodi “Madrid Derby” iliyodumu kwa miaka 86



Ukiachana ns ile Derby ya kaskazini mwa London itakayopigwa pale nchini Uingereza hii leo, kule katika ligi kuu nchini Hispania katika dimba la Wanda Metrpolitana kutakuwa na derby nyingine.

Real Madrid ambao msimu huu wanaonekana kuchechemea watakuwa wageni wa Atletico Madrid ambao nao toka msimu uanze wanaonekana kutokuwa vizuri kama ilivyo kwa majirani zao.

Py Laurance anaweza kuwa mtu pekee ambaye anakwenda katika mchezo huu akiwa na presha kubwa kwani hatapenda timu yoyote kati ya Atletico Madrid au Real Madrid ipoteze mchezo wa hii leo.

Py ni mama mzazi wa mlinzi wa kushoto wa Atletico Madrid Theo Hernandez lakini vile vile Py huyuhuyu ndio mama mzazi wa mlinzi wa Real Madrid Lucas Hernandez jambo linalomfanya kushabikia timu zote mbili.

Katika mahojiano na jarida la Marca mwanamama huyu ameeleza kwamba kabla ya mechi ya leo aliwaita na kuwaambia kwamba anawapenda sana na akiwasisitiza wasipigane kwa kuwa wao ni ndugu.

Py anakuwa mzazi wa kwanza kukutanisha watoto wake katika mchezo wa Madrid Derby tangu jambo kama hili lilipotokea katika msimu wa mwaka 1929/1930 na tangu kipindi hicho hakuna aliyeweza kuvunja rekodi hiyo.

Real Madrid na Atletico Madrid wote wana alama sawa (23) na atakayeshinda katika mchezo wa leo atakaa juu ya mwenzake na kupunguza pengo la alama na vinara Barcelona

Wazimbabwe waandamana kumtaka Mugabe ajiuzulu



Maelfu ya raia wa Zimbabwe jana walijitokeza barabarani hasa mjini Harare wakijiandaa kwa mkutano mkubwa unaoungwa mkono na chama tawala ZANU-PF katika jitihada za kuongeza shinikizo la kumtaka rais Mugabe ajiuzuulu,wakishikilia mabango yaliyoandikwa 'Mugabe Must Go'.

Zanu-PF ndio chama kilichomsaidia Mugabe kuwa madarakani nchini kwa takriban miaka 40.

Lakini sasa inabidi wamshinikize ajiuzulu kufuatia mpasuko mkubwa katika chama tawala.

Kikubwa kinachodhaniwa ni nani atakayemrithi rais Mugabe atakapoochia madaraka.

Jeshi la nchi hiyo lilichukua hatamu za kiserikali na kumuweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazungumzo ya kina.

Mugabe angependelea mkewe kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe alimfuta kazi wiki iliyopita, kutokana na uhasama mkubwa baina yake na mkewe rais Mugabe uliotokana na upiganiaji huo wa madaraka.

Zaidi ya hayo Rais Mugabe angependa kuendelea kuwa uongozini hadi chama kitakapofanya mkutano wao mkuu mwezi ujao.

CHUO CHA ST DAVID KIMARA DAR KINATANGAZA NAFASI ZA MASOMO



CHUO CHA ST DAVID COLLEGE OF HEALTH KILICHOPO KIMARA TEMBONI DSM NI CHUO CHA KIPEKEE KATIKA UKANDA HUU WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KINACHOTOA KOZI ZA AFYA KWA NGAZI ZOTE ZA CHETI NA DIPLOMA.

SIFA KUU NI UFAULU MASOMO YA SAYANSI IKIWEO HESABU NA KIINGEREZA ANGALAU ALAMA D.

ADA ZETU NI NAFUU UTALIPA KIDOGO KIDOGO KUKIDHI UWEZO WAKO, KWA MAWASILIANO 0626 231 364 / 0786 658 535 /  0716 044 610 / 0718 229 977 AU INGIA MTANDAONI  www.stdavidcollege.ac.tc

WAHI SASA MUHULA MPYA TAYARI UMEANZA.
PIA KUNA KOZI MAALUMU KWA WOTE WASIO NA VIGEZO KAMILI KUMUWEZESHA KUPAMBANA MPAKA AFIKIE VIWANGO NA KUJIUNGA NA MEDICINE..CA/CO

JIUNGE NA KOZI INAYOTOLEWA ST DAVID COLLEGE PEKEE IITWAYO PRE-MEDICINE PROGRAME KWA KUSHIRIKIANA NA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA NECTA TUMEKUANDALIA NJIA RAHISI KABISA.

FIKA SASA KIMARA TEMBONI ZAMANI MOA AU OFISI ZETU ZILIZOPO MWANANYAMALA A CCM MINAZINI KWA DR DAVID B.MWANGANDA.

CHUO NI CHA KUTWA NA BWENI.







Mbunge Nassari atumia CD kufanya kampeni

Mbunge Nassari atumia CD kufanya kampeni



Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemnadi kitofauti mgombea udiwani wa Kata ya Ambureni, Dominick Mollel kwa kugawa CD anazodai zinaonyesha baadhi ya madiwani wa chama hicho wilayani Arumeru walivyoshawishiwa kupokea rushwa.

Nassari aligawa zaidi ya nakala 500 katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Kwa Pole wilayani hapa huku akiwataka wananchi kutowachagua wagombea wa CCM kwa kudai baadhi yao wanatuhumiwa kupokea rushwa.

Nassari amefafanua kwamba pamoja na kuwasilisha ushahidi wake Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ameamua kugawa nakala hizo kuwafungua macho wananchi waelewe kwamba wagombea kutoka CCM hawafai.

Akizungumzia kitendo cha baadhi ya wagombea wa CCM kutoa ahadi ya kuyakomboa baadhi ya mashamba yaliyotwaliwa na wawekezaji wilayani humo, Nassari amesema kwamba wakati hao wanatoa ahadi jukwaani wao wataingia shambani kudai haki.

“Wakati wao wanaahidi kushughulika na nyaraka sisi watatukuta shambani tunaendelea na kazi sawa,” alisema Nassari.


John Heche aamua kujisalimisha polisi



Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche amesema kesho ataripoti polisi mkoani Morogoro kuitikia wito wa jeshi hilo.

Heche alisema jana kuwa ana taarifa kwamba anatafutwa na jeshi hilo na anatakiwa kwenda kuhojiwa mkoani Morogoro.

Heche, pia alidai kuwa polisi walikuwa wamkamate, hata hivyo hilo halikufanyika.

Mbunge huyo alisema hajui kosa alilotenda, isipokuwa anatakiwa kuhojiwa kwa kauli alizotoa alipomsindikiza mbunge wa Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali kutoka gerezani.

Akizungumza na gazeti hili, kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema kwamba mbunge huyo alifanya mkutano wa hadhara wilayani Kilombero Aprili 8, 2017.

Alisema kwamba wanamtafuta kwa tuhuna za kutotii amri za viongozi na kufanya mkutano kisha kutoa lugha za matusi zilizotaka kusababisha vurugu.

Alisema tangu siku ya tukio, jeshi hilo limekuwa likimtafuta mbunge huyo bila mafanikio ndipo lilipoamua kulishirikisha Bunge.

Polisi iliandika barua kwa Spika wa Bunge kumtaarifu kuwa mbunge huyo anatafutwa kwenda kujibu tuhuma zinazomkabili mkoani Morogoro.

“Barua ni mambo ya siri kati ya jeshi na Bunge, tunachotaka sisi ni kumuona Heche hapa na asitake tutumie nguvu,” alisema Kamanda Matei.

Mwananchi: