Tuesday, 24 October 2017

Umoja wa Mataifa wataka Wapinzani waliokamatwa waachiwe...

Umoja wa mataifa umetoa wito ya kuachiwa mara moja kwa watu 30, wa chama kikuu cha upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutoka korokoroni.
Wanachama wa vyama vikuu viwili vya Union for Democracy na wenzao wa Social Progress, walikamatwa siku ya Jumapili katika mji wa Lubumbashi, ulioko Kusini mashariki mwa nchi hiyo, baada ya polisi kuvunja mkutano waliokuwa nao.
Utawala wa Rais, Joseph Kabila, umepiga marufuku mkutano wa aina yoyote wa kisiasa, pamoja na maandamano ya upinzani, tangu muda wake wa kuhudumu kama Rais kisheri, ulipomalizika mwaka mmoja uliopita.
Rais Joseph Kabila amesalia mamlakani hata baada ya muhula wake kuhudumu kumalizika mwaka mmoja uliopita
Tume ya uchaguzi nchini humo, imesema kuwa, haitakuwa rahisi kuandaa uchaguzi mkuu wa Urais, kabla ya mwezi Aprili mwaka ujao wa 2019.
Chama kingine cha upinzani- Union for the Congolese Nation, kimesema kwamba, kitajiondoa katika serikali ya ugawanaji mamlaka, kuhusiana na kucheleweshwa kwa uchaguzi mkuu.
Maandamano ya mara kwa mara ya upinzani nchini humo umekabiliwa vikali na utawala wa Rais Joseph Kabila.

Ronaldo Anyakua tuzo FIFA

England. Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa Fifa 2017 baada ya kuwapiku wachezaji Lionel Messi na Neymar katika kipengele hicho.
Tuzo hizo zimetolewa Oktoba 23 ambapo mchezaji huyo aliyeambatana na mpenzi wake na mwanae amewashukuru waliompigia kura kwa kuweza kushinda pamoja na mashabiki na wachezaji wenzake.
“Nashukuru wote mlionipigia kura kwa kunifanya nishinde tuzo hii,” amesema Ronaldo.
Mbali na tuzo hiyo Ronaldo ametajwa katika kikosi bora cha mwaka 2017 ambacho kimewajumuisha Messi na Neymar na nyota wengine akiwemo Sergio Ramos, Toni Kroos, Andres Iniesta, na Dani Alves.
Tuzo ya mchezaji bora wa kike wa Fifa 2017 ilienda kwa Lieke Martens ambaye hakuudhuria katika utoaji wa tuzo kutokana na kujiandaa na kujiandaa na mechi ya kufuzu kombe la dunia la wanawake.
Ukumbi ulilipuka kwa shangwe wakati linatangazwa goli bora la mwaka ‘Puskas’ ambapo katika magoli 10 bora mashabiki walisikika wakimtaja nyota wa Arsenal, Olivier Giroud ambaye alitangazwa kama mshindi.
Wengine walioshinda tuzo za Fifa 2017 ni Zinedine Zidane (Kocha bora kwa waume), Sarina Wiegman (kocha bora kwa wanawake) Gianluigi Buffon (Kipa bora), Mashabiki wa Celtic (Kikundi bora), Francis Kone (Mchezo wa kiungwana).

Mawaziri Na Wabunge Kuanza Kupewa Tuzo

Kamati ya utawala ya shindano la tuzo za utekelezaji maendeleo kwa kasi ya juu kwa Wabunge na Mawaziri (THSDA) imezindua shindano la kutoa tuzo kwa Wabunge na Mawaziri watakaofanya vizuri katika kutekeleza majukumu ya kuwaletea Wananchi maendeleo.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Kamati hiyo Bw. Wilson Maage alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, juu ya uzinduzi wa shindano hilo ambalo litafanyika kwa muda wa miezi miwili.
“Tuzo hizo zimetokana na kuwepo wazo bunifu (intellectual property) ambalo azma yake ni kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za huduma na maendeleo kwa wananchi wa Tanzania na kupima kasi ya utekelezaji wa shughuli hizo kwa viongozi wa ngazi mbalimbali katika sekta na taasisi za kiserikali hapa nchini,” alifafanua Maage.
Aliendelea kusema kuwa, vigezo vitakavyotumiwa katika kuteua viongozi hao ambao ni wabunge pamoja na Mawaziri ni pamoja na kuwa mtetezi wa Wananchi wake bila uoga akiwa ndani au nje ya Bunge, mtendaji bora wa maendeleo yenye kuonekana, sifa ya kutoa hoja zenye tija kwa kutumia lugha ya staha bila matusi, sifa ya utekelezaji wa haraka apatapo matatizo ya Wananchi wake pamoja na sifa ya kutetea demokrasia, uhuru na kutetea wanyonge.
“Faida za shindano la tuzo hizi ni kwamba zinaweka Wananchi karibu na viongozi, kuchochea utekelezaji huduma na maendeleo kwa kasi ya juu, utawla bora na uwajibikaji wa viongozi kwa Wananchi, uhusiano mzuri kati ya serikali na Wananchi na kuimarisha furaha, utulivu na amani,” alieleza Maage.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Kamati hiyo, Herman Mnenuka alisema kuwa Wananchi ndiyo nguzo kuu ya kupata kiongozi atakayepata tuzo hiyo kwani wao ndio watakaopendekeza majina ya wabunge pamoja na mawaziri wanaofaa kuwania tuzo hiyo.
Katika tuzo hiyo, hatua ya kwanza, wananchi wanapaswa kupendekeza wabunge 15 kwa kila kigezo shindanishi, pia Wananchi watawateua Mawaziri 5 kwa kila kipengele shindanishi kwaajili ya kuingia kwenye ushindani wa tuzo hiyo na wabunge watano na Mawaziri watatu watakaopata kura nyingi kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kwa wananchi wataingia katika fainali ya king’anyiro kuwania tuzo hiyo.
Aidha aliongeza kuwa, katika hatua nyingine, wananchi kupitia simu watawachuja washiriki waliofika hatua ya fainali kwa kutuma SMS na mbunge pamoja na waziri atakayepata kura nyingi ndiye atakaye kuwa mshindi katika kilele cha tuzo hiyo kitakachofanyika tarehe 23 Desemba Mwaka huu.
“Niwaombe wananchi washiriki kikamilifu ili kuweza kupata kiongozi anayejishughulisha na anayechapa kazi kupitia tuzo hii na mwisho wa kilele tutapata mshindi wa kila kipengele kilichowekwa ambacho kina tija muhimu katika taifa kupitia waheshimiwa wabunge na mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alieleza Mnenuka.
Aidha aliongeza kuwa, Wananchi watapendekeza majina kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu kupitia namba 15555 kwa mitandao ya Tigo, Airtel, Vodacom, Halotel Smart na Zantel na kila SMS itatozwa gharama ya shilingi 500 vilevile kutakuwa na vipindi vya radio runinga na magazeti ili kuwakumbusha mwenendo na hatua za shindano la tuzo za THSDA hadi siku ya kilele.
Hizi ni tuzo za kwanza kuandaliwa hapa nchini na kamati hiyo ambazo zitafanyika kwa awamu kulingana na upatikanaji wa rasilimali fedha.

Kizimbani kwa kutishia kumuua Diwani,,

WATU nane wakazi wa Ntyuka Manispaa ya Dodoma, wamefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Chamwino kwa tuhuma za kutishia kumuua kwa maneno Diwani wa Kata ya Ntyuka, Theobale Emmanuel.
Waliofikishwa kizimbani na kusomewa shtaka hilo ni Edward Lamoli, Edward Lauli, Petro Mjelwa, Yona Andrea, Lucas Mombo, Stephen Karashani, Zabron Leganga na Mussa Majana.
Kesi hiyo namba 234 ya mwaka 2017 inasikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo ya Chamwino, Zawadi Ndudumizi.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Ntyuka kinyume cha kifungu cha 89 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ambacho kilifanyiwa marejeo mwaka 2002.
 Hata hivyo, Washtakiwa wako nje kwa dhamana na kesi hiyo itasikilizwa tena Oktoba 24 mwaka huu.

Watumishi Wala rushwa Watangaziwa kiama

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni mstaafu George Mkuchika
Dar es Salaam. Serikali imesema mtumishi anayefanya kazi katika Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (Mkurabita) akibainika kushiriki vitendo vya rushwa atachukuliwa hatua mara moja.
Mkurabita ilianzishwa kwa lengo la kumsaidia anayemiliki ardhi kimila atambulike kisheria na apewe hati itakayomwezesha kupata mkopo ili aendeleze biashara.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni mstaafu George Mkuchika alitoa onyo hilo alipotembelea taasisi hiyo. Alisema asingependa kusikia kuna mwananchi anatafuta hati au wanataka eneo lake lipimwe lakini mtumishi wa Mkurabita anamweleza kuwa ili kazi yako iende haraka lazima ‘waonane’ jambo ambalo si sawa.
“Naomba muelewe, anayepambana na rushwa ni Rais mwenyewe kwa sababu Takukuru (Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa) ipo chini yake. Pia, Mkurabita ipo chini ya Ofisi ya Rais Ikulu.
“Maana yake Waziri wa Mkurabita ni Rais John Magufuli, mimi namsaidia kwa hiyo mnapofanya kazi hapa mjue mkuu wa nchi ndiyo mwenye wizara,” alisema Kapteni Mkuchika ambaye pia ni Mbunge wa Newala Mjini (CCM).
Mratibu wa Mkurabita, Seraphia Mgembe alisema licha ya mafanikio walionayo kuna changamoto ya kutopata fedha za kutosha ili kujiendesha. Alisema mwaka 2009 Mkurabita iliomba Sh43 bilioni kwa ajili kufanya shughuli zake kulingana na mpango kazi wao, lakini fedha walizopata hadi sasa ni asilimia 55 sawa na Sh23 bilioni.

TanzaniteOne: Wakubari kuingia makubaliano mapya

UONGOZI wa Kampuni ya uchimbaji madini aina ya tanzanite ya TanzaniteOne Mining Limited, umejitokeza na kutangaza wazi kuwa wako tayari kushirikiana na serikali katika kupitia upya makubaliano ya mkataba wa uchimbaji na kuhakikisha kuwa taifa linanufaika na vito hivyo.
“Wakati tunasubiri taratibu za serikali kukamilika kabla ya kuanza majadiliano, tunapenda kumhakikishia Mheshimiwa Rais John Magufuli na Watanzania kwa ujumla kwamba sisi kama TanzaniteOne tutatoa ushirikiano utakaowezesha kuwa na hitimisho lenye tija kwa taifa letu,” ilisema taarifa kutoka kwenye uongozi wa kampuni hiyo.
Taarifa hiyo rasmi kutoka Bodi ya Uongozi wa TanzaniteOne Limited iliyosainiwa na Katibu wa Kampuni, Kisaka Mnzava, inasema kuwa viongozi wake wako tayari kufuata maelekezo yoyote yatakayotolewa na serikali baada ya mazungumzo yanayotarajiwa kufanyika baina ya kampuni hiyo na serikali.
“TanzaniteOne iko tayari kuingia kwenye majadiliano na serikali kwa ajili ya kufanya mapitio ya mkataba husika pamoja na kurekebisha taratibu zote za uchimbaji na biashara ya madini nchini kwa manufaa ya Watanzania wote,” alifafanua Mnzava.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo rasmi, TanzaniteOne itashirikiana bega kwa bega na timu ya serikali itakayoundwa kwa ajili ya kutekeleza wajibu huo, lengo likiwa ni kuwezesha madini ya tanzanite yanayopatikana Tanzania peke yake, kuwa yenye manufaa kwa taifa.
“Tunafanya hivyo kwa sababu mbili: Kwanza ni kutambua juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli na hatua anazochukua kulinda rasilimali za taifa na kuhakikisha kuwa madini yanawanufaisha Watanzania wote kwa ujumla.”
“Pili tunaamini kuwa wabia wa kampuni ya TanzaniteOne, mbao ni Watanzania wazawa wana wajibu wa kushiriki katika mchakato mzima wa kuliwezesha taifa kunufaika na rasilimali za madini nchini,” waliongeza viongozi wa TanzaniteOne katika taarifa yao kutoka Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
TanzaniteOne Mining Limited ni kampuni ya ubia baina ya wafanyabiashara wa jijini Arusha, Hussein Gonga na Faisal Shahbhat kupitia Sky Associate wanaomiliki asilimia 50 za hisa na serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (Stamico) lenye hisa 50 pia.
Wakati wa ziara yake ya uzinduzi wa Barabara ya KIA-Mirerani, Septemba 27, mwaka huu, Rais Magufuli aliagiza kupitiwa upya mkataba wa uchimbaji na biashara ya madini hayo ya vito baina ya Sky Associate na Stamico.
Oktoba 19, mwaka huu, baada ya kushuhudia kutiwa saini makubaliano baada ya mazungumzo baina ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Barrick Gold Corporation, Rais Magufuli alimuagiza Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kwamba timu ya serikali ianze kufanyia kazi madini ya tanzanite na almasi.

Lulu Amwaga machozi Mahakamani


AUDIO | Peter Msechu _ Milele | Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/283959/by/NSQ
wwizCtY

AUDIO | Salamu TMK _ Nitarudi | Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/283963/by/lgEQX3xwej

Audio | Nameless _ Oh Why | Mp3 Download

Audio | Naneless _ Oh Why | Mp3 Download


https://my.notjustok.com/track/download/id/284047/by/4q6xc865zU

AUDIO | Darasa _ Shida | Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/284055/by/xvjreuFCap

Monday, 23 October 2017

Ubunifu wa Makonda waimarisha Jeshi la Polisi Dar es Salaam

Makonda akabidhi magari 18 kwa jeshi la polisi Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amekabidhi Magari ya kisasa 18 kati ya 26 yaliyopelekwa Mkoani Kilimanjaro yakiwa Mabovu kwa ajili ya kufufuliwa.
Magari hayo yalipelekwa Kilimanjaro yakiwa yamebebwa kutokana na ubovu lakini sasa yanarejea Dar es Salaam yakiwa mazima na mwonekano kama magari ya UN ambapo yatakuwa na uwezo wa kubeba Askari 11 wakiwa wamekaa na silaha zao.
Akikabidhi magari hayo kwa Jeshi la Polisi leo Makonda amesema yataenda kuhudumia wananchi kwa kuimarisha ulinzi na usalama jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa kilichomgusa kuboresha Jeshi la Polisi ni baada ya kuona askari wakifanya kazi katika mazingira magumu na wakati mwingine kuvamiwa na majambazi kisha kuuawa na kuporwa silaha.
Aidha Makonda ameishukuru kampuni ya Rajinder Motors Ltd (RSA) kwa kumuahidi kutengeneza magari 56 ya Polisi Dar es Salaam bila kutumia fedha za serikali. Makonda ametumia makabidhiano hayo kutuma salamu kwa majambazi, vibaka na wale wenye nia ya kuvuruga amani na usalama kuwa kiama chao kimefika.
Amesema alipotangaza mpango wa kufufua Magari yaliyokufa wapo waliombeza lakini sasa wanajionea magari yakiwa mapya. Makabidhiano hayo yameshuhudiwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mngwira, Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar ea Salaam Lazaro Mambosas na viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama ambapo wamempongeza Makonda kwa ubunifu mkubwa aliona

Waziri mkuu wa Japan kula sahani moja na Korea Kaskazini

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ameahidi kukabiliana vilivyo na Korea Kaskazini baada ya matokeo ya kwanza kuonyesha kuwa alipata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa siku ya Jumapili.
Bw. Abe alikuwa ameitisha uchaguzi wa mapema kwa ahadi ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili Japan, likiwemo tisho kutoka Korea Kaskazini.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa muungano wa Bw. Abe umeshinda theluthi mbili ya viti vya bunge.
Hii inampa Bw. Abe nafasi ya kuifanyia mabadiliko katiba ya baada ya vita vya pili vya dunia.
Awali waziri mkuu alikuwa ametoa wito wa kutaka jeshi la nchi lifanyiwe mabadiliko, hatua yenye utata ambayo anasema kuwa inahitajika kuboresha ulinzi wa jeshi la Japan.
Akizungumza baada ya kutolewa matokeo ya kwaza Bw. Abe alisema: "Jinsi nilivyoahidi lengo langu kubwa ni kuikabili Korea Kaskazini.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa muungano wa Bw. Abe umeshinda theluthi mbili ya viti vya bune.
Miezi miwili tu iliyopita umaarufu wake ulikuwa ukishuka kufuatia kupatikana kwenye sakata, lakini alipata mwamko mpya baada ya Korea Kaskazini kurusha makombora mawili kupitia anga ya Japan.
Vyombo vya habari viliripoti kuwa muungano wa chama tawala cha Abe cha Liberal Democratic Party (LDP) na chama cha Komeito ulishinda viti 312 kati ya viti 465 katika bunge la chini, ushindi unaoupa muungano huo nguvu za kubadilisha katiba.
Awali Bw. Abe alikuwa ametangaza kuwa alikuwa anataka kukifanyia mabadiliko kipengee cha katiba kinachozuia vita na kupelekea kutambuliwa kwa jeshi la Japan.
Miaka miwili iliyopita Bw Abe alifanikiwa kubadilisha katiba ambayo iliruhusu wanajeshi kupigana vita nje hatua ambayo ilipingwa vikali.