Thursday, 19 October 2017

Shehena ya bangi yaibuka kwenye ajali

Kibaha. Majeruhi wawili wa ajali ya gari wanashikiliwa na polisi mkoani Pwani wakituhumiwa kuhusika na usafirishaji na biashara ya bangi kilo 7,500.
Majeruhi hao ni Gudluck Kundaeli maarufu Mbowe (24) mkazi wa Kiwalani na Ally Gebra maarufu Mtena (28) wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jonathan Shanna amesema leo Alhamisi Oktoba 19,2017 kuwa watuhumiwa walikamatwa jana eneo la Kwa Mathias mjini Kibaha baada ya upekuzi kufanyika kwenye gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota IST lililopata ajali.
Amesema gari hilo lilipata ajali eneo hilo saa tatu usiku na askari walifika kutoa msaada ikiwemo kuwaokoa majeruhi ambao walipelekwa Hospitali ya Tumbi kwa matibabu.
Kamanda Shanna amesema baada ya kuwaokoa majeruhi na askari kufanya upekuzi kwenye gari walikuta magunia saba yenye bangi.
"Tulipata taarifa ya ajali kutokea eneo la Kwa Mathias, askari wakaenda kwa ajili ya uokoaji na waliwaokoa vijana hawa. Baadaye walifanya upekuzi kwenye gari na kukuta bangi hiyo. Tumepima ina kilogramu 7,500 kwa hiyo tunawashikilia watusaidie katika uchunguzi," amesema Kamanda Shanna.

Kauli ya Ridhiwani kikwete kuhusu Tundu Lissu,,,,

Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete amefunguka na kusema kuwa amefurahi kumuona Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akiwa mwenye tabasamu na furaha na kuzidi kumuombea apone kabisa na kurudi kupambana.
Ridhiwani Kikwete amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram na kusema Mungu siku zote anatenda wema kwa watu kufuata kushambuliwa kwa risasi nyingi Tundu Lissu na hatimaye kuweza kupona na sasa furaha yake kuanza kurejea.
"Mungu utenda wema siku zote. Ashukuliwe yeye kwa kazi ya kurejesha tabasamu katika sura yako na afya kwa wanaokuuguza. Nimefurahi kukuona tena msomi, Kiongozi wangu na mwana kamati mwenzangu wa Bunge ukitabasamu na mwenye Afya njema. Mungu akulinde na akusimamie katika matibabu yako .Looking forward to see you back into your good shape" aliandika Ridhiwani Kikwete
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mnamo Septemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake mjini Dodoma na kisha baadaye kusafirishwa na kupelekwa jijini Nairobi Kenya kwa matibabu ambapo mpaka sasa yupo nchini Kenya akiendelea kupatiwa matibabu

CHADEMA Waliamsha Dude

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeweka wazi kwamba hakimuhitaji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bw. Christopher Kazeri kuwa msimamizi wa uchaguzi mdogo kwa madai hawana imani naye pia hana sifa kwani anaweza kusababisha umwagikaji wa damu.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeweka wazi kwamba hakimuhitaji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Bwana Christopher Kazeri kuwa msimamizi wa uchaguzi mdogo kwa madai kwamba hawana imani naye pia hana sifa kwani anaweza kusababisha umwagikaji wa damu.
Akiitoa taarifa hiyo Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini Amani Golugwa amesema kwamba Mkurugenzi huyo alipoteza sifa za kusimamia uchaguzi tangu Juni, 24 walipokuwa kwenye uchaguzi wa vitongoji na vijiji kwa kufoji matokeo katika vijiji kadhaa na kuwalazimisha wasimamizi wabadilishe namba kwenye fomu.
Golugwa amesema kwamba vitendo ambavyo Mkurugenzi huyo alivifanya anavitafsiri kama mambo ya kihuni kwani yalipelekea kugombanisha watu ambao ni ndugu hivyo hofu yao ni kwamba anaweza kusababisha umwagikaji damu katika uchaguzi mdogo wa marudiano Arumeru Mashariki.
"Tumeishauri Tume iweze kuwasiliana na mamlaka ya uteuzi kwamba hatumtaki ndg Kazeri awe msimamizi wa uchaguzi huu mdogo Arumeru Mashariki, kwanza aliingilia uchaguzi wa vitongoji na vijiji na kulazimisha kubadilishwa matokeo ambayo yalionyesha Chadema wameshinda, jambo ambalo lilileta ugombanishi kwa wagombea, na hata wagombea wa CCM walikataa matokeo kwa kukubali kwamba walishindwa na hata wasimamizi na askari waliokuwepo hapo walithibitisha kwamba Chadema walikuwa wameshindwa" Golugwa
Ameongeza "Kama uchaguzi wa vitongoji Mkurugenzi ametumia mabavu na kufanya uhuni ambao tumeumbatanisha kwa Tume, kwenye uchaguzi huu wa madiwani si ataleta hata vifaru au kusababisha umwagaji wa damu? Kwa busara na hekima ya kawaida matendo aliyoyafanya Kazeri hayampi sifa ya kuwa msimamizi.
Hata hivyo Golugwa amefafanua na kusema kwamba wamewasilisha ushahidi wa wagombea wa CCM wakikataa kupokea ushindi huo wa vitongoji kwa madai kwamba hawawez kupokea ushindi wa mtutu wa bunduki.

Mwigamba avuta 'jeshi' kujiunga CCM

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba na wanachama wengine 10 wametangaza kujiunga na chama cha CCM baada ya kujivua uanachama wa ACT Wazalendo leo.
Taarifa za Mwigamba kujiunga na CCM zimetolewa leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, na kusema kwamba wameamua kufanya hivyo ili kujitenga na upinzani unaokerwa na maendeleo ya nchi, na pia kuunga mkono juhudi za serikali za mapambano dhidi ya rushwa.
“CCM ya sasa ndicho chama kinachotekeleza kwa karibu itikadi, falsafa na sera za ACT Wazalendo ambazo mimi na wenzangu tulishiriki kukiasisi, nchi yetu ndio kinara wa mapambano dhidi ya rus
hwa sasa hivi, sera ambazo ndio misingi ya ACT Wazalendo, tumeamua kujitenga na upinzani unaokerwa na mafanikio ya nchi ili tuendelee kuwa sehemu ya mapambano katika kurejesha nchi kwenye misingi yake”, amesema Mwigamba.
Samson Mwigamba atakuwa kiongozi wa pili ACT Wazalendo kujivua uanachama wa ACT Wazalendo kwa mwaka huu baada ya Prof. Kitila Mkumbo ambaye naye alifanya hivyo wiki kadhaa zilizopita.

Nafasi za kazi Leo 19

Bonyeza Links Zifuatazo Kusoma zaidi na Kuapply
Nafasi zingine ingia Nafasi za kazi leo October 19
2 Job Opportunities at Vodacom Tanzania
Job Opportunity at Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA)
Job Opportunity at Alliance for a Green Revolution in (AGRA), Finance & Administration Officer
Job Opportunity at Multinational
Bank, Branch Manager
Job Opportunity at TAPBDS CO LTD, Accountant
Job Opportunity at The Belgian Red Cross, Regional Cash Delegate, Tanzania
Job Opportunity at EngenderHealth Tanzania, Research Coordination Advisor
Job Opportunity at NMB Tanzania, Senior Manager Branch Technology Support
Job Opportunity at ILO, Technical Officer
www.ajirayako.co.tz

Picha ya faru aliyeuawa yashinda tuzo ya picha bora

Picha ya kutisha ya uhalifu wa mazingira imetangazwa kuwa mshindi katika tuzo za shindano la wapiga picha la mwaka huu
Picha ya kutisha ya uhalifu wa mazingira imetangazwa kuwa mshindi katika tuzo za shindano la wapiga picha la mwaka huu.
Picha hiyo iliopigwa na mpiga picha wa Afrika Kusini Brent Stirton inaoyesha hali ya faru mweusi katika mbuga ya wanyama pori ya Hluhluwe Imfolozi.
Wawindaji haramu walimuua mnyama huyo usiku kabla ya kumtoa pembe zake.
Stirton alipiga picha hiyo ikiwa miongoni mwa uchunguzi kuhusu biashara haramu ya bidhaa za faru.
Mpiga picha huyo alizuru zaidi ya maeneo 30 uliofanyika uhalifu huo wakati wa uchunguzi wake ambao aliutaja kuwa wa kuogofya.
Mwanangu wa kwanza atazaliwa mnamo mwezi Februari ; nina umri wa miaka 48. Unaweza kupoteza utu mara nyengine.
Stirton, ambaye alipokea tuzo hiyo katika tamasha la chakula cha jioni lililofanyika katika jumba la kumbukumbu mjini London , anaamini kwamba unyama huo aliofanyiwa faru huyo ulitekelezwa na wakaazi wa eneo hilo.
Lengo kubwa la uwindaji huo ni kuuza pembe mbili za faru huyo kwa wafanyibiashara.
Wafanyibiashara hao baadaye huzipeleka pembe hizo hadi Afrika Kusini kupitia Msumbiji hadi China ama hata Vietnam.
Katika mataifa hayo ya bara Asia, pembe za faru zina thamani ya juu ikilinganishwa na dhahabu ama dawa ya kulevya ya Cocaine.
Biashara hiyo hupata msukumo wa imani kwamba sawa na kucha za vidole vya mguuni, zinaweza kutibu ugonjwa wowote kutoka saratani hadi mawe ya figo.
Brent Stirton aliambia BBC : Kwa mimi kushinda tuzo hii, kwa majaii kuweza kutambua kazi yangu ni wazi kwamba tunaishi katika muda tofauti na kwamba hili ni swala nyeti.
''Swala la kuangamia kwa baadhi ya wanyama ni la kweli na faru ni mojawapo ya aina ya wanyama wanaoendelea kuangamia kwa kiwango kikubwa na ninashukuru kwamba majaji waliweza kutambua picha yangu kwa kuwa inaliangazia swala hili kwa hatua nyengine''.
Lewis Blackwell, mwenyekiti wa jopo la majaji hao wa WPY, alisema kuwa picha hiyo ya faru ilikuwa na athari kubwa katika jopo lake.
''Watu wanaweza kusinywa ama kushtushwa lakini ukweli ni kwamba picha hiyo inakuvutia na kukufanya kuhisi kana kwamba unataka kujifunza mengi.Unataka kujua habari kuihusu. Na huwezi kuitoroka kwa sababu inakuangazia yale yanayoendelea duniani''.

MAGAZETI YA LEO 19/10/2017














AUDIO | Rayvanny _ Tabia | Np3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/282350/by/nUXzBDbVsZ

Msami afunguka ishu ya kutoka na Nandy Kimapenzi

Msanii wa Bongo Flava, Msamii amesema si kweli kwamba ameshawahi kutoka kimapenzi na Nandy.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma katika mahojiano na Bongo5 amesema Nandy ni kama dada yake hivyo hawezi kufanya hivyo.
“Nandy sijawahi kupita naye ni kama mdogo wangu, dada yangu, kwa hiyo kwa sasa hivi mimi na Nandy ni kaka na dada, let say mimi ni mtu ambaye nimetoka kwenye familia ya THT Nandy pia kwenye familia hiyo hiyo, tupo familia moja” amesema Msami.
Msami anaungana na rapper Bill Nass ambaye amekuwa akidaiwa kuwa na mahusiano na Nandy kitu ambacho amekuwa akikikanusha kila mara.

Wema Afunguka sababu za kutokwenda kumuona lissu Nairobi

Mrembo wa Tanzania na Kada wa Chadema Wema Sepetu ametoa ya Moyoni kwa nini hakwenda kumuona mapema Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi septemba 7 ni kwamba asingeweza kumuona akiwa kwenye maumivu.
Wema ameweka wazi maneno hayo kwenye ukurasa wake wa Instagram ikiwa ni baada ya dakika chache tangu kuachiwa kwa picha za kwanza za Mbunge huyo akiwa hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Wema ameandika "Kisichokuua kinakufanya uwe na nguvuz zaidi....Utarudi tena ukiwa na nguvu kuliko ulivyokuwa awali...Shujaa wetu. ... Picha hii imenifanya nipate hisia. Sasa naweza andaa safari ya Nairobi kuja kukuona.. Awali nisingeweza kuvumilia kukuona ukiwa kwenye maumivu".
Wema Sepetu ametajwa na Chama cha Chadema kama mmoja wa wahamasishaji aliyeweza kuhamasisha watu kutoa michango kwa ajili ya matibabu ya Mbunge Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa kwenye gari lake nje ya makazi yuke huko mjini Dodoma.

Beka Flavour : Siwezi kurudi yamoto band,,

Msanii wa Bongo Fleva, Beka Flavour amefunguka na kusema kuwa yeye kwa sasa hayupo tayari kurudi kwenye kundi la Yamoto Band na kudai ukweli ni kwamba kundi hili lilishakufa na kila msanii sasa anasimama kivyake.
Beka alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet bongo na kusema kuwa wakati wanaondoka kwenye kundi hilo hawakuwa na pesa zozote zile kwani enzi zao wakati wanafanya show mbalimbali walikuwa wanapewa fedha za matumizi tu na wao walipendekeza kwa uongozi fedha zinapopatikana wafanyiwe mambo kadhaa ikiwa pamoja na kujengewe nyumba.
"Mimi saizi ukisema nitoke kwenye uongozi wangu mpya nirudi Yamoto Band sidhani kama itawezekana unajua watu hawajui tu lile kundi ndiyo limeshakufa kwa sababu saizi kila msanii yupo na uongozi wake, sidhani kama wanaweza kukubaliana watoke walipo na kurudi kule" alisema Beka Flavour
Mbali na hilo msanii huyo aliweka wazi kuwa anafurahi kuona Aslay msanii ambaye alikuwa naye kwenye kundi moja na yeye saizi anakuwa ni kati ya wasanii wanaozungumziwa sana kwa kazi nzuri.
"Mimi nazidi kumuombea kwani mwenzangu saizi amekuwa ni kati ya wasanii ambao wanazungumziwa sana kutokana na kazi zake, lakini napenda kuwaambia Watanzania kuwa wasanii ambao tulikuwa tunaunda kundi la Yamoto Band Mungu alitupa kitu ndani yetu hivyo muda si mrefu mtakuja kuona haya nayosema kwani kila mmoja ana upekee wake katika kazi zake" alisisitiza Beka

Wednesday, 18 October 2017

Simbaye : sekta binafsi Hali tete,,,,,

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Bwana Godfrey Simbeye, amesema sekta binafsi sasa hivi zinapitia kwenye wakati mgumu kutokana na kodi ambazo TRA wameziweka, kitu ambacho kinaweka mazingira magumu ya kazi za uzalishaji.
Bwana Simbeye ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba licha ya serikali kuweka jitihada zake za kuimarisha sekta hizo, lakini kumekuwa na changamoto kubwa inakuja kwenye utaratibu usiofaa wa ukasanyaji kodi.
“Serikali kwa juhudi zake imeendelea kutengeneza mazingira mazuri ya biashara, kama kurekebisha njia za usafirishaji ikiwemo reli na viwanja vya ndege, lakini suala la kodi limekuwa ni tatizo, malalamiko mengi ya sekta binafsi yanatoka kwa namna ambavyo TRA wanakusanya kodi, ni kero kubwa, imekuwa kwa mwezi mmoja taasisi binafsi inaweza ikatembelewa na timu ya TRA tatu na zote zikaja na makadirio tofauti, kwa hiyo hilo suala tunatakiwa tuliangalie”, amesema Bwana Simbeye.
Bwana Simbeye ameendelea kwa kusema kwamba changamoto nyingine ambazo sekta binafsi zinapitia kwenye kipindi hiki ambacho uwekezaji unakua, ni pamoja na kukosa mikopo, kutokana na hali ya mabenki ilivyo kwa sasa.
“Uwekezaji mpya unakua Tanzania, hata kwenye kituo cha uwekezaji project mpya zimeongeneka, lakini uwekezaji wa ndani bado haujakuwa sana kwa sababu hali ya kukopesha kwenye sekta binafsi bado haijawa nzuri, bado hatujaona dalili nzuri ya ukopeshaji wa mabenki kwenda sekta binafsi, ingawa serikali imekuwa ikiendelea kutoa dhamana ya serikali, lakini kwa upande wa sekta binafsi bado”, amesema Bwana Simbeye.

TAKUKURU Yawahoji Madiwani Waliojihuzulu CHADEMA

Maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutoka makao makuu jijini Dar es Salaam, wamewahoji kwa zaidi ya saa sita, madiwani waliojiuzulu Chadema wanaotuhumiwa na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kuwa walipewa rushwa.
Waliofika Takukuru ni Catherine Mtui, aliyekuwa diwani wa viti maalumu, Japhet Jackson (aliyekuwa diwani wa Ambuleni) na Bryson Isangya (aliyekuwa diwani wa Maroroni). Baada ya kuhojiwa hawakutaka kuzungumza chochote wakisema wanaacha uchunguzi uendelee.
Pamoja nao, diwani wa Mbuguni, Ahimidiwe Rico anayedaiwa kuwa ndiye alirekodi sauti na picha wakati akishawishiwa na viongozi wa Serikali na wa Halmashauri ya Meru amehojiwa kwa zaidi ya saa tatu jana Jumanne Oktoba 17, 2017.
Rico amesema amewaeleza Takukuru kila kitu ambacho anakifahamu katika sakata hilo, ikiwemo kuwarekodi viongozi ambao walimshawishi kujiuzuru udiwani.
"Msimamo wangu ni kwamba, nachukia rushwa. Nimewaeleza kila kitu na wao waliniuliza kuhusu vifaa nilivyotumia kuwarekodi nikawaambia ni mali ya mbunge, alivitoa nchini Uingereza," alisema.
Rico aliyesindikizwa na diwani wa Nkwanankore, Wilson Nanyaro amesema ana imani na Takukuru kwamba watafanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua.
"Nimewaeleza wazi kuwa hata shauri hili likienda mahakamani nipo tayari kwenda kutoa ushahidi na kuthibitisha sauti za watu ambao niliwarekodi," alisema.
Alisema baada ya mahojiano yaliyoanza saa tatu hadi saa sita mchana, maofisa wa Takukuru walimwambia aondoke na watamuita watakapomuhitaji.
Hakuna ofisa wa Takukuru aliyekuwa tayari kuzungumzia mahojiano hao wakisema wasemaji ni makao makuu ya ofisi hiyo Dar yaliyoko jijini Dar es Salaam.