Saturday, 14 October 2017

Yanga kamili kuivaa kagera sugar ,,,,

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, George Lwandamina amethibitisha kuwa kikosi chake kipo tayari kuivaa Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara VPL leo jioni kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Akizungumza katika mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo, Lwandamina amesema wachezaji wake wote wapo vizuri kuivaa Kagera ambayo itakuwa nyumbani.
Pamoja na kuwakosa wachezaji wake watatu, kiungo Thabani Kamusoko, mshambuliaji Donald Ngoma na mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe lakini bado Lwandamina ana imani na wachezaji wengine waliopo kwenye kikosi chake.
“Timu yetu inawakosa Tambwe, Ngoma na Kamusoko, lakini bado timu yetu ina kikosi cha kutosha na nina imani na wachezaji wote wanaweza kufanya vizuri,”amesema Lwandamina.
Ukiacha mchezo wa Yanga, Ligi Kuu itaendelea leo kwa mechi zingine nne ambapo Mwadui FC wataikaribisha Azam FC Uwanja wa Mwadui Complex, Ndanda watawakaribisha Maji Maji ya Songea, wakati Singida United itacheza na wenyeji Ruvu Shooting ya Pwani.
Njombe Mji na Lipuli ya Iringa watacheza kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe

Breaking News: Marekani yasikitishwa na Hatua ya Odinga

Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani imesema inaheshimu lakini inajutia uamuzi wa kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, kujiondoa kwenye Uchaguzi mpya wa urais tarehe 26 mwezi huu.
Hata hivyo, Marekani imeendelea kusisitiza kuwa, itaendelea kushinikiza kuwepo kwa Uchaguzi utakaokuwa huru na haki.
Afisa wa juu katika Wizara hiyo ameliambia Gazeti la Daily Nation kuwa, pamoja na hilo Odinga anakaribishwa nchini Marekani.
Taarifa hii imekuja baada ya kuwepo kwa madai kuwa Odinga amenyimwa Visa ya kwenda Marekani.
Marekani imesema hakuna kinachomzuia Odinga kuja nchini Marekani wakati wowote anaotaka.
Kwa sasa Odinga yupo jijini London nchini Uingereza, anakotoa midhahara ya kisiasa na kukutana na viongozi mbalimbali

Video : Diamond Platnumz Alivyokinukisha Uganda,,,,,,


Kocha Lwandamina: Vijana wapo tayari kwa kuipigania Yanga kesho

KOCHA wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amesema kwamba wachezaji wake wako vizuri kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Akizungumza baada ya mazoezi ya jioni Uwanja wa Kaitaba, Lwandamina amesema wachezaji wake wote wapo vizuri kuelekea mchezo huo kesho jioni.
Lwandamina amesema japokuwa atawakosa wachezaji wake watatu tegemeo, Wazimbabwe kiungo Thabani Kamusoko, mshambuliaji Donald Ngoma na mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe - lakini hana shaka vijana waliopo watafanya vizuri.
“Tutawakosa Kamusoko, Ngoma na Tambwe, lakini nina imani na wachezaji niliokuja nao hapa wanaweza kufanya vizuri,”amesema.
Kwa ujumla, Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho na mbali na mabingwa hao watetezi, Yanga kuwa wageni wa Kagera Sugar, Mwadui FC wataikaribisha Azam FC Uwanja wa Mwadui Complex,
Shinyanga na Ndanda watawakaribisha jirani zao, Maji Maji ya Songea Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati Singida United itasafiri hadi Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi kucheza na wenyeji Ruvu Shooting ya Pwani.
Majirani wengine, Njombe Mji na Lipuli ya Iringa watacheza kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe ilihali michezo mingine ya Ligi hiyo ikifanyika Jumapili Oktoba 15, ambako Simba itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Tanzania Prisons itacheza na Stand United kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Friday, 13 October 2017

Audio | Sarge Beynaud_ Matta Swaga | Mp3 Download

https://cloudup.com/files/iAoSJUP3zk7/download

Nafasi Za Kazi Leo October 13,

Bonyeza Links zifuatazo kusoma na kuapply:
Nafasi zingine ingia Nafasi za kazi leo October 13
6 Job Opportunities at TPB Bank PLC, Sales Executives
17 Jobs at Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI)
Paid Internship Abroad Job Opportunities, AIESEC in Tanzania
Job Opportunity at Pestalozzi Children’s Foundation (PCF), Education Officer
Job Opportunity at Dalberg, Global Manager Training Program
Job Opportunity at Nokia Tanzania, Engineer
Job Opportunity at Radar Recruitment, Operations
Job Opportunity at MeTL , Processing Operator
www.ajirayako.co.tz

Jeshi la polisi latoa onyo kwa viongozi Wa magroup ya whatsapp

Dar es Salaam. Jeshi la polisi kitengo cha makosa ya mtandaoni limewatahadharisha viongozi wa makundi ya What's App na kuwataka kutoa taarifa pindi uhalifu unapofanyika kwenye makundi yao.
Kufanya hivyo kutasaidia polisi kuchukua hatua dhidi ya mhusika aliyefanya uhalifu huo ili kukabiliana na ongezeko la vitendo vya uhalifu mtandaoni.
Hayo yameelezwa leo Ijumaa na naibu mkuu wa kitendo hicho, Joshua Mwangasa wakati wa semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) na kuwakutanisha viongozi wa dini wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema makosa ya kimtandao yameendelea kuongezeka kwa kasi kubwa huku makundi ya What's App yakionekana kuwa kichocheo kikubwa.
Mwangasa amesema viongozi wa makundi hayo hawatakiwi kuvumilia makosa hayo hivyo wanatakiwa watoe taarifa polisi.
"Usikubali umeanzisha kundi kwa nia nyingine halafu mtu au watu wanaweka mambo yasiyofaa, toa taarifa hatua zichukuliwe kinyume na hapo hata wewe utahusika,"
Amesema kwa kiasi kikubwa makundi hayo yamekuwa yakitumika kusambaza taarifa za uongo na uchochezi.
Mwangasa ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kuwahubiria waumini wao juu ya matumizi sahihi ya mitandao ili kujiweka mbali na uhalifu.
"Ukosefu wa maadili ndio unachangia haya yote haya, ndiyo sababu narudi kwenu viongozi wa dini wasisitizeni waumini wenu watumie mitandao kwa maendeleo," amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema mamlaka hiyo inaendelea kuchukua hatua kuimarisha ulinzi wa mawasiliano mtandaoni.
Amesema simu za mkononi kwa sasa zimekuwa kama silaha hivyo matumizi yake yanapaswa kuangaliwa kwa umakini zaidi.

Ndege ya Uturuki yatua Kwa dharula pwani ya kenya

Ndege ya Uturuki yatua kwa ghafla katika uwanja wa ndege wa Moi mjini Mombasa Kenya
Ndege moja ya kampuni ya ndege ya Uturuki Turkish Airlines iliokuwa ikibeba abiria 121 na wafanyikazi sita ilitua kwa dharura nchini Kenya siku ya Ijumaa alfajiri baada ya mojawapo ya injini zake kuingiwa na ndege, kulingana na polisi.
Ndege hiyo aina ya TK673 ilikuwa ikiondoka katika mji huo wa pwani ya Kenya ikielekea Istanbul wakati ndege huyo alipoingia katika injini yake mwendo wa saa 10 alfajiri .
Ilibidi ndege hiyo izunguke katika anga ya mombasa kwa takriban saa moja ili kumaliza mafuta yake kabla ya kutua kwa dharura.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Ndege hiyo ilichunguzwa na mafundi kabla ya kuondoka.

Marekani na Israel zajiondoa katika UNESCO

Marekani na Israel zimetangaza kujiondoa kutoka shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO zikidai Israel inabaguliwa.
Wizara ya mambo ya kigeni ilisema kuwa itabuni ujumbe wa waangalizi kwenye shirika hilo lenye makao yake nchini Ufaransa kuchukua mahala pa uwakilishi wake.
Mkuu wa Unesco Irina Bokova, amesema amesikitishwa lakini hajashangazwa.
Tangu wakati wa kampeni zake Trump alikuwa akitoa matamshi ya kuubeza Umoja wa mataifa na pia kulalamika kwamba Marekani ndio inayochangia fedha nyingi zaidi, hivyo kukariri kwamba atapunguza mchango wake.
Mwaka 2011 Marekani ilifuta bajeti yake kwa Unesco kupinga hatua yake ya kuwapa Wapalestina uanachama kamili.
Marekani hutoa asilimia 22 ya bajeti ya kawaida ya Umoja wa Mataifa na asilimia 28 kwa shughuli za amani za Umoja wa Mataifa.
Unesco iko katika mikakati ya kumteua kiongozi mpya huku mawaziri wa zamani wa Qatari na Ufaransa, Hamad bin Abdulaziz al-Kawari na Audrey Azoulay wakiwa mstari wa mbele katika ushindani huo wa ni nani atachukua mahala pake bi Bokova

ACACIA waendelea kulia na makinikia..wadai yanawatia hasara

Ikitarajia kuchapisha hesabu zake za fedha kwa robo ya tatu ya mwaka, kampuni ya Acacia inaendelea kuugulia maumivu ya zuio la kutosafirisha mchanga wa madini.
Kwenye taarifa yake ya awali iliyotolewa jana kwa wadau wake na jamii kwa ujumla, kampuni hiyo imeeleza kuimarika kwa uzalishaji lakini ikabainisha kupungua kwa mapato kutokana na zuio hilo lililoanza mapema Machi.
“Mauzo yalikuwa madogo kutokana na zuio la kusafirisha makinikia yanayozalishwa kwenye migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi nchini Tanzania,” inasema taarifa hiyo fupi.
Machi, Serikali ilizuia usafirishaji wa mchanga wa madini na Rais John Magufuli akaunda kamati mbili za kuchunguza uchimbaji, usafirishaji na biashara nzima ya dhahabu ambazo zilibaini udanganyifu unaofanywa hivyo kulinyima Taifa mapato linayostahili.
Licha ya zuio hilo, Serikali ilifanya mabadiliko kwenye sheria za madini ili kuongeza usimamizi wa uzalishaji, udhibiti wa mapato na ushiriki wa Watanzania katika umiliki wa kampuni zenye vibali vya uchimbaji nchini.
Kwa robo nzima ya mwaka, kampuni hiyo inayomilikiwa na Barrick Gold Corporation kwa asilimia 63.9 imezalisha wakia 191,203 na kuuza wakia 132,787. Pamoja na takwimu hizo, changamoto za upatikanaji wa vibali na kupunguzwa kwa uzalishaji kwenye baadhi ya migodi yake kumeathiri kiasi cha dhahabu iliyopatikana.
Vibali viliathiri uzalishaji wa Mgodi wa North Mara ambao umetoa wakia 72,011 ndani ya miezi mitatu ya Julai, Agosti na Septemba wakati Mgodi wa Bulyanhulu ukizalisha wakia 50,094 kutokana na kupunguza operesheni zake.
“Uzalishaji umezidi matarajio katika Mgodi wa Buzwagi uliochangiwa na ubora dhahabu iliyopatikana. Tulizalisha wakia 69,097,” inasomeka taarifa hiyo.
Kuanzia Julai 31, mazungumzo baina ya Serikali na Barrick yanaendelea kutafuta muafaka wa zuio hilo pamoja na kuongeza faida kwa kila upande. Miongoni mwa yanayojadiliwa kwenye mazungumzo hayo ni faini ya Dola 190 bilioni za Marekani (zaidi ya Sh424 trilioni) ambayo Acacia imeandikiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) ikiwa ni kodi iliyokwepwa pamoja na riba yake.
Tangu kuanza kutekelezwa kwa zuio hilo, bei ya hisa za kampuni hiyo iliyoorodheshwa Soko la Hisa London (LSE) na Dar es Salaam (DSE) imeshuka kutoka Sh12,000 mpaka Sh5,000 kila moja.

Audio | chin beez Ft kaligraph jones _ Kababayee Remix | Mp3 Download

Bovya hapa kudownload.....
https://cloudup.com/files/iJSBNBKQTq0/download

Audio | Lee1 Ft Side kichwa – Sina Raha | Mp3 Downloa

Audio | Lee1 Ft Side kichwa – Sina Raha | Mp3 Download

Bovya hapa kidownload....
https://cloudup.com/files/iXQeCKcdRvn/download

Audio | Chidinma_Live and Die In Africa | mp3 Download

https://cloudup.com/files/iu6P0VNDJ8v/download