Benki Kuu ya Tanzania imetoa gawio la Shilingi Bilioni 300 kwa Serikali kutokana na faida iliyopatikana kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Taarifa iliyotolewa na Benki Kuu imesema kwamba gawio hilo kutoka benki kuu kwenda kwa Serkali linafikisha jumla ya Bil 780 kwa kipindi cha miaka mitatu (2014/2015- 2016-2017)
Hata hivyo taarifa hiyo imewekwa wazi kwamba majukumu ya msingi ya Benki Kuu siyo kutengeneza faida na inapotokea faida imepatikana , sehemu kubwa hutolewa kama gawio kwa serikali.
No comments:
Post a Comment