Familia ya watoto wanne wakiongozwa na mama yao mzazi Julieta Majaliwa wamelazimika kufukua kaburi la baba yao Stanford Gombo, wakidai kuwa na mashaka na sababu ya kifo cha baba yao.
Tukio hilo limetokea huko katika cha kijiji cha Kilimani wilayani Gairo mkoani Morogoro ikiwa ni utekelezaji wa amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani humo baada ya familia hiyo kutaka mwili huo kufanyiwa uchunguzi.
Wanafamilia hao walifika kijijini hapo wakiwa na ulinzi wa polisi kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa amri ya mahakama inayoelekeza kufukuliwa kwa kaburi hilo, ili watoto wapate nafasi ya kuhakiki mwili uliozikwa kama ni wa baba yao pamoja na kufanyiwa uchunguzi kubaini sababu zilizopelekea kifo chake.
Kwa upande wake Mke wa marehemu ,Bi. Julieta Majaliwa amesema mara ya mwisho kuwasiliana na mumewe walikua nyumbani kwao jijini Dar es salaam ambapo alimuaga anaenda kijiji kwao kuwajulia hali lakini tangu alivyo ondoka hawa kuwa na mawasiliano hadi kifo chake.
No comments:
Post a Comment