Tuesday, 26 December 2017

Aliyemlawiti Mtoto Tarime Matatani



Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya, linamshikilia Said Selemani 30-40 mkazi wa Mtaa wa Kebasa Halmashauri ya Mji Tarime mkoani Mara kwa tuhuma za kulawiti mtoto wa miaka minne.
Kamanda mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya, Henery Mwaibambe, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa amefunguliwa shtaka kituoni hapo namba TAR/IR/5034/2017 na kuwa atafikishwa mahakamani baada ya
upelelezi kukamilika.
Aidha, Kamanda huyo aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo anatarajia kupelekwa mahakamani kesho ili kujibu shtaka linalomkabili kwa kuongeza kuwa mtuhumiwa huyo pia amatuhumiwa kumsababishia maumivu makali mtoto huyo.
Akizungumzia tukio hilo nyumbani kwake, mama mzazi wa mtoto huyo (jina limehifadhiwa), amesema tukio hilo lilibainika Disemba 14, 2017 wakati mtoto aliposhindwa kula na kuanza kuharisha mara kwa mara.
“Kugundua kuwa mtoto wangu ameathirika na kitendo hicho ni baada ya kuwa ameshindwa kula huku akiwa anaharisha mara kwa mara, kitendo ambacho kilinishtua moyo wangu na mtoto hakuwa na dalili ya kuugua ikabidi nianze kufanya ufuatiliaji wa kina ili kujua kilichompata,” alisema.
Ameongeza kuwa tukio hilo amelipokea kwa masikitiko makubwa na kuwa hakuwa na habari kuwa mwanaye wa miaka minne anaweza kutendewa kitendo cha kinyama kiasi hicho na mtuhumiwa ambaye ni mpangaji mwenzake.
Akizidi kufafanua, amesema kuwa baada ya kugundua mwanaye amekuwa akilawitiwa mara nyingi kwa nyakati tofauti, alichukua hatua za kwenda kwa wataalamu ili kuchukuliwa vipimo kwa ajili ya kijiridhisha.
“Hatua nilizochukua baada ya kugundulika kuwa mwanangu alikuwa ameathirika kwa muda mrefu ni kwenda kituoni polisi ili kutoa taarifa kwa hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya mtuhumiwa,”alisema mama huyo..
”Baada ya kwenda polisi ilibidi twende hospitalini kwa uchunguzi ambapo daktari alisema hakuona dalili zozote ila nikasema kuwa haiwezekani kuna mchezo unafanywa, andipo niliomba kwenda Bugando kwa uchunguzi zaidi ambapo polisi walitoa askari wa kwenda kujiridhisha,” aliongeza.
Alibainisha wakati wakiwa Bugando, daktari aliyemfanyia vipimo alisema mtoto huyo amelewitiwa mara nyingi zaidi ya mwaka mmoja.

No comments:

Post a Comment