Thursday, 18 January 2018

Anusurika Kifo akipambana na Mamba kwa zaidi ya saa moja


MKAZI wa Kijiji cha Mkombe Kata ya Kabwe wilayani Nkasi, John Mwipungi (30), amenusurika kifo baada ya kupambana na mamba kwa zaidi ya saa moja.

Mwipungi akikumbana na mkasa huo alipokwenda mtoni kunawa miguu baada ya kutoka shambani.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 11 baada ya Mwipungu kufika mtoni  kisha kuanza kunawa miguu kutoa tope baada ya kutoka katika shamba lake alikokuwa aking’oa majani katika  mpunga.

Diwani wa Kabwe, Asante Lubisha, alisema majeru huyo alifika mtoni hapo na kuanza kunawa huku akiwa ameinama bila kuona kama kuna mamba katika eneo hilo.

Alisema wakati akiendelea kunawa miguu, ghafla aliibuka mamba mkubwa na kumvutia ndani ya mto, lakini kwa kuwa alikuwa anajua  kuogelea alipambana naye ndani ya maji.

Alisema ujuzi wa kuogelea ulimsaidia Mwipungi kwa sababu  aliamua kuvutana na mambo huyo eneo ambalo lina kina kirefu, hali iliyosababisha mamba huyo kushindwa kumuua na  ilichukua saa nzima kupambana majini huku akipiga kelele za kuomba msaada.

Diwani huyo alisema Mwipungi alijeruhiwa na mamba huyo katika mguu wake wa kulia.

Aliongeza kuwa kutokana na kelele alizokuwa akipiga za kuomba msaada, wanakijiji walifika na kumtoa majini akiwa amejeruhiwa kisha kumkimbiza katika Zahanati ya Kabwe kupatiwa matibabu ya jelaha la mguu.

Diwani huyo alisema wananchi wamekuwa wakiuawa na mamba katika mto huo na kuwa mwaka jana mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kabwe wa darasa la sita aliliwa na mamba wakati  akivuka katika mto Mkombe.

Alisema Kijiji cha Kabwe kimapakana na Pori la Akiba la Lwafi, hali inayosababisha wanyama wa hatari kama mamba, tembo, viboko na nyati kuingia kijijini hapo, hivyo kuhatarisha maisha ya wakazi wa kijiji hicho.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kabwe, Gwira Aron,  alisema majeruhi huyo alipatiwa matibabu na anaendelea vizuri.



Sanchez rasmi Man United



Alexis Sanchez amekubali kujiunga na Manchester United, hii sasa ni rasmi. Kikubwa kinachosubiriwa ni uamuzi wa kiungo Henrikh Mkhitaryan ambaye Arsenal inamtaka kama sehemu ya mauzo ya Sanchez.

Mkhitaryan alionekana kuwa anasita kujiunga na Arsenal lakini yuko katika hatua za mwisho kwa kuwa Kocha Jose Mourinho ameonekana kumruhusu aondoke.

Katika makubaliano, Sanchez amekubali kuwa Shetani Mwekundu kwa dili la miaka minne na nusu likiwa na thamani ya pauni milioni 14 kwa kila msimu.


Rais Magufuli amteua Dk Mwinuka kuwa Mkurugenzi wa Tanesco



Dar es Salaam.Rais  John Magufuli amemteua Dk Titus Mwinuka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania(Tanesco).

Kabla ya Utendaji huu Dk Mwinuka alikuwa akikaimu Nafasi hiyo.

Awali Dk Mwinuka alikuwa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).

Na pia alikuwa ni Mkuu wa Idara ya Mekanika na Uhandisi wa Viwanda Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

TFF yaishukia Yanga madai kuibeba Simba



OFISA WA HABARI WA TFF, CLIFFORD NDIMBO.

BAADA ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, kutoa malalamiko kuhusiana na matumizi ya Uwanja wa Taifa, Shirikisho la Soka Nchini (TFF) limetoa ufafanuzi kuhusiana na matumizi ya uwanja huo unaomilikiwa na serikali.

Yanga kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Boniface Mkwasa, ilisema kuwa TFF inaependelea Simba na kuipanga itumie Uwanja wa Taifa na wao ikiwapangia mechi zao kwenye Uwanja wa Uhuru.

Ofisa wa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, alisema jana katika taarifa yake kuwa Bodi ya Ligi ndiyo inayosimamia ligi na hupanga mechi kwa kuzingatia viwanja vilivyochaguliwa na klabu.

Ndimbo alisema katika taarifa yake kuwa katika upangaji wa ratiba hizo pamoja na viwanja, Kaimu Mwenyekiti wa Yanga ambaye ni Mwenyekiti wa klabu hiyo ni mmoja wa watendaji wa bodi hivyo hakuna suala la upendeleo kwenye upangaji wa matumizi wa Uwanja wa Taifa.

"TFF hatuamini kama Mkwasa anaweza kuzungumza maneno hayo kwa sababu anaujua utaratibu na anafahamu kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Yanga (Clement Sanga) ndiye Mwenyekiti wa Bodi ambaye angempa sababu kwa nini Simba wameruhusiwa kucheza kesho (leo) na Yanga wataruhusiwa kucheza mechi ijayo," ilisema sehemu ya taarifa.

Afisa huyo aliongeza kuwa TFF inasisitiza kufuatwa na kuheshimiwa kwa kanuni na taratibu za mpira wa miguu huku ikiendelea kufanya kazi kwa karibu na Yanga kwenye mambo mbalimbali na kuhakikisha inaisaidia kukabiliana na changamoto zinazotokea kwenye klabu hiyo.

Nafasi za kazi leo Jan 18

Waombolezaji wasambaratika baada ya mtu aliyedhaniwa amekufa kuibukia msibani


Kenya: Wakazi wa kijiji cha Marindi huko Kaunti ya Migori walipaniki na kuchanganyikiwa baada mwanaume wa miaka 35 ambaye aliaminika kuwa amefariki kuibukia msibani nyumbani kwake ghafla

Familia ya mwanaume huyo walikuwa wakimalizia mipango ya mazishi ndipo Okelo Nyamwaga alipojitokeza

Kufika kwake huko kusikotarajiwa kulileta hofu na furaha katika familia yake na marafiki na waombolezaji wengine kukimbia

Nyamwaga alikuwa amepotea kwa miezi miwili na familia yake ilipoteza matumaini ya kumpata akiwa hai

Wiki moja iliyopita marafiki wa Nyamwanga walisema mwili wake ukiwa umeharibika ulikuwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Migori

Mwili huo uliokotwa mtoni ukiwa umeharibika na kupelekwa mochwari


Kimbitor kugombea Ubunge jimbo la Kinondoni



Dar es Salaam. Diwani wa kata ya Hananasifu (Chadema), Ray Kimbitor amepitishwa na mkutano mkuu wa wilaya ya Kinondoni kugombea ubunge jimbo la Kinondoni.

Akitangaza matokeo hayo jana usiku mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kinondoni, Waziri Muhunzi amesema matokeo hayo watayawasilisha Kamati Kuu Taifa ya chama hicho kwa ajili ya kupata baraka.

Amesema Kimbitor amepata kura 40 na kuwashinda wagombea wengine sita.

Amesema wajumbe wa mkutano huo walikuwa 102 na kura zilizoharibika ni tano.

“Kimbitor amepata kura 40 na kufuatiwa na Mustapher Muro (diwani Kinondoni) aliyepata kura 33,” amesema.

Amesema Rose Moshi amepata kura 5, Nicolas Mkwama kura 16, David Asey kura 2, Moza Ally kura moja huku Juma Uloleulole ambaye ni diwani kata ya Kijitonyama akipata kura sifuri.

Hata hivyo, jana Katibu wa Mambo ya Nje na Itifaki wa Chadema, John Mrema alilieleza Mwananchi kuwa chama kingetoa msimamo huo jana baada ya kuunda kamati ndogo kufanya utafiti, lakini akasema Chadema haikutoa baraka za kufanyika kwa mchakato wa ndani wa kuchukua fomu na kupitisha wagombea.

Beki wa Liverpool ahukumiwa baada ya kumpiga mpenzi wake



Beki wa Liverpool ya England ambaye msimu wa 2016/2017 alikuwa akiichezea Burnley kwa mkopo Jon Flanagan amehukumiwa baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga mpenzi wake.

Jon Flanagan amekutwa na hatia baada ya mahakama jijini Liverpool kujiridhisha na ushahidi, hivyo amehukumiwa saa 40 za kufanya kazi bila malipo na miezi 12 ya kufanya shughuli za kijamii.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 25 alitenda kosa hilo kwa kumpiga Ms Wall ambaye ndio mpenzi wake December 22 wakiwa mtaa wa Duke jijini Liverpool.

Snura afunguka kuhusu kupigwa vibuti



MSANII wa filamu Bongo, Snura Mushi amesema kuwa, japo amekuwa akionekana kulalamika kuhusu masuala ya mapenzi, ukweli ni kwamba kinachomuuma ni kutompata mwanaume stahiki kwake, lakini hajawahi kuachwa, huwa anaacha.

Snura alifunguka hayo kutokana na kuibuka minong’ono ya mara kwa mara kuwa huenda anaongoza kwa kupewa vibuti kwenye mapenzi ndomana hachoki kulalamika kuwa na stress za mahusiano, jambo ambalo amelipinga vikali.

“Nani kakudanganya huwa naachwa hiyo haijawahi kutokea, nikiona mtu haeleweki huwa najiengua mwenyewe sisubiri anipasue kichwa changu, hivyo kinachoniliza ni kutopata mtu sahihi kwangu na siyo kuachwa na wanaume,”alisema.

Wednesday, 17 January 2018

BLT: What Holds Women Back? - BBC News

BLT: What Holds Women Back? - BBC News



Dozens of women describe abuse by ex-doctor Larry Nassar - BBC News

Dozens of women describe abuse by ex-doctor Larry Nassar - BBC News



US senator to Trump official: Your amnesia is complicity - BBC News

US senator to Trump official: Your amnesia is complicity - BBC News

Tanzia: Johari amefiwa na Mama yake mzazi


Muigizaji wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’.

Muigizaji wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amepata pigo kwa kuondokewa na mama yake mzazi. Mungu ailaze roho ya mama Johari mahala pema peponi, Amina.