Wednesday, 13 December 2017

Ushindi wa CCM watenguliwa na Mahakama



Mahakama ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara imetengua ushindi wa CCM wa nafasi ya mwenyekiti wa Kitongoji cha Sola kilichopo Kata ya Mutuka na kuamuru uchaguzi urudiwe.

Mgombea wa CCM alipita bila kupingwa baada ya mgombea wa Chadema kuenguliwa katika mchakato wa uchaguzi.

Hakimu John Shao akitoa hukumu ya kesi namba 1/2017 jana Jumanne Desemba 12,2017ameamuru uchaguzi ufanyike upya kwa nafasi hiyo.

Kesi hiyo ilifunguliwa na mgombea uenyekiti wa kitongoji hicho (Chadema), Vincent Slaa akipinga kuenguliwa na kamati ya rufaa ya uchaguzi ya wilaya hiyo. Aliwakilishwa na wakili Tadey Lister.

Hakimu Shao amesema Mahakama inakubaliana na pingamizi lililowekwa na Slaa kwamba alienguliwa kwenye mchakato wa uchaguzi bila sababu za msingi, hivyo Sagwale wa CCM akapitishwa bila kupingwa kwa nafasi ya mwenyekiti wa kitongoji.

Amesema Slaa aliondolewa kwenye mchakato wa uchaguzi uliofanyika Aprili 29,2017 na kamati ya rufaa ya uchaguzi Wilaya ya Babati.

Hakimu Shao ameamuru uchaguzi wa nafasi hiyo urudiwe na upande wa wadaiwa unapaswa kulipa gharama za kuendesha kesi hiyo.

"Kamati ya rufaa ya uchaguzi ya Wilaya ya Babati haikutenda haki ilipoondoa jina la Slaa kwenye uchaguzi, hivyo Mahakama inatengua nafasi ya Sagwale aliyepitishwa bila kupingwa na kuamuru uchaguzi ufanyike upya," alisema hakimu Shao.

Wadaiwa wengine kwenye kesi hiyo ni kamati ya rufaa ya uchaguzi, msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa kata ya Mutuka na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo.

Mbunge wa Babati Mjini (Chadema), Pauline Gekul ametoa shukrani kwa Mahakama kwa kutenda haki kwa kuwa mgombea wa chama hicho aliondolewa kwenye mchakato huo kwa kuonewa.

"Mgombea wa CCM alipitishwa bila kupingwa sasa turudi uwanjani ili nafasi hiyo ipate mwenyewe kwa jasho na kwa halali kupitia kura za wananchi," amesema Gekul.

Aliyekuwa mwenyekiti wa kitongoji hicho, Sagwale alisema wananchi wa eneo hilo wana imani naye kwa kuwa muda mfupi aliowaongoza wamempa ushirikiano wa kutosha.

Pep Gurdiola awaomba radhi Manchester United “kinafiki”



Baada ya mchezo kati ya Manchester United na Man City mwishoni mwa wiki iliyopita, inadaiwa kuliibuka fujo kubwa katika eneo la kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo la uwanja wa Old Traford.

Chanzo cha fujo hiyo kinatajwa kwamba ni kitendo cha Manchester City kushangilia sana na kupiga kelele nyingi, jambo hilo liliwakera baadhi ya watu wa United akiwemo Jose Mourinho na mvutano ulianzia hapo.

Pep Gurdiola ambaye ndiye aliwaongoza vijana wake kuichapa United bao 2 kwa 1 amesema hawakuwa na nia ya kuwakera Manchester United kwani wao walikuwa wakishangilia tu lakini kama wamekereka anawaomba msamaha.

“Lakini na wao kuna michezo ambayo walishinda na wakashangilia sana, sisi tumeshinda Derby na tulipaswa kufurahia hilo na kama limewaudhi tunaomba radhi kwa kila mtu wa United aliyekereka” alisema Pep.

Pep Gurdiola amesisitiza kwamba akama timu ikifanya vizuri uwanjani na ikaibuka na ushindi kinachofuatia ni kwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo ambapo watu wanakwenda kufurahia walichofanya.

Tayari shirikisho la soka nchini Uingereza FA limeiandikia Manchester United barua kuhusiana na tukio hilo ambapo inadaiwa kwamba kulikuwa na vitendo vya urushwaji wa chupa za maji na maziwa kati ya pande hizo mbili.

Hukumu ya Simba na Yanga kujulikana leo



 

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa ngazi ya klabu msimu wa 2017/18 Simba na Yanga, watajulikana leo ambapo droo ya kupanga hatua ya awali ya michuano hiyo itafanyika jijini Cairo, Misri.

Yanga ambao ni mabingwa wa Tanzania Bara wanasubiri kuwajua wapinzani wao katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na wakati Simba SC wao wakisubiri kujua wataanza na nani katika Kombe la Shirikisho.

Michuano hiyo huandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Tayari kamati kuu ya utendaji ya shirikisho hilo imeshaanza vikao vya awali tangu Disemba 11 mwaka huu ikijadili maboresho mbalimbali yanayohitajika kufanyika kwenye michuano hiyo.

MKutano huo unaojulikana kama (CAF interclubs competitions think-tank 2017) unatarajia kutoka na uamzi wa juu ya nini kifanyike ili kuboresha michuano hiyo na hii huenda ikaangukia kwenye kubadili muundo wa mashindano hayo.

Tayari klabu zote za Simba na Yanga zimeshawasilisha majina ya usajili wa wachezaji wao kwa ajili ya michuano ya klabu bingwa na Kombe la Shirikisho Afrika. Mabingwa watetezi wa klabu bingwa ni Wydad Casablanca ya Morocco wakati mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho ni TP-Mazembe ya DR Congo.

Dirisha la Helikopta ya Jeshi la Marekani Yaanguka Shuleni Japan



Sehemu ya ndege ye jeshi la Marekani imeanguka kwenye shule katika kisiwa cha Okinawa nchini Japan na kuzua upya misukosuko na watu wa eneo hilo.

Sehemu hiyo ya dirisha ilianguka kwenye uwanja wa shule na kusabisha majeraha madogo kwa mwanafunnzi mmoja.

Katika miaka ya hivi karibuni, ajali kadha na visa vya uhalifu vimesababisha kuwepo upinzani dhidi ya kambi hiyo ya Marekani.

Jeshi la Marekani lilithibitisha kuwa dorisha kutoka moja ya helikopta zake ilianguka kwenye uwanja wa michezo wa shule iliyo nje ya kambi ya yake ya jeshi la wanahewa.

"Tanzania imeshaonekana kuwa ni kichaka cha fedha za kigeni" - JPM

"Tanzania imeshaonekana kuwa ni kichaka cha fedha za kigeni" - JPM

Audio | S Kide – 900 Itapendeza | Mp3 Download

Audio | S Kide – 900 Itapendeza | Mp3 Download

Audio | S Kide – 900 Itapendeza | Mp3 Download

  DOWNLOAD

Alichoandika Zari kwenye Birthday ya Marehemu Ivan

Alichoandika Zari kwenye Birthday ya Marehemu Ivan


Spidi ileile kuileta Treni ya Umeme Tanzania, Prof. Mbarawa kagoma kulala

Spidi ileile kuileta Treni ya Umeme Tanzania, Prof. Mbarawa kagoma kulala


LIVE: "Tanzania imeshaonekana kuwa ni kichaka cha fedha za kigeni"

LIVE: "Tanzania imeshaonekana kuwa ni kichaka cha fedha za kigeni"

TBC1: Waliosamehewa na JPM, Sasa Wamuomba Mtaji!

TBC1: Waliosamehewa na JPM, Sasa Wamuomba Mtaji!

Mazoezi ya Yanga Yashusha Majembe Mawili ya Kimataifa


Mazoezi ya Yanga Yashusha Majembe Mawili ya Kimataifa


Afanya sherehe ya kuagwa kabla hajafariki


Satoru Anzaki akiwa kwenye karamu hiyo

Mfanyabiashara mmoja nchini Japan ambaye anaugua saratani na anatarajiwa kufariki karibuni aliwashangaza watu baada ya kuandaa karamu kubwa ya kuaga.

Satoru Anzaki aliwaalika wageni karibu 1,000 wakiwemo marafiki zake, watu waliosoma naye, washirika wake wa kibiashara na wafanyakazi wake.

Satoru, 80, ambaye ni mkuu wa zamani wa kampuni ya kuunda mashine ya Komatsu alipatikana na saratani ya kibofu cha nyongo Oktoba.

"Nimeridhika kwamba niliweza ksuema 'asante' kwa watu niliokutana nao maishani," aliwaambia wanahabari baada ya sherehe hiyo.

"Kwa kuwa nilitaka kufurahia kabisa sehemu ndogo ya maisha niliyobaki nayo, nimeamua nisipokee matibabu baada ya kuzingatia madhara ya tiba," alisema.

Alitangaza mpango wake wa kufanya sherehe hiyo kupitia tangazo gazetini, taarifa ambazo zilisambazwa sana mtandaoni watu wakitaniana kuhusu ingelikuwa wao wangewaalika nani.

Satoru alikodisha chumba katika hoteli moja Tokyo na akaipamba kwa picha za kumbukumbu ya maisha yake.


Marekani iko tayari kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini


Rex Tillerson

Marekani iko tayari kwa mazungumzo wakati wowote na Korea Kaskazini bila ya masharti yoyote, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani Rex Tillerson amesema.

Taaarifa yake ilionekana kuwa tofauti na msimamo wa awali wa Marekani kuwa Korea Kaskazini ni lazima iharibu zana zake kabala ya mazungummzo yoyote kufanyika

Lakini saa chache baadaye Ikulu wa White House ilisema msimamo wake Trump kwa Korea Kaskazini haujabadilika.

Hatua ya Korea Kaskazini ya kuunda zana za nyuklia imesababisha Marekani kuongoza vikwazo vikubwa dhidi ya nchi hiyo.

Jordan yaitaka Marekani isiutambue Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel
Kando na hilo mkuu wa masuala ya siasa wa Umoja wa Mataifa ambaye hivi karibu alizuru Korea Kaskazini aliwaambia waandishi wa habari kuwa maafisa wa Korean Kaskazini wanaamini kuwa ni muhimu kuzuia vita.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Korea Kaskazini umeharibika kufuatia majaribio ya hivi karibuni ya mabomu ya nyuklia na makombora na kuwepo vita vya Maneno kati ya rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.

Akizungumza kwenye mkutano wa baraza la nchi za Atlantic siku ya Jumanne, Bw Tillerson alisema kuwa Marekani haiwezi kukubali Korea Kaskazini kujihami kwa silaha za nyuklia.