Ubishani wa kisheria umeibuka katika kesi inayowakabili Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga baada ya hoja ya wakili wa washtakiwa, Peter Kibatala kutaka kuanza na shahidi wa kwanza ambaye ni Mkuu Upelelezi Mkoa wa Mbeya, kupingwa na Jamhuri.
Mabishano kati ya pande hizo mbili yametokea leo Februari 8, 2018 na kusababisha Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite kuahirisha kesi kwa muda na kuwaita mawakili wa pande zote na kwenda nao ofisini kwake ili wakajadiliane.
Awali, Kibatala aliieleza Mahakama hiyo kwamba wapo tayari kuendelea na utoaji ushahidi na ataanza na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya (RCO).
“Mmh! Naona kama kuna ukakasi, eti hakimu upande wa Serikali?” amehoji hakimu Mteite.
Wakili wa Jamhuri, Joseph Pande alisimama na kupinga kwa shahidi huyo kuwa wa kwanza huku akisisitiza kwamba katika utetezi huo, watuhumiwa ndiyo wanaopaswa kuanza.
"Kimsingi anayetakiwa kuanza ni mtuhumiwa kujitetea na kama atakuwa na mashahidi ndipo wataitwa hao mashahidi wake. Sasa hii itakuwa ni jambo la ajabu kutokea kama ataanza shahidi tofauti na mhusika mkuu (mshtakiwa),” amesema Pande.
Kibatala alisimama na kumpinga Pande akidai hakuna kifungu cha sheria kinachozuia kufanya hivyo na wala hakuna athari yoyote.
“Hapa tutakuwa tunapoteza muda bure. Hakuna katazo lolote kisheria,” amesema Kibatala.
Kutokana na mabishano hayo Mteute amewaita mawakili hao kwa ajili ya kujadiliana, hivyo kuahirisha kesi hiyo kwa muda.
Sugu na Masonga wanakabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli ambayo wanadaiwa kuitoa Desemba 30, 2017
Kampeni ya kuwataka wanaume waongozane na wenza wao wajawazito kiliniki kwa ajili ya kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu afya ya uzazi sambamba na uzazi wa mpango, inaelekea kukwama katika jiji la Arusha na hivyo kutishia kinamama kukosa matibabu.
Jaji Mkuu nchini Kenya David Maraga, ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume cha Sheria na Katiba ya nchi hiyo katika kukabiliana na upinzani.
Usiku wa kuamkia January 29 mwaka huu label ya WCB walimtambulisha msanii mpya ambaye ni Mbosso aliyekuwa Yamoto Band.
Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond amesema mazungumzo katika kesi yake Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa watoto kati yake na mwanamitindo Hamisa Mobeto, imekwenda vizuri.
Afrika Kusini. Kamati ya Bunge ya Chama cha ANC (caucus) inakutana mchana huu katika kikao cha siri ambacho hata hivyo ajenda zake hazikuwekwa wazi kwa waandishi wa habari.
Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo imepunguza gharama za kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kitaifa na kimataifa kwa asilimia 27.5.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi amekiri kuwepo kwa mgogoro wa wananchi na Jeshi la Kujenga Taifa (JWTZ) eneo la Kisakasaka.


