Ngoma, Kamusoko waondolewa kikosi cha Yanga kesho
Donald Ngoma (kushoto) akifanya yake.
Kocha wa Yanga, George Lwandamina, raia wa Zambia, amewatoa katika mipango yake nyota hao kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City.
Kamusoko anayecheza nafasi ya kiungo na Ngoma ambaye ni straika, wote kwa sasa ni majeruhi na tayari kocha huyo amewatafutia mbadala wao ambao watacheza mechi hiyo.
Daktari wa Yanga, Edward Bavu, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, wachezaji hao bado wana matatizo kwani Kamusoko anaumwa kifundo cha mguu na Ngoma anasumbuliwa na nyama za paja.
“Kamusoko na Ngoma wameondolewa katika mipango ya kocha kuelekea mechi ya wikiendi hii, maana hawataweza kuwa sawa kwa siku moja,” alisema Bavu.
Kwa wiki nzima, wawili hao hawakufanya mazoezi ya maandalizi ya mchezo wao wa kesho na huenda
wakaonekana tena uwanjani mwezi ujao kama watakuwa fiti.
Mara ya mwisho kwa nyota hao kuonekana uwanjani, ilikuwa kwenye mechi ya ligi kuu msimu huu dhidi ya Mtibwa Sugar, iliyopigwa Septemba 30 kwenye Uwanja wa Uhuru na kumalizika kwa suluhu
No comments:
Post a Comment