Friday, 12 January 2018

Naibu waziri wa Ujenzi ameiagiza Temesa kupeleka Kivuko



NAIBU Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi,  Elias Kwandikwa, ameuagiza uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) makao makuu kusaini haraka mkataba kwa mkandarasi atakayebeba kivuko kipya  kutoka eneo kinapotengenezwa wilayani Pangani mkoani Tanga hadi mkoani Lindi.

Taarifa ya wizara hiyo ilimkariri Kwandikwa akitoa agizo hilo wakati akizungumza baada ya kukagua maegesho ya kivuko hicho ambacho alisema kinatarajiwa kutoa huduma za usafiri kutoka Lindi Mjini-Kitunda mkoani humo, na kuwahakikishia wananchi kutegemea kupata huduma nzuri za usafiri kwani ujenzi wa kivuko na  maegesho  yake kwa sasa umefika katika hatua nzuri.

“Naagiza mamlaka husika kusaini haraka mkataba kwa mkandarasi atakayebeba kivuko hiki kutoka Tanga hadi hapa ili wananchi waone kwamba kivuko kimefika na kipo tayari kwa ajili ya kutoa huduma,” Naibu Waziri Kwandikwa alikaririwa akisema.

Aidha, Naibu Waziri huyo aliridhishwa na ujenzi wa maegesho hayo ambayo kwa sasa ujenzi wake umebakia asilimia 10, hivyo kutarajiwa kukamilika muda wowote.

Katika hatua nyingine, Kwandikwa, alitembelea na kukagua uwanja wa ndege wa Lindi ambapo alisema Serikali inaendelea na mpango wake wa kuboresha viwanja vya ndege nchini ili kuimarisha huduma katika usafiri wa anga.

Alifafanua kuwa Serikali kupitia mwaka wa fedha 2018/19 licha ya kuwa na mpango wa kuboresha uwanja huo, pia itaboresha uwanja wa ndege wa Kilwa Masoko lengo ni kuleta maendeleo kwa wananchi.

Meneja wa Temesa mkoani Lindi, Greyson Maleko, alimhakikishia Naibu Waziri huyo kujipanga katika kuhakikisha wananchi wa Lindi wanapata huduma bora za kivuko.

Naye, Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani humo, Hamida Abdallah, aliipongeza na kuishukuru Serikali kwa kusogeza maendeleo kwa wananchi na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Kwandikwa alimaliza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo kwa kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake ili kujionea m

No comments:

Post a Comment