Kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Nike imevujisha kuwa huenda usajili wa nyota wa Liverpool na Brazil Phillipe Coutinho kwenda Barcelona umekamilika tayari.
Nike kupitia tovuti yao jana waliweka picha ya jezi ya Barcelona ya msimu huu yenye jina la Coutinho, huku wakiambatanisha na ujumbe unaoonyesha kuwa nyota huyo anatua Cam Nou kabla ya msimu kumalizika.
"Philippe Coutinho yuko tayari kuipamba Camp Nou'', Waliandika Nike ujumbe huo kwenye picha ya jezi za FC Barcelona za msimu huu 2017-18 iliyoandikwa jina la Coutinho.
Baadae Nike walifuta ujumbe huo baada ya mashabiki wa Liverpool kuanza kuishambulia kampuni hiyo kuwa inashinikiza mchezaji wao ahamie Barcelona kwa kuwa Nike wanaidhamini klabu hiyo ya Hispania.
Coutinho mwenye umri wa miaka 25 amefunga mabao saba na kutoa msaada wa mabao sita kwenye Ligi Kuu soka nchini Englanda msimu huu.
No comments:
Post a Comment